Isaya 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 10:1-34

110:1 Za 58:2; Isa 5:8Ole wao wawekao sheria zisizo za haki,

kwa wale watoao amri za kuonea,

210:2 Isa 3:14; 5:23; Kum 10:18; Ay 6:27; Isa 1:17kuwanyima maskini haki zao

na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa,

kuwafanya wajane mawindo yao

na kuwanyangʼanya yatima.

310:3 Isa 31:3; Hes 9:7; Lk 19:44; Ay 31:14; Za 59:5; Isa 13:6Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu,

wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali?

Mtamkimbilia nani awape msaada?

Mtaacha wapi mali zenu?

410:4 Mao 1:12; Yer 39:6; Isa 24:22; Nah 3:3; Zek 9:11; Isa 5:25; 63:10; Yer 30:24Hakutasalia kitu chochote,

isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka,

au kuanguka miongoni mwa waliouawa.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

Hukumu Ya Mungu Juu Ya Ashuru

510:5 Sef 2:13; Yer 50:23; 51:20; Isa 37:7; Eze 30:24-25; 2Fal 19:21; Isa 7:20; 14:25“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu,

ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!

610:6 Isa 9:17-19; 2Nya 28:9; Amu 6:4; Isa 5:29; 2Sam 22:43; Isa 37:26-27; Za 7:5Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu,

ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha,

kukamata mateka na kunyakua nyara,

pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.

710:7 Mwa 50:20; Mdo 4:23-28; Mik 4:12Lakini hili silo analokusudia,

hili silo alilo nalo akilini;

kusudi lake ni kuangamiza,

kuyakomesha mataifa mengi.

810:8 2Fal 18:24Maana asema, ‘Je, wafalme wote

si majemadari wangu?

910:9 2Nya 35:20; Mwa 14:15; 2Fal 17:6; Yer 49:24; Hes 13:21; 34:8; Amo 6:2; Mwa 10:10Je, Kalno hakutendwa kama Karkemishi?

Hamathi si kama Arpadi,

nayo Samaria si kama Dameski?

1010:10 2Fal 19:18Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu,

falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria:

1110:11 2Fal 19:13; Isa 36:18-20; 37:10-13je, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake

kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’ ”

1210:12 2Fal 19:7, 31; Isa 28:21; 2:8; Yer 50:18; 5:29; Isa 2:11; Eze 28:17; Za 18:27Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.” 1310:13 Kut 15:9; Eze 28:4; Dan 4:30; Kum 32:26-27; 8:17; Isa 47:7; 14:13-14Kwa kuwa anasema:

“ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili,

kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu.

Niliondoa mipaka ya mataifa,

niliteka nyara hazina zao,

kama yeye aliye shujaa

niliwatiisha wafalme wao.

1410:14 Oba 1:4; Hab 2:6-11; Ay 31:25; Yer 49:16; Isa 37:24-25; 2Fal 19:22-24Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota,

ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa;

kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa,

ndivyo nilivyokusanya nchi zote;

wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa

au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’ ”

1510:15 Rum 9:20-21; Isa 7:20; 45:9Je, shoka laweza kujigamba kuwa na nguvu zaidi

kuliko yule anayelitumia,

au msumeno kujisifu

dhidi ya yule anayeutumia?

Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua yeye aichukuaye,

au mkongojo ungemwinua mwenye kuutumia!

1610:16 Hes 11:33; Isa 17:14; Za 78:31; Isa 8:7; Yer 21:14Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari,

katika fahari yake moto utawaka

kama mwali wa moto.

1710:17 Ay 41:21; Isa 37:23; 2Sam 23:6; Isa 9:18; 31:9; Zek 2:5Nuru ya Israeli itakuwa moto,

Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto;

katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba

na michongoma yake.

1810:18 2Fal 19:23Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba

utateketeza kabisa,

kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo.

1910:19 Isa 21:12; 32:19; 17:6; 21:17; 27:13; Yer 44:28Nayo miti inayobaki katika misitu yake itakuwa michache sana

hata mtoto mdogo angeweza kuihesabu.

Mabaki Ya Israeli

2010:20 Isa 52:6; Zek 9:16; 2Fal 16:7; Eze 7:16; Isa 28:5; 2Nya 14:11; Isa 48:2; Yer 21:2Katika siku ile, mabaki ya Israeli,

walionusurika wa nyumba ya Yakobo,

hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga,

lakini watamtegemea kwa kweli

Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli.

2110:21 Sef 3:13; Mwa 45:7; Isa 6:13; 9:6Mabaki watarudi,10:21 Kiebrania ni Shear-Yashubu, pia 22. mabaki wa Yakobo

watamrudia Mungu Mwenye Nguvu.

2210:22 Rum 9:27-28; Yer 40:2; Dan 9:27; Isa 48:19; Yer 33:22; Isa 11:11Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani,

ni mabaki yao tu watakaorudi.

Maangamizi yamekwisha amriwa,

ni mengi tena ni haki.

2310:23 Isa 6:12; 28:22; Rum 9:27-28; Dan 9:25Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatekeleza

maangamizi yaliyoamriwa juu ya nchi yote.

2410:24 Za 87:5-6; Kut 5:14; Isa 7:4; 10:5Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Enyi watu wangu mkaao Sayuni,

msiwaogope Waashuru,

wanaowapiga ninyi kwa fimbo

na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.

2510:25 Isa 17:14; Dan 11:36; Za 30:5; Isa 29:17; Hag 2:6; Isa 24:21; 30:30Bado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma,

na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.”

2610:26 Isa 37:36-38; Kut 14:16; Isa 30:32; 9:4Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi,

kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu,

naye atainua fimbo yake juu ya maji,

kama alivyofanya huko Misri.

2710:27 Isa 9:4; 52:2; Law 26:13; Yer 30:8; Za 66:11; Isa 14:25; 47:6Katika siku hiyo mzigo wao utainuliwa kutoka mabegani mwenu,

na nira yao kutoka shingoni mwenu;

nira itavunjwa

kwa sababu ya kutiwa mafuta.

2810:28 1Sam 14:2; 13:2; Neh 11:31; Yos 1:11Wanaingia Ayathi,

wanapita katikati ya Migroni,

wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi.

2910:29 Yos 18:25; 1Sam 13:23; Amu 19:14; Isa 15:5Wanavuka kivukoni, nao wanasema,

“Tutapiga kambi huko Geba usiku kucha.”

Rama inatetemeka;

Gibea ya Sauli inakimbia.

3010:30 1Sam 25:44; Neh 11:32; 1Sam 25:44Piga kelele, ee Binti Galimu!

Sikiliza, ee Laisha!

Maskini Anathothi!

3110:31 Yos 15:31Madmena inakimbia;

watu wa Gebimu wanajificha.

3210:32 1Sam 21:1; Za 9:14; Yer 6:23; Ay 15:25Siku hii ya leo watasimama Nobu;

watatikisa ngumi zao

kwa mlima wa Binti Sayuni,

kwa kilima cha Yerusalemu.

3310:33 Isa 2:13; 5:15; 18:5; Amo 2:9; Kut 12:2Tazama, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

atayakata matawi kwa nguvu kuu.

Miti mirefu sana itaangushwa,

ile mirefu itashushwa chini.

3410:34 Nah 1:12; Zek 11:2; 2Fal 19:23; Mwa 49:24; Za 93:4; Isa 33:21Atakata vichaka vya msitu kwa shoka;

Lebanoni itaanguka mbele zake yeye Mwenye Nguvu.