Hosea 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 7:1-16

17:1 Eze 24:13; Hos 4:2; 6:4; Kut 22:2; Sef 2:7; Za 126:1kila mara nilipotaka kumponya Israeli,

dhambi za Efraimu zinafichuliwa

na maovu ya Samaria yanafunuliwa.

Wanafanya udanganyifu,

wevi huvunja nyumba,

maharamia hunyangʼanya barabarani,

27:2 Yer 14:10; 44:21; Mit 5:22; Yer 2:19; 4:18; Hos 8:13; Ay 35:15lakini hawafahamu kwamba

ninakumbuka matendo yao yote mabaya.

Dhambi zao zimewameza,

ziko mbele zangu siku zote.

37:3 Rum 1:32; Yer 28:1-4; Mik 7:3; Hos 4:2; 10:13“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,

wakuu wao kwa uongo wao.

47:4 Yer 9:2Wote ni wazinzi,

wanawaka kama tanuru

ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea

kuanzia kukanda unga

hadi umekwisha kuumuka.

57:5 Isa 28:1, 7; Za 1:1Katika sikukuu ya mfalme wetu

wakuu wanawaka kwa mvinyo,

naye anawaunga mkono wenye mizaha.

67:6 Za 21:9Mioyo yao ni kama tanuru,

wanamwendea kwa hila.

Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,

wakati wa asubuhi inalipuka

kama miali ya moto.

77:7 Za 14:4; Sef 1:6; Isa 9:13; Hos 13:10Wote ni moto kama tanuru;

wanawaangamiza watawala wao.

Wafalme wake wote wanaanguka,

wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.

87:8 Za 106:35; Hos 5:13; 7:11“Efraimu anajichanganya na mataifa;

Efraimu ni mkate ambao haukuiva.

97:9 Isa 1:7; Hos 8:7Wageni wananyonya nguvu zake,

lakini hafahamu hilo.

Nywele zake zina mvi hapa na pale,

lakini hana habari.

107:10 Hos 5:5; Isa 9:13Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,

lakini pamoja na haya yote

harudi kwa Bwana Mungu wake

wala kumtafuta.

117:11 Mwa 8:8; Hos 9:3; 11:11; Mao 5:6; Yer 2:18“Efraimu ni kama hua,

hudanganywa kwa urahisi na hana akili:

mara anaita Misri,

mara anageukia Ashuru.

127:12 Eze 12:13; 32:3; Law 26:14Wakati watakapokwenda,

nitatupa wavu wangu juu yao;

nitawavuta chini waanguke

kama ndege wa angani.

Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,

nitawanasa.

137:13 Hos 9:12, 17; Yer 14:10; 51:9; Eze 34:4-6; Mt 23:37; Za 116:11Ole wao, kwa sababu

wamepotoka kutoka kwangu!

Maangamizi ni yao

kwa sababu wameniasi!

Ninatamani kuwakomboa,

lakini wanasema uongo dhidi yangu.

147:14 Ay 35:9; Yer 3:10; Hos 4:10; 13:16; Za 78:34-37; Amo 2:8Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,

bali wanaomboleza vitandani mwao.

Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,

lakini hugeukia mbali nami.

157:15 Za 2:1; 140:2; Nah 1:9; Hos 11:3Niliwafundisha na kuwatia nguvu,

lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.

167:16 Za 78:57; Eze 23:32; Hos 9:3; 11:5; Mal 3:14Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,

wako kama upinde wenye kasoro.

Viongozi wao wataanguka kwa upanga

kwa sababu ya maneno yao ya jeuri.

Kwa ajili ya hili watadhihakiwa

katika nchi ya Misri.