Hesabu 21 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 21:1-35

Nchi Ya Aradi Yaangamizwa

121:1 Hes 33:40; Yos 12:14; Mwa 12:9; Hes 13:17; Kum 1:7; Amu 1:9Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyeishi huko Negebu aliposikia kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kwa njia ya Atharimu, aliwashambulia Waisraeli na kuwateka baadhi yao. 221:2 Law 7:16; Kut 22:20; Kum 2:34; Yos 2:10; 8:26; Yer 25:9; 50:21Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.” 321:3 Mwa 10:18; Hes 14:45Bwana akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.21:3 Horma maana yake Maangamizi.

Nyoka Wa Shaba

421:4 Hes 20:22; 14:25; Kum 2:1; 11:4; Hes 20:21; Kum 2:8; Amu 11:18Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu,21:4 Yaani Bahari Nyekundu au Bahari ya Mafunjo (ona 14:25). kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani, 521:5 Za 78:19; Kut 14:11; Hes 11:20; 14:2, 3; 20:3; 11:5wakamnungʼunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”

621:6 Kum 8:15; 32:33; Ay 20:14; Za 58:4; 140:3; Yer 8:17; 1Kor 10:9Ndipo Bwana akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa. 721:7 Za 78:34; Hos 5:15; Hes 14:40; Kut 8:8; 1Sam 7:8; Yer 27:18; 37:3; Mdo 8:24; Hes 11:2Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya Bwana na dhidi yako. Mwombe Bwana ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu.

821:8 Yn 3:14Bwana akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.” 921:9 2Fal 18:4; Yn 3:14-15Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.

Safari Kwenda Moabu

1021:10 Hes 33:43Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi. 1121:11 Mwa 36:35; Hes 33:44; Kum 34:8; Yer 40:11Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua. 1221:12 Kum 2:13, 14Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi. 1321:13 Hes 22:36; Kum 2:24; Yos 12:1; Amu 11:13, 18; 2Fal 10:33; Isa 16:2; Yer 48:20; Mwa 10:16Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori. 1421:14 1Sam 17:47; 18:17; 25:28Ndiyo sababu Kitabu cha Vita vya Bwana kinasema:

“…Mji wa Wahebu nchini Seifa na mabonde

ya Arnoni, 1521:15 Kum 2:9, 18; Isa 15:1na miteremko ya mabonde

inayofika hadi mji wa Ari

na huelekea mpakani mwa Moabu.”

1621:16 Hes 25:1; 33:49; Amu 9:21; Isa 15:8Kutoka hapo waliendelea mbele hadi kisima cha Beeri; kwenye kisima ambacho Bwana alimwambia Mose, “Wakusanye watu pamoja, nami nitawapa maji.”

1721:17 Kut 15:1Kisha Israeli akaimba wimbo huu:

“Bubujika, ee kisima!

Imba kuhusu maji,

18kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu,

ambacho watu mashuhuri walikifukua,

watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.”

Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana, 19kutoka Matana wakafika Nahalieli, kutoka Nahalieli wakafika Bamothi, 2021:20 Hes 23:14; Kum 3:17; 34:1; Yos 12:3; 13:20na kutoka Bamothi wakafika kwenye bonde lililoko Moabu, mahali ambapo kilele cha Pisga kinatazamana na nyika.

Kushindwa Kwa Sihoni Na Ogu

(Kumbukumbu 2:26–3:11)

2121:21 Mwa 32:3; Hes 32:33; Kum 1:4; Yos 2:10; 12:2; 13:10; Amu 11:19-21; 1Fal 4:19; Neh 9:22; Za 135:11; 136:19; Yer 48:4; 48:45; Kut 23:23Israeli akawatuma wajumbe kumwambia Sihoni mfalme wa Waamori:

2221:22 Hes 20:17“Uturuhusu tupite katika nchi yako. Hatutageuka kando kwenda katika mashamba au mashamba ya mizabibu, ama kunywa maji kutoka kisima chochote. Tutasafiri kwenye njia kuu ya mfalme hata tutakapokuwa tumekwisha kupita katika nchi yako.”

2321:23 Hes 20:21; Kum 2:32; Yos 13:18; 21:36; Amu 11:20; Isa 15:4; Yer 48:21, 34; Hes 20:18Lakini Sihoni hakumruhusu Israeli apite katika nchi yake. Alilikutanisha jeshi lake lote, wakaondoka kwenda jangwani ili kupigana na Israeli. Alipofika huko Yahazi, akapigana na Israeli. 2421:24 Kum 2; 33; 3:3; 29:7; Za 135:10-11; Amo 2:9; Kum 3:4; Mwa 32:22; Hes 32:33; Amu 11:13, 22; Mwa 19:38; Kum 2:37; Yos 13:10Hata hivyo, Israeli alimshinda kwa upanga na kuiteka ardhi yake kutoka Arnoni mpaka Yaboki, lakini ni hadi kufikia nchi ya Waamoni tu, kwa sababu mipaka yake ilikuwa imezungushwa ukuta. 2521:25 Hes 13:29; Amu 10:11; 11:26; Amo 2:10; Hes 32:3; Kum 1:4; 29:7; Yos 9:10; 12:2; Isa 15:4; 16:8; Yer 48:2Israeli akaiteka miji yote ya Waamori na kuikalia, pamoja na Heshboni na makazi yote yanayoizunguka. 2621:26 Kum 29:7; Za 135:11; Hes 13:29Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.

27Ndiyo sababu watunga mashairi husema:

“Njoo Heshboni na ujengwe tena;

mji wa Sihoni na ufanywe upya.

2821:28 Yer 48:45; Hes 11:1; 22:41; Kum 12:2; Yos 13:17; Isa 15:2; Yer 1:5“Moto uliwaka kutoka Heshboni,

mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni.

Uliteketeza Ari ya Moabu,

raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.

2921:29 Hes 24:17; 2Sam 8:2; 1Nya 18:2; Za 60:8; Isa 25:10; Yer 48:46; Amu 10:6; 11:24; Rum 1:15; 1Fal 11:7; 2Fal 23:13; Yer 48:7; Isa 15:5; 16:2Ole wako, ee Moabu!

Umeharibiwa, enyi watu wa Kemoshi!

Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,

na binti zake kama mateka

kwa Mfalme Sihoni wa Waamori.

3021:30 Hes 32:3; Yos 13:19; Neh 11:25; Isa 15:2; Yer 48:18; Yos 13:16; 1Nya 19:7“Lakini tumewashinda;

Heshboni umeharibiwa hadi Diboni.

Tumebomoa hadi kufikia Nofa,

ulioenea hadi Medeba.”

3121:31 Hes 13:29Kwa hiyo Israeli akaishi katika nchi ya Waamori.

3221:32 Yos 2:1; 6:22; 7:2; Amu 18:2; 2Sam 10:3; 1Nya 19:3; Hes 32:1; Yos 13:25; 2Sam 24:5; 1Nya 6:8; Isa 16:8; Yer 48; 32Baada ya Mose kutuma wapelelezi kwenda mji wa Yazeri, Waisraeli waliteka viunga vya mji huo na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanaishi huko. 3321:33 Hes 32:33; Kum 3:3; 31:11; Yos 2:10; 12:4; 13:30; 1Fal 4:19; Neh 9:22; Za 135:11; 136:20; Kum 3:4; 32:14; Yos 9:10; 1Fal 4:13; Kum 1:4; 3:1; Yos 12:4; 13:12; 19:37Kisha wakageuka na kwenda katika njia inayoelekea Bashani, naye Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote wakatoka kupigana nao huko Edrei.

3421:34 Kum 3:2Bwana akamwambia Mose, “Usimwogope Ogu, kwa sababu nimeshamkabidhi mikononi mwako, pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Mtendee kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

3521:35 Hes 21:35; Yos 9:10; 22:1; Hes 22:11; 13:29; Yos 2:7; Hes 31:12; 33:48; Kum 32:49; Yos 2:1Kwa hiyo wakamuua, pamoja na wanawe na jeshi lake lote, bila ya kumwacha hata mtu mmoja hai. Nao wakaimiliki nchi yake.