Hosea 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 13:1-16

Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli

113:1 Mit 18:12; Amu 8:1; 12:1; Hos 11:2Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka,

alikuwa ametukuzwa katika Israeli.

Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali

naye akafa.

213:2 Isa 46:6; Yer 10:4; 44:8; Isa 44:17-20; Hos 8:4; 1Fal 19:18Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi;

wanajitengenezea sanamu

kutokana na fedha yao,

vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari,

vyote kazi ya fundi stadi.

Inasemekana kuhusu hawa watu,

“Hutoa dhabihu za binadamu

na kubusu sanamu za ndama.”

313:3 Hos 6:4; Ay 13:25; Dan 2:35; Za 68:213:3 Isa 17:13Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao,

kama makapi yapeperushwayo

kutoka sakafu ya kupuria nafaka,

kama moshi utorokao kupitia dirishani.

413:4 Yer 2:6; Isa 43:10; 45:21-22; Hos 2:20; 12:9; Kut 20:3; Za 18:46“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu,

niliyewaleta ninyi toka Misri.

Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,

hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

513:5 Kum 1:19; 2:7; 32:10; 8:15; 32:10Niliwatunza huko jangwani,

katika nchi yenye joto liunguzalo.

613:6 Mit 30:7-9; Yer 7:5; Eze 28:5; Kum 32:18; Isa 17:10; Hos 2:13; 4:7Nilipowalisha, walishiba,

waliposhiba, wakajivuna,

kisha wakanisahau mimi.

713:7 Ay 10:16; Yer 4:7; Mao 3:10Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba,

kama chui nitawavizia kando ya njia.

813:8 2Sam 17:8; Za 17:12; 50:22; Mao 3:10; Hos 2:12Kama dubu aliyenyangʼanywa watoto wake,

nitawashambulia na kurarua vifua vyenu.

Kama simba nitawala;

mnyama pori atawararua vipande vipande.

913:9 Yer 2:17-19; Kum 33:29“Ee Israeli, umeangamizwa,

kwa sababu wewe u kinyume nami,

kinyume na msaidizi wako.

1013:10 2Fal 17:4; 1Sam 8:6; Hos 7:7; 8:4Yuko wapi mfalme wako,

ili apate kukuokoa?

Wako wapi watawala wako katika miji yako yote

ambao ulisema kuwahusu,

‘Nipe mfalme na wakuu’?

1113:11 Yos 24:20; 1Sam 13:14; Hes 11:20; 1Fal 14:10; Hos 10:7Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme

na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.

1213:12 Kum 32:34; Ay 14:7Kosa la Efraimu limehifadhiwa,

dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu.

1313:13 Isa 13:8; Mik 4:9-10; Isa 66:9; 2Fal 19:3Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia,

lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima;

wakati utakapowadia hatatoka

katika tumbo la mama yake.

1413:14 1The 4:14-17; Za 16:10; 49:15; Eze 37:12-13; 1Kor 15:54-55; Ufu 21:4“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi,

nitawakomboa kutoka mautini.

Yako wapi, ee mauti, mateso yako?

Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako?

“Sitakuwa na huruma,

1513:15 Ay 1:19; Eze 19:12; Yer 20:5; 51:36; Hos 4:19hata ingawa Efraimu atastawi

miongoni mwa ndugu zake.

Upepo wa mashariki kutoka kwa Bwana utakuja,

ukivuma kutoka jangwani,

chemchemi yake haitatoa maji

na kisima chake kitakauka.

Ghala lake litatekwa

hazina zake zote.

1613:16 2Fal 8:12; 15:16; 17:5; Hos 7:14; 10:2, 14; Isa 13:16; Amo 1:13Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao,

kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao.

Wataanguka kwa upanga;

watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini,

wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”