Isaya 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 12:1-6

Kushukuru Na Kusifu

112:1 Zek 14:20-21; Isa 25:1; 10:20; Ay 13:16; Za 71:21; 9:1Katika siku ile utasema:

“Nitakusifu wewe, Ee Bwana.

Ingawa ulinikasirikia,

hasira yako imegeukia mbali

nawe umenifariji.

212:2 Kut 15:2; Dan 6:23; Za 26:1; 118:14; Isa 17:10; 25:9; 26:4; Ay 13:15Hakika Mungu ni wokovu wangu;

nitamtumaini wala sitaogopa.

Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu.”

312:3 Yer 2:13; 17:13; Za 39:6; Yn 4:10, 14; 2Fal 3:17; Kut 15:25Kwa furaha mtachota maji

kutoka visima vya wokovu.

412:4 Za 80:18; 113:2; Hos 12:5; Kut 3:15; Isa 10:20; 24:15; Yer 10:7Katika siku hiyo mtasema:

“Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake;

julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,

tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

512:5 Kut 15:1; Za 98:1Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu,

hili na lijulikane duniani kote.

612:6 Za 78:41; Eze 39:7; Sef 3:14-17; Za 46:5; 98:4; Mwa 21:6; Isa 48:20; Zek 2:10Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”