Hosea 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 14:1-9

Toba Iletayo Baraka

114:1 Hos 5:5; 9:7; 12:6; Yer 3:12; Isa 19:22Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mungu wako.

Dhambi zako zimekuwa

ndilo anguko lako!

214:2 Rum 8:26; Za 51:16-17; Mik 7:18-19; Ebr 13:15; Kut 34:9Chukueni maneno pamoja nanyi,

mkamrudie Bwana.

Mwambieni:

“Samehe dhambi zetu zote

na utupokee kwa neema,

ili tuweze kutoa matunda yetu

kama sadaka za mafahali.

314:3 Mik 5:10; Isa 31:1; Hos 5:13; 8:6; Yer 49:11; Za 10:14; 33:17Ashuru hawezi kutuokoa,

hatutapanda farasi wa vita.

Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’

kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza,

kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”

414:4 Isa 30:26; 55:1; Hos 6:1; Yer 2:19; 31:20; Sef 3:17; Ay 13:16“Nitaponya ukaidi wao

na kuwapenda kwa hiari yangu,

kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao.

514:5 Wim 2:1; Isa 18:4; 35:2; Ay 29:19; Mwa 27:28Nitakuwa kama umande kwa Israeli;

atachanua kama yungiyungi.

Kama mwerezi wa Lebanoni

atashusha mizizi yake chini;

614:6 Za 52:8; 92:12; Yer 11:16; Wim 4:11matawi yake yatatanda.

Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,

harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.

714:7 Za 91:1-4; Hos 2:22; Eze 17:23; Mwa 40:10Watu wataishi tena kwenye kivuli chake.

Atastawi kama nafaka.

Atachanua kama mzabibu,

nao umaarufu wake utakuwa

kama divai itokayo Lebanoni.

814:8 Yer 31:18; Yak 1:17; Isa 37:24Ee Efraimu, nina shughuli gani tena na sanamu?

Nitamjibu na kumtunza.

Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi;

kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.”

914:9 Za 107:43; Mit 10:29; Dan 12:10; Sef 3:5; Mdo 13:10; Isa 1:28; 26:7Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya.

Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa.

Njia za Bwana ni adili;

wenye haki huenda katika njia hizo,

lakini waasi watajikwaa ndani yake.