Hosea 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hosea 11:1-12

Upendo Wa Mungu Kwa Israeli

111:1 Kut 4:22; Mt 2:15; Yer 2:2; Eze 16:22; Hos 12:9; 13:4“Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,

nilimwita mwanangu kutoka Misri.

211:2 Hos 2:13; 4:13; 2Fal 17:15; Isa 65:7; Yer 18:15Lakini kadiri nilivyomwita Israeli,

ndivyo walivyokwenda mbali nami.

Walitoa dhabihu kwa Mabaali

na kufukiza uvumba kwa vinyago.

311:3 Kum 1:31; 32:11; Kut 15:26; Yer 30:17Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,

nikiwashika mikono;

lakini hawakutambua

kuwa ni mimi niliyewaponya.

411:4 Yer 31:2-3, 20; Law 26:13; Kut 16:32; Za 78:25Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,

kwa vifungo vya upendo;

niliondoa nira shingoni mwao

nami nikainama kuwalisha.

511:5 Yer 8:4-6; Hos 7:16; 10:6; Kut 13:17“Je, hawatarudi Misri,

nayo Ashuru haitawatawala

kwa sababu wamekataa kutubu?

611:6 Hos 13:16; Mao 2:9Panga zitametameta katika miji yao,

zitaharibu makomeo ya malango yao

na kukomesha mipango yao.

711:7 Yer 3:6-7; 8:5; Isa 26:10Watu wangu wamedhamiria kuniacha.

Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,

kwa vyovyote hatawainua.

811:8 Mwa 14:8; 19:25; Hos 6:4; Mao 3:32; Yer 7:29; Za 25:6; 1Fal 3:26“Efraimu, ninawezaje kukuacha?

Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?

Nitawezaje kukutendea kama Adma?

Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?

Moyo wangu umegeuka ndani yangu,

huruma zangu zote zimeamshwa.

911:9 Kum 13:17Sitatimiza hasira yangu kali,

wala sitageuka na kumharibu Efraimu.

Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,

wala si mwanadamu,

Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.

Sitakuja kwa ghadhabu.

1011:10 Hos 3:5; 6:1-3; Isa 31:4; 42:13; Za 18:45Watamfuata Bwana;

atanguruma kama simba.

Wakati angurumapo,

watoto wake watakuja wakitetemeka

kutoka magharibi.

1111:11 Isa 11:11; Mwa 8:8; Eze 28:26; 34:25-28Watakuja wakitetemeka

kama ndege wakitoka Misri,

kama hua wakitoka Ashuru.

Nitawakalisha katika nyumba zao,”

asema Bwana.

Dhambi Ya Israeli

1211:12 Hos 4:2; 10:13; Kum 7:9Efraimu amenizunguka kwa uongo,

nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.

Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,

hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.