Hesabu 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 9:1-23

Pasaka Huko Sinai

19:1 Hes 1:1; Kut 40:2Bwana akasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema, 29:2 Kut 12:11; Hes 28:16; Ebr 10:1“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. 39:3 Kut 12:2-11, 43-49; Law 23:5-8; Kum 16:1-8Adhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

49:4 Kut 12:11Hivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka, 59:5 Kut 12:6; Yos 5:10nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Bwana alivyomwamuru Mose.

69:6 Law 5:3; 13:3; 21:11; Kut 18:15; Hes 27:2; Yn 18:28; Hes 6:6-7Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Mose na Aroni siku ile ile, 7wakamwambia Mose, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtolea Bwana sadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamriwa?”

89:8 Kut 18:15; Law 24:12; Hes 15:34; 27:5, 21; Za 85:8; Yn 7:17; Efe 1:9, 18; Ebr 3:5-6Mose akawajibu, “Ngojeni mpaka nitafute kile Bwana anachoagiza kuwahusu ninyi.”

9Ndipo Bwana akamwambia Mose, 109:10 2Nya 30:2“Waambie Waisraeli: ‘Wakati mmoja wenu au wazao wenu wanapokuwa najisi kwa sababu ya maiti au wakiwa safarini, hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka ya Bwana. 119:11 Kut 12:6-8; 2Nya 30:2, 15Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu. 129:12 Kut 12:8, 10, 43, 46; Yn 19:36Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote. 139:13 Mwa 17:14; Kut 12:15; Law 17:4; Ebr 12:25; Hes 5:31; Gal 3:10; Ebr 10:26Lakini kama mtu ni safi kwa taratibu za kiibada naye hayuko safarini, asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake kwa sababu hakutoa sadaka ya Bwana kwa wakati ulioamriwa. Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake.

149:14 Kut 12:19, 43-49“ ‘Mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana, lazima afanye hivyo kwa kufuata desturi na masharti. Lazima masharti yawe sawasawa kwa mgeni na mzawa.’ ”

Wingu La Moto Juu Ya Maskani

(Kutoka 40:34-38)

159:15 Kut 38:21; 26:30; 33:16; 13:21; 40:34Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, iliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya Maskani lilionekana kama moto. 169:16 Kut 40:38; Kum 1:33; Neh 9:12Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto. 179:17 Kut 40:36-38; 1Kor 10:1; Za 78:14; Isa 49:10; Yn 10:4; Hes 9:21; Kut 13:21, 22Wakati wowote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali popote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi. 189:18 Kut 40:37Kwa amri ya Bwana Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.

199:19 Law 8:35; Kut 40:37Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri ya Bwana nao hawakuondoka. 209:20 Za 48:14; Mit 3:5-6Wakati mwingine wingu lilikuwa juu ya Maskani kwa siku chache tu; kwa amri ya Bwana wangelipiga kambi na kisha kwa amri yake wangeliondoka. 219:21 Mt 28:20Wakati mwingine wingu lilikuwepo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka. 22Ikiwa wingu lilikaa juu ya Maskani kwa siku mbili au mwezi au mwaka, Waisraeli wangebaki wamepiga kambi na hawakuondoka; lakini lilipoinuka, wangeondoka.

239:23 Za 73:24; 107:7; Isa 63:14Kwa amri ya Bwana walipiga kambi, na kwa amri ya Bwana waliondoka. Walitii amri ya Bwana, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.