Hesabu 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 6:1-27

Mnadhiri

1Bwana akamwambia Mose, 26:2 Hes 6:5, 6; Mwa 28:20; Mdo 21:23; Amu 13:5; 16:17“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Bwana kama Mnadhiri, 36:3 Law 10:9; 25:5; Lk 1:15; Rut 2:14; Za 69:21; Mit 10:26ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu. 4Kwa muda wote atakaokuwa Mnadhiri, kamwe hatakula chochote kitokanacho na mzabibu, sio mbegu wala maganda.

56:5 Za 52:2; 57:4; 59:7; Isa 7:20; Eze 5:1; 1Sam 1:11; Mao 4:7“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 66:6 Law 21:1-3; Hes 19:11-22; Law 19:28; Yer 16:5-6; Eze 24:18; Mt 8:21Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Bwana hatakaribia maiti. 76:7 Hes 9:6Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake. 8Kwa kipindi chote cha kujitenga kwake yeye ni wakfu kwa Bwana.

96:9 Law 14:9; Hes 6:18“ ‘Kama mtu yeyote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba. 106:10 Law 14:10-11; 5:7; 14:22Kisha siku ya nane ni lazima alete hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa kuhani katika mlango wa Hema la Kukutania. 116:11 Kut 29:36; 30:10; Mwa 8:20Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake. 126:12 Law 12:6; 5:15Ni lazima ajitoe kabisa kwa Bwana kwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

136:13 Mdo 21:26; Law 14:11“ ‘Basi hii ndiyo sheria kwa ajili ya Mnadhiri baada ya kipindi chake cha kujitenga kupita. Ataletwa kwenye ingilio la Hema la Kukutania. 146:14 Kut 12:5; Law 4:3; 14:10; 5:15; 3:1Hapo atatoa sadaka zake kwa Bwana: yaani, mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani, 156:15 Law 2:1; 6:14; Mwa 35:14; Kut 29:2; Hes 15:1-7; Yn 6:50-53; Isa 62:9; 1Kor 10:31; 11:26pamoja na sadaka zake za nafaka na za vinywaji, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, yaani maandazi yaliyotengenezwa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta, na mikate myembamba iliyopakwa mafuta.

16“ ‘Kuhani atavileta vitu hivyo mbele za Bwana na kufanya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa. 176:17 Kut 29:41; Law 23:13Ataleta pia kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, na atatoa dhabihu kondoo dume kama sadaka ya amani kwa Bwana, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka ya kinywaji.

186:18 Mdo 21:24; Lk 17:10; Rum 6:6; Gal 5:24; Efe 4:23; Kol 3:9“ ‘Kisha kwenye ingilio la Hema la Kukutania, Mnadhiri ni lazima anyoe nywele zake ambazo alikuwa ameziweka wakfu. Atazichukua hizo nywele na kuziweka ndani ya moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka ya amani.

196:19 Law 7:12-13“ ‘Baada ya Mnadhiri kunyoa hizo nywele zake za kujitenga kwake, kuhani atampa mikononi mwake bega la kondoo dume lililochemshwa, na pia andazi na mkate mwembamba kutoka kwenye kikapu, vyote vikiwa vimetengenezwa bila kuwekwa chachu. 206:20 Law 7:30; 27:9; 7:34; Mhu 9:7; Isa 35:10; Ufu 14:13Kisha kuhani ataviinua mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua; ni vitakatifu na ni mali ya kuhani, pamoja na kile kidari kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. Baada ya hayo, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

21“ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwa Bwana kufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya chochote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”

Baraka Ya Kikuhani

22Bwana akamwambia Mose, 236:23 Kum 21:5; 1Nya 23:13“Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni:

246:24 Mwa 28:3; Kum 28:3-6; Za 17:9; 28:9; 128:5; 1Sam 2:9“ ‘ “Bwana akubariki

na kukulinda;

256:25 Ay 29:24; Za 4:6; 25:16; 86:16; 31:16; 80:3; 119:29, 135; Mwa 43:29Bwana akuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

266:26 Za 4:6; 44:3; 4:8; 29:11; 37:11, 37; 127:2; Isa 14:7; Yer 33:6; Yn 14:27Bwana akugeuzie uso wake

na kukupa amani.” ’

276:27 Kum 28:10; 2Sam 7:23; Neh 9:10; Yer 25:29; Eze 36:23“Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”