Hosea 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 8:1-14

Israeli Kuvuna Kisulisuli

18:1 Kum 28:49; Yer 4:13; 11:10; Hos 4:6; 6:7; Hes 10:2; Eze 33:3“Wekeni tarumbeta midomoni mwenu!

Tai yuko juu ya nyumba ya Bwana

kwa sababu watu wamevunja Agano langu,

wameasi dhidi ya sheria yangu.

28:2 Za 78:34; Mt 7:21Israeli ananililia,

‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’

38:3 Mt 7:23; Tit 1:16Lakini Israeli amekataa lile lililo jema,

adui atamfuatia.

48:4 Hos 2:8; 13:1-2, 10; Mt 7:21; 1Fal 12:16-20; 2Fal 15:13, 17, 25Wanaweka wafalme bila idhini yangu,

wamechagua wakuu bila kibali changu.

Kwa fedha zao na dhahabu

wamejitengenezea sanamu kwa ajili

ya maangamizi yao wenyewe.

58:5 Hos 10:5; Yer 13:27; Hos 8:6Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama!

Hasira yangu inawaka dhidi yao.

Watakuwa najisi mpaka lini?

68:6 Yer 16:20; Hos 14:3; Kut 32:4Zimetoka katika Israeli!

Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu.

Atavunjwa vipande vipande,

yule ndama wa Samaria.

78:7 Ay 4:8; Gal 6:8; Hos 2:9; 7:9; 10:11-12; Mit 22:8; Isa 17:11; 66:15“Wanapanda upepo

na kuvuna upepo wa kisulisuli.

Bua halina suke,

halitatoa unga.

Kama lingetoa nafaka,

wageni wangeila yote.

88:8 Yer 22:28; 51:34; 2Fal 17:6; Yer 22:28; 48:38Israeli amemezwa;

sasa yupo miongoni mwa mataifa

kama kitu kisicho na thamani.

98:9 Yer 2:18; 22:20; Mwa 16:12; Eze 23:5; Hos 5:13Kwa kuwa wamepanda kwenda Ashuru

kama punda-mwitu anayetangatanga peke yake.

Efraimu amejiuza mwenyewe

kwa wapenzi.

108:10 Eze 16:37; 22:20; Yer 42:2; Dan 2:34Ingawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa,

sasa nitawakusanya pamoja.

Wataanza kudhoofika chini ya uonevu

wa mfalme mwenye nguvu.

118:11 Hos 10:1; 12:11“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi

kwa ajili ya sadaka za dhambi,

hizi zimekuwa madhabahu

za kufanyia dhambi.

128:12 Hos 8:1; Kum 4:6; Za 119:18; 147:19-20Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi

kuhusu sheria yangu,

lakini wameziangalia

kama kitu cha kigeni.

138:13 Yer 6:20; 7:21; Neh 9:13-14; Hos 4:9; 9:3-9; Ay 21:14Wanatoa dhabihu nilizopewa mimi

nao wanakula hiyo nyama,

lakini Bwana hapendezwi nao.

Sasa ataukumbuka uovu wao

na kuadhibu dhambi zao:

Watarudi Misri.

148:14 Kum 32:18; Isa 17:10; Yer 5:17; Amo 2:5; 1Fal 12:31; Hos 2:13; Za 95:6Israeli amemsahau Muumba wake

na kujenga majumba ya kifalme,

Yuda amejengea miji mingi ngome.

Lakini nitatuma moto kwenye miji yao

utakaoteketeza ngome zao.”