Hosea 2 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hosea 2:1-23

12:1 1Pet 2:10; Hos 2:5“Waambie ndugu zako, ‘Watu wangu,’ na pia waambie dada zako, ‘Wapendwa wangu.’

Israeli Aadhibiwa Na Kurudishwa

22:2 Isa 1:21; 50:1; Eze 16:25; 23:45; Hos 4:5“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni,

kwa maana yeye si mke wangu,

nami si mume wake.

Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake

na uzinzi kati ya matiti yake.

32:3 Eze 16:4, 37; 19:13; Isa 32:13-14Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi

na kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.

Nitamfanya kama jangwa,

nitamgeuza awe nchi ya kiu,

nami nitamuua kwa kiu.

42:4 Eze 8:18; Hos 1:6; 5:7Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake,

kwa sababu ni watoto wa uzinzi.

52:5 Yer 3:6; 44:17-18; Hos 1:2Mama yao amekosa uaminifu

na amewachukua mimba katika aibu.

Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,

ambao hunipa chakula changu

na maji yangu,

sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu

na kinywaji changu.’

62:6 Ay 3:23; 19:8; Mao 3:9Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake

kwa vichaka vya miiba,

nitamjengea ukuta ili kwamba

asiweze kutoka.

72:7 Hos 5:13; Yer 3:1; Eze 16:8; Isa 54:5Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;

atawatafuta lakini hatawapata.

Kisha atasema,

‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza,

kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi

kuliko sasa.’

82:8 Eze 16:15-19; Hes 18:12; Kum 8:18; Hos 8:4Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiye

niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta,

niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumia

kwa kumtumikia Baali.

92:9 Hos 8:7; 9:2“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa

na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari.

Nitamnyangʼanya sufu yangu na kitani yangu

iliyokusudiwa kufunika uchi wake.

102:10 Eze 16:37; 23:10; Yer 13:26Basi sasa nitaufunua ufisadi wake

mbele ya wapenzi wake;

hakuna yeyote atakayemtoa

mikononi mwangu.

112:11 Isa 1:14; 24:8; Amo 5:21; 8:10; Yer 7:34; 16:9; Hos 9:5Nitakomesha furaha na macheko yake yote:

sikukuu zake za mwaka,

sikukuu za Miandamo ya Mwezi,

siku zake za Sabato,

sikukuu zake zote zilizoamriwa.

122:12 Isa 5:6; 7:23; Yer 8:13; Hos 5:7; 13:8Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake,

ambayo alisema yalikuwa malipo yake

kutoka kwa wapenzi wake;

nitaifanya kuwa kichaka,

nao wanyama pori wataila.

132:13 Yer 7:9; Hos 4:13; 8:14; 11:2; 13:6; Eze 16:17; 23:40; Isa 65:7Nitamwadhibu kwa ajili ya siku

alizowafukizia uvumba Mabaali;

alipojipamba kwa pete

na kwa vito vya thamani,

na kuwaendea wapenzi wake,

lakini mimi alinisahau,”

asema Bwana.

142:14 Eze 19:14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi;

nitamwongoza hadi jangwani

na kuzungumza naye kwa upole.

152:15 Yos 7:24-26; Kut 15:1-18; Eze 16:22; 28:26; Hos 12:9; 1Kor 13:13Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,

nami nitalifanya Bonde la Akori2:15 Akori maana yake ni Taabu.

mlango wa matumaini.

Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,

kama siku zile alizotoka Misri.

162:16 Isa 54:5“Katika siku ile,” asema Bwana,

“utaniita mimi ‘Mume wangu’;

hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’

172:17 Kut 23:13; Za 16:4; Yer 23:7; Zek 13:2Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake,

wala hataomba tena kwa majina yao.

182:18 Ay 5:22-23; Za 49:6; Zek 9:10; Eze 34:25; Yer 23:6Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao

na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,

na viumbe vile vitambaavyo ardhini.

Upinde, upanga na vita,

nitaondolea mbali katika nchi,

ili kwamba wote waweze kukaa salama.

192:19 Isa 1:27; 62:4; 54:8; 2Kor 11:2Nitakuposa uwe wangu milele;

nitakuposa kwa uadilifu na haki,

kwa upendo na huruma.

202:20 Yer 31:34; Hos 4:1; 6:6; 13:4; Eze 16:8Nitakuposa kwa uaminifu,

nawe utamkubali Bwana.

212:21 Zek 8:12; Mal 3:10-11; Isa 55:10“Katika siku ile nitajibu,”

asema Bwana,

“nitajibu kwa anga,

nazo anga zitajibu kwa nchi;

222:22 Yer 31:12; Yoe 2:19; Hos 14:7; Eze 36:29-30nayo nchi itajibu kwa nafaka,

divai mpya na mafuta,

navyo vitajibu kwa Yezreeli.

232:23 Yer 29:12; 31:27; Isa 19:25; Hos 1:10; Rum 9:25; Zek 13:9; 1Pet 2:10Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe;

nami nitaonyesha pendo langu kwake

yule ambaye nilimwita, ‘Si mpenzi wangu.2:23 Kiebrania ni Lo-Ruhama.

Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio watu wangu,’2:23 Kiebrania ni Lo-Ami.

‘Ninyi ni watu wangu’;

nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu.’ ”