Hosea 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 6:1-11

Israeli Asiye Na Toba

16:1 Ay 16:9; Kum 32:39; Mao 3:11; Ay 5:18; Isa 10:20; 19:22; Hes 12:13; Yer 3:22; 30:17; Hos 14:4“Njooni, tumrudie Bwana.

Ameturarua vipande vipande

lakini atatuponya;

ametujeruhi lakini

atatufunga majeraha yetu.

26:2 Mit 2:1-9; Za 80:18; 30:5; Mt 16:21Baada ya siku mbili atatufufua;

katika siku ya tatu atatuinua,

ili tuweze kuishi mbele zake.

36:3 Ay 4:3; 29:23; Yoe 2:23; Hos 12:6; Za 72:6; Hos 11:10Tumkubali Bwana,

tukaze kumkubali yeye.

Kutokea kwake ni hakika kama vile

kuchomoza kwa jua;

atatujia kama mvua za masika,

kama vile mvua za vuli

ziinyweshavyo nchi.”

46:4 Hos 11:8; 7:1; 13:3“Nifanye nini nawe, Efraimu?

Nifanye nini nawe, Yuda?

Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao.

56:5 Yer 5:14; 23:29; Ebr 4:12; Yer 1:9-10Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande

kwa kutumia manabii wangu;

nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,

hukumu zangu zinawaka

kama umeme juu yenu.

66:6 1Sam 15:22; Mk 12:33; Yer 4:22; Hos 2:20; Mit 21:3; Mt 12:7; Za 40:6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,

kumkubali Mungu zaidi

kuliko sadaka za kuteketezwa.

76:7 Mwa 9:11; Yer 11:10; Hos 5:7; 8:1Wamevunja Agano kama Adamu:

huko hawakuwa waaminifu kwangu.

86:8 Hos 12:11Gileadi ni mji wenye watu waovu,

umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

96:9 Yer 5:30-31; Eze 22:9; Za 10:8; Hos 4:2; Yer 7:9-10Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,

ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;

wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,

wakifanya uhalifu wa aibu.

106:10 Yer 5:31; Eze 23:7; Yer 23:14; Hos 5:3Nimeona jambo la kutisha

katika nyumba ya Israeli.

Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba

na Israeli amenajisika.

116:11 Yoe 3:12-13; Yer 51:33“Pia kwa ajili yako, Yuda,

mavuno yameamriwa.

“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,