Hesabu 3 – NEN & CCL

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 3:1-51

Walawi

13:1 Kut 6:27; 19:11Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati ambao Bwana alizungumza na Mose katika Mlima Sinai.

23:2 Hes 1:20; 26:30; Kut 6:23; 1Nya 6:3Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari. 33:3 Kut 28:41; 29:30Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani. 43:4 Law 10:1-6, 12; Hes 4:28; 1Nya 24:1; Hes 26:61; Kum 4:24; Isa 66:15; 2The 1:8; Ebr 12:29Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.

5Bwana akamwambia Mose, 63:6 Kum 10:8; 31:9; 1Nya 15:2; Hes 8:6-22; 18:1-7; 2Nya 29:11“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie. 73:7 Hes 1:53; 8:19; Law 8:35Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani. 8Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani. 93:9 Hes 8:19; 18:6Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa. 103:10 Kut 30:7; 29:9; Hes 1:51; 18:7; Mdo 6:3-4; Rum 12:7; 1Sam 6:19; Hes 16:40; 18:7Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

11Bwana akamwambia Mose, 123:12 Neh 13:12; Mal 2:4; Hes 8:14, 16-18; 16:9; Kut 13:2“Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu, 133:13 Kut 13:12; Law 11:44kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.”

14Bwana akamwambia Mose katika Jangwa la Sinai, 153:15 Hes 1:19; 18:16; 26:62“Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.” 16Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.

173:17 Mwa 29:34; 46:11; Hes 1:47; 1Nya 15:4; 23:6; 2Nya 29:12; Yos 21:4-6Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:

Gershoni, Kohathi na Merari.

183:18 Kut 6:16-17Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni:

Libni na Shimei.

193:19 Kut 6:18Koo za Wakohathi zilikuwa ni:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

203:20 Mwa 46:11; Kut 6:19Koo za Wamerari zilikuwa ni:

Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

213:21 Mwa 46:11; Kut 6:17Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni. 22Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500. 233:23 Hes 2:18Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani. 24Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli. 253:25 Kut 25:9; 26:14, 36; 40:2; Hes 7:1; 4:25; 1Nya 9:14-33; Ezr 8:28-30Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania, 263:26 Kut 27:9; 35:18; Hes 4:26mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

273:27 Mwa 46:11; Kut 6:18; 1Nya 26:23; Hes 4:15, 37Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamramu, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi. 283:28 Hes 4:4, 15; Kut 25:8; 30:13; 2Nya 30:19; Za 15:1; 20:2; Eze 44:27Hesabu ya waume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu. 293:29 Hes 1:53Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani. 303:30 Kut 6:22Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli. 313:31 Kut 25:10-22, 23, 31; 26:33; Kum 10:1-8; 2Nya 5:2; Yer 3:16; 1Nya 28:15; Yer 52:19; Hes 1:50; 4:5, 15; 18:3Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake. 323:32 Kut 6:23; Hes 4:19; 18:3; 20:25-28; 2Fal 25:18Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

333:33 Kut 6:19; Mwa 46:11Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari. 34Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200. 353:35 Hes 1:53; 2:25Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani. 363:36 Hes 4:32; Kut 26:15-25; 35:20-29; 36:36; Hes 18:3Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake, 373:37 Kut 27:10-19na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

383:38 Hes 2:3; 18:5; 1:51; 1Nya 9:27; 23:32Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.

393:39 Hes 26:62Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri ya Bwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa 22,000.

40Bwana akamwambia Mose, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao. 413:41 Law 11:44Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi Bwana.”

42Hivyo Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru. 43Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza waume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina, walikuwa 22,273.

44Bwana akamwambia Mose, 453:45 Hes 3:12; 1Sam 1:28“Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana. 463:46 Kut 13:13; Hes 18:15Ili kukomboa wazao wa kwanza 273 wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi, 473:47 Law 27:6, 25; Kut 30:13; Hes 18:16; Eze 45:12kusanya shekeli tano3:47 Shekeli tano ni sawa na gramu 55. kwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.3:47 Gera 20 ni sawa na gramu 11. 48Mpe Aroni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”

493:49 1Tim 2:6; Tit 2:14; Gal 4:4-5; 1Pet 1:18; Ebr 9:12Kwa hiyo Mose akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi. 503:50 1Sam 12:3-4; Mdo 20:33Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli 1,3653:50 Shekeli 1,365 ni sawa na kilo 15.5. kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu. 51Mose akampa Aroni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.

The Word of God in Contemporary Chichewa

Numeri 3:1-51

Alevi

1Iyi ndi mbiri ya banja la Aaroni ndi Mose pa nthawi yomwe Yehova anayankhula ndi Mose pa phiri la Sinai.

2Mayina a ana aamuna a Aaroni anali Nadabu, woyamba kubadwa, Abihu, Eliezara ndi Itamara. 3Amenewa ndi mayina a ana aamuna a Aaroni, ansembe odzozedwa omwe anapatulidwa kuti azitumikira ngati ansembe. 4Koma Nadabu ndi Abihu, anagwa nafa pamaso pa Yehova pamene ankapereka nsembe ndi moto wachilendo pamaso pa Yehova mʼchipululu cha Sinai. Iwowo analibe ana aamuna. Choncho Eliezara ndi Itamara ndiwo amene ankatumikira ngati ansembe nthawi imene Aaroni abambo awo anali moyo.

5Yehova anati kwa Mose, 6“Bweretsa fuko la Levi ndipo ulipereke kwa Aaroni wansembe kuti lizimutumikira. 7Azigwira ntchito yothandiza iyeyo ndi gulu lonse ku tenti ya msonkhano pogwira ntchito ya ku Chihema. 8Azisamalira zipangizo zonse za mu tenti ya msonkhano, ndipo azigwirira ntchito Aisraeli potumikira mu tenti. 9Pereka Alevi kwa Aaroni ndi kwa ana ake aamuna. Amenewa ndiwo Aisraeli amene aperekedwa kwa iye kwathunthu. 10Usankhe Aaroni ndi ana ake aamuna kuti azitumikira pa ntchito ya unsembe. Koma wina aliyense woyandikira malo opatulika aphedwe.”

11Yehova anawuzanso Mose kuti, 12“Pakati pa Aisraeli onse ndatenga Alevi kulowa mʼmalo mwa mwana wamwamuna aliyense woyamba kubadwa kwa amayi a Chiisraeli. Alevi ndi anga, 13pakuti ana onse oyamba kubadwa ndi anga. Nditakantha ana onse oyamba kubadwa mu Igupto, ndinadzipatulira ndekha mwana aliyense woyamba kubadwa mu Israeli, wa munthu ndi nyama. Azikhala anga. Ine ndine Yehova.”

14Yehova anawuza Mose mʼchipululu cha Sinai kuti, 15“Werenga Alevi monga mwa mabanja awo ndi mafuko awo. Werenga mwamuna aliyense kuyambira wa mwezi umodzi kapena kupitirirapo.” 16Choncho Mose anawawerenga potsatira zomwe Yehova anamulamulira.

17Mayina a ana aamuna a Levi ndi awa:

Geresoni, Kohati ndi Merari.

18Mayina a ana a Geresoni potsata mabanja awo ndi awa:

Libini ndi Simei.

19Ana a Kohati potsata mabanja awo ndi awa:

Amramu, Izihari, Hebroni ndi Uzieli.

20Ana a Merari potsata mabanja awo ndi awa:

Mali ndi Musi.

Amenewa ndiwo anali mabanja a Alevi monga mwa makolo awo.

21Kwa Geresoni kunali banja la Alibini, banja la Asimei. Amenewa ndiwo anali mabanja a Ageresoni. 22Chiwerengero cha amuna onse amene anawawerenga a mwezi umodzi kapena kupitirirapo chinali 7,500. 23Mabanja a Ageresoni azimanga misasa yawo kumadzulo, kumbuyo kwa Chihema. 24Mtsogoleri wa mabanja a Ageresoni anali Eliyasafu mwana wa Laeli. 25Ntchito imene Ageresoni anapatsidwa ku tenti ya msonkhano inali yosamalira Chihema ndi tenti, pamodzi ndi zophimbira zake, katani ya pa khomo la ku tenti ya msonkhano, 26ndi makatani wotchinga bwalo, katani ya pa chipata cholowera ku bwalo lozungulira Chihema ndi guwa lansembe, zingwe ndi zonse zokhudzana ndi ntchito yawo.

27Kwa Kohati kunali mabanja a Amramu, Aizihara, Ahebroni ndi Auzieli. Awa ndiye anali mabanja a Akohati. 28Chiwerengero cha amuna onse a mwezi umodzi kapena kupitirirapo chinali 8,600. Akohati ankagwira ntchito yosamalira malo wopatulika. 29Mabanja a ana a Kohati ankamanga misasa yawo kummwera kwa Chihema. 30Mtsogoleri wa magulu a mabanja a Kohati anali Elizafani mwana wa Uzieli. 31Iwo ankagwira ntchito yosamalira Bokosi la Chipangano, tebulo, choyikapo nyale, maguwa, zipangizo za kumalo wopatulika zimene ansembe ankagwiritsa ntchito, katani, ndi zonse zomwe ankagwiritsa ntchito. 32Mtsogoleri wamkulu wa Alevi anali Eliezara mwana wa Aaroni wansembe. Iye anasankhidwa kukhala woyangʼanira omwe ankasamalira malo wopatulika.

33Kwa Merari kunali banja la Mali ndi banja la Musi. Amenewa ndiye anali mabanja a Amerari. 34Chiwerengero cha amuna onse kuyambira a mwezi umodzi kapena kupitirirapo chinali 6,200. 35Mtsogoleri wa magulu a mabanja a Amerari anali Zuriyeli mwana wa Abihaili. Iwo ankamanga misasa yawo kumpoto kwa Chihema. 36Amerari anapatsidwa ntchito yosamalira mitengo ya chihema, nsichi zake, mizati yake, matsinde ake, ndi zida zake zonse, ndi zonse zomwe ankagwiritsa ntchito, 37pamodzi ndi mizati yozungulira bwalo ndi matsinde ake, zikhomo za chihema ndi zingwe zake.

38Mose ndi Aaroni ndi ana ake aamuna ankamanga misasa yawo kummawa kwa chihema, kuyangʼana kotulukira dzuwa, kutsogolo kwa tenti ya msonkhano. Anali ndi ntchito yosamalira malo wopatulika mʼmalo mwa Aisraeli. Aliyense woyandikira malo wopatulika ankayenera kuphedwa.

39Alevi onse amene Mose ndi Aaroni anawawerenga potsatira lamulo la Yehova monga mwa magulu a mabanja awo, amuna onse kuyambira a mwezi umodzi kapena kupitirirapo anali 22,000.

40Yehova anawuza Mose kuti, “Werenga ana onse aamuna oyamba kubadwa mu Israeli, omwe ali ndi mwezi umodzi kapena kupitirirapo ndipo ulembe mndandanda wa mayina awo. 41Unditengere Alevi onse mʼmalo mwa ana oyamba kubadwa onse a Aisraeli, ndiponso ziweto zazimuna za Alevi mʼmalo mwa ziweto zonse zazimuna zoyamba kubadwa za Aisraeli. Ine ndine Yehova.”

42Choncho Mose anawerenga ana aamuna onse oyamba kubadwa a Aisraeli monga momwe Yehova anamulamulira. 43Chiwerengero chonse cha ana aamuna oyamba kubadwa kuyambira a mwezi umodzi kapena kupitirirapo chinali 22, 273.

44Ndipo Yehova anawuzanso Mose kuti, 45“Tenga Alevi mʼmalo mwa ana aamuna oyamba kubadwa onse a Aisraeli, ndiponso zoweta zonse za Alevi mʼmalo mwa zoweta za Aisraeli. Alevi ndi anga. Ine ndine Yehova. 46Pofuna kuwombola ana aamuna 273 oyamba kubadwa a Aisraeli amene anaposa chiwerengero cha aamuna a fuko la Levi, 47utenge masekeli asanu pa munthu aliyense. Masekeliwo akhale ofanana ndi masekeli a ku malo wopatulika, kumene sekeli imodzi imakwanira magera makumi awiri. 48Ndalama zimenezi uzipereke kwa Aaroni ndi ana ake aamuna kuti ukhale mtengo woombolera Aisraeli woonjezerawo.”

49Choncho Mose anatenga ndalama zowombolera zija kuchokera kwa Aisraeli amene chiwerengero chawo chinaposa chiwerengero cha omwe anawomboledwa ndi Alevi. 50Anatenga masekeli a siliva okwana 1,365 molingana ndi masekeli a ku malo opatulika, kuchokera kwa ana aamuna oyamba kubadwa a Aisraeli. 51Mose anapereka ndalama zowombolera zija kwa Aaroni ndi ana ake aamuna monga mwa mawu amene Yehova analamulira.