Hosea 5 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hosea 5:1-15

Hukumu Dhidi Ya Israeli

15:1 Hos 6:9; 9:8; Ay 10:12; Yer 5:26“Sikieni hili, enyi makuhani!

Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli!

Sikieni, ee nyumba ya mfalme!

Hukumu hii ni dhidi yenu:

Mmekuwa mtego huko Mispa,

wavu uliotandwa juu ya Tabori.

25:2 Hos 4:2; 9:15Waasi wamezidisha sana mauaji.

Mimi nitawatiisha wote.

35:3 Eze 23:7; Za 90:8; Hos 1:2; 6:10; Amo 5:12Ninajua yote kuhusu Efraimu,

Israeli hukufichika kwangu.

Efraimu, sasa umegeukia ukahaba,

Israeli amenajisika.

45:4 Hos 4:6, 11; 7:10; Yer 4:22“Matendo yao hayawaachii

kurudi kwa Mungu wao.

Roho ya ukahaba imo ndani ya mioyo yao,

hawamkubali Bwana.

55:5 Isa 3:9; Yer 2:19; Hos 7:10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao;

Waisraeli, hata Efraimu,

wanajikwaa katika dhambi zao;

pia Yuda atajikwaa pamoja nao.

65:6 Mik 6:6-7; Mit 1:28; Mal 1:10; Eze 8:6; Isa 1:26Wakati wanapokwenda na makundi yao

ya kondoo na ngʼombe

kumtafuta Bwana,

hawatampata;

yeye amejiondoa kutoka kwao.

75:7 Isa 1:14; 24:16; Hos 2:4, 11-12; 6:7; Eze 12:28Wao si waaminifu kwa Bwana;

wamezaa watoto haramu.

Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi

zitawaangamiza wao

pamoja na mashamba yao.

85:8 Amu 19:12; Hos 4:15; 10:9; Isa 10:29; Yos 7:2; Hes 10:2; Yer 4:21“Pigeni tarumbeta huko Gibea,

baragumu huko Rama.

Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni,5:8 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

ongoza, ee Benyamini.

95:9 Isa 37:3; Hos 9:11-17; Isa 46:10; 7:16; Zek 1:6Efraimu ataachwa ukiwa

katika siku ya kuadhibiwa.

Miongoni mwa makabila ya Israeli

ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia.

105:10 Kum 19:14; Eze 7:8Viongozi wa Yuda ni kama wale

wanaosogeza mawe ya mpaka.

Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao

kama mafuriko ya maji.

115:11 Hos 9:16; Mik 6:16Efraimu ameonewa,

amekanyagwa katika hukumu

kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.

125:12 Ay 13:28; Isa 51:8; Ay 18:16Mimi ni kama nondo kwa Efraimu,

na kama uozo kwa watu wa Yuda.

135:13 Hes 12:1; Eze 23:5; Mao 5:6; Hos 2:7; Yer 30:12; Isa 7:16; 3:7“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,

naye Yuda vidonda vyake,

ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,

na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.

Lakini hawezi kukuponya,

wala hawezi kukuponya vidonda vyako.

145:14 Ay 10:16; Yer 4:7; Kum 32:39; Mik 5:8; Amo 3:4Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,

kama simba mkubwa kwa Yuda.

Nitawararua vipande vipande na kuondoka;

nitawachukua mbali,

na hakuna wa kuwaokoa.

155:15 Hes 21:7; Za 24:6; 50:15; Yer 2:27; Eze 20:43; Isa 18:4; 64:9Kisha nitarudi mahali pangu

mpaka watakapokubali kosa lao.

Nao watautafuta uso wangu;

katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”