Isaya 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 11:1-16

Tawi Kutoka Kwa Yese

111:1 Zek 6:12; Isa 9:7; Mdo 13:23; Ay 14:7; 2Fal 19:26-30; Isa 27:9; Ufu 5:5Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,

kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.

211:2 Mt 3:16; Yoe 2:28; Yn 16:13; Kut 28:3; Kol 2:3; Amo 3:10; Isa 32:15; 48:16Roho wa Bwana atakaa juu yake,

Roho wa hekima na wa ufahamu,

Roho wa shauri na wa uweza,

Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

311:3 Isa 33:6; Yn 7:24; 2:25naye atafurahia kumcha Bwana.

Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,

wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

411:4 Ufu 19:11; Za 72:2-4; Zek 14:12; 2The 2:8; Za 18:8; Isa 14:30; Ufu 19:11; Ay 5:16bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,

kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.

Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,

kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

511:5 Isa 25:1; Efe 4:16; Kut 12:11; 1Fal 18:46Haki itakuwa mkanda wake

na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.

611:6 Hos 2:18; Isa 65:25Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,

naye chui atalala pamoja na mbuzi,

ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,

naye mtoto mdogo atawaongoza.

711:7 Ay 40:15Ngʼombe na dubu watalisha pamoja,

watoto wao watalala pamoja,

na simba atakula majani makavu kama maksai.

811:8 Isa 65:20; 14:29; 30:6; 59:5Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,

naye mtoto mdogo ataweka mkono wake

kwenye kiota cha fira.

911:9 Hab 2:14; Hes 25:12; Za 98:2-3; Ay 5:23; 1Sam 17:46; Isa 19:21; 52:10Hawatadhuru wala kuharibu

juu ya mlima wangu mtakatifu wote,

kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana

kama maji yajazavyo bahari.

1011:10 Yn 12:32; Rum 15:10-12; Mdo 11:18; Za 116:7; Isa 60:5, 10; 32:17-18; Yer 6:16Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu. 1111:11 Mwa 10:22; Zek 10:10; Mik 7:12; Isa 66:19; 10:20; 19:24; Kum 30:4; Hos 11:11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi,11:11 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini.

1211:12 Yn 7:35; Sef 3:10; Eze 28:25; Za 20:5; Isa 14:2; 43:5; Yer 16:15; 31:10Atainua bendera kwa mataifa

na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni;

atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika

kutoka pembe nne za dunia.

1311:13 2Nya 28:6; Hos 1:11; Gal 3:28; Yer 3:18; Eze 16:22; 37:16-17, 22Wivu wa Efraimu utatoweka,

na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;

Efraimu hatamwonea Yuda wivu,

wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.

1411:14 Yoe 3:19; Sef 2:8-11; Yer 48:40; 2Nya 26:6; Amu 6:3; 11:14-18; Isa 25:3; Hes 24:18Watawashukia katika miteremko ya Wafilisti

hadi upande wa magharibi,

kwa pamoja watawateka watu nyara

hadi upande wa mashariki.

Watawapiga Edomu na Moabu,

na Waamoni watatawaliwa nao.

1511:15 Isa 19:16; 30:32; 7:20; Ufu 16:12; Kut 14:22, 29; Kum 11:10; Yer 50:38; Mwa 41:16Bwana atakausha

ghuba ya bahari ya Misri;

kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake

juu ya Mto Frati.

Ataugawanya katika vijito saba

ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.

1611:16 Kut 14:26-31; Yer 50:5; Isa 19:23; 35:8; 51:10; 62:10; Mwa 45:7Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wake

wale waliosalia kutoka Ashuru,

kama ilivyokuwa kwa Israeli

walipopanda kutoka Misri.