Hesabu 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 24:1-25

124:1 Hes 23:20, 23, 28Basi Balaamu alipoona imempendeza Bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani. 224:2 Hes 11:25; 1Sam 19:20; 2Nya 15:1; Mt 7:21-22; 1Kor 12:8-10Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake, 324:3 Hes 23:7naye akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

424:4 Hes 22:9; Mwa 15:1; 1Sam 19:24; Eze 1:28; Dan 8:18; 10:15; 2Kor 12:2ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi,24:4 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania (pia 24:16).

ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:

524:5 Yer 4:20; 30:18; Mal 2:12“Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,

maskani yako, ee Israeli!

624:6 Mwa 2:10; Za 1:3; 45:8; 104:16; Wim 4:14; Ay 29:19; Eze 31:5“Kama mabonde, yanaenea,

kama bustani kando ya mto,

kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana,

kama mierezi kando ya maji.

724:7 Kut 17:8-16; Kum 28:1; 2Sam 5:12; 1Nya 14:2; Za 89:27; 145:11-13Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;

mbegu yake itakuwa na maji tele.

“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;

ufalme wake utatukuka.

824:8 Kut 15:6; Yer 50:17; 2Sam 18:14; Za 45:5“Mungu alimleta kutoka Misri;

yeye ana nguvu kama nyati.

Anayararua mataifa yaliyo adui zake,

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

huwachoma kwa mishale yake.

924:9 Kut 23:23; Hes 23:24; Mwa 12:2, 3; 27:29; Za 122:6Hujikunyata na kuvizia kama simba,

kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?

“Abarikiwe kila akubarikiye,

na alaaniwe kila akulaaniye!”

1024:10 Kut 4:14; Ay 27:23; 34:37; Mao 2:15; Eze 21:14; 22:13; 25:6; Hes 22:6; 23:7-11, 18-24; Kum 23:5Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu. 1124:11 Hes 22:17Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.”

1224:12 Hes 22:18Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi, 1324:13 Hes 22:18, 20‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosema’? 1424:14 Mwa 49:1; Hes 31:8; Mik 6:5Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”

Ujumbe Wa Nne Wa Balaamu

15Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

1624:16 Hes 22:9; Mwa 14:18; Isa 14:14ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,

huona maono kutoka Mwenyezi,

ambaye huanguka kifudifudi

na ambaye macho yake yamefunguka:

1724:17 Ufu 1:7; Mt 2:2; Mwa 49:10; 19:37; Hes 21:29; Kum 23:6; Isa 15:1–16:14; Yer 48:45“Namwona yeye, lakini si sasa;

namtazama yeye, lakini si karibu.

Nyota itatoka kwa Yakobo,

fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.

Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyuso

na mafuvu yote ya wana wa Shethi.

1824:18 2Sam 8:12; 1Nya 18:11; Za 60:8; Isa 11:14; Amo 9:12; Mwa 9:25; 14:6; Kum 1:44; Yos 12:7; 15:10; Amu 5:4; Oba 1:2Edomu itamilikiwa,

Seiri, adui wake, itamilikiwa,

lakini Israeli atakuwa na nguvu.

1924:19 Mwa 49:10; Mik 5:2Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo

na kuangamiza walionusurika katika mji.”

Ujumbe Wa Mwisho Wa Balaamu

2024:20 Mwa 14:7; Kut 17:14; Kum 25:19; 1Sam 15:20; 30:17-20; 2Sam 8:12; 1Nya 18:11Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:

“Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa,

lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”

2124:21 Mwa 15:19; Za 37:27; Mit 1:33; Isa 32:18; Eze 34:27Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake:

“Makao yenu ni salama,

kiota chenu kiko kwenye mwamba.

2224:22 Mwa 10:22Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwa

Ashuru atakapowachukua mateka.”

23Ndipo akatoa ujumbe wake:

“Lo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili?

2424:24 Mwa 10:4, 21; Hes 22:5; Isa 23:1; Dan 11:30; Law 26:28; Kum 28:36; Mt 23:37Meli zitakuja kutoka pwani za Kitimu,

zitaitiisha Ashuru na Eberi,

lakini nao pia wataangamizwa.”

25Kisha Balaamu akainuka na kurudi nyumbani kwake, naye Balaki akashika njia yake.