Hesabu 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 20:1-29

Maji Kutoka Kwenye Mwamba

(Kutoka 17:1-7)

120:1 Hes 13:21; 13:26; 33:36; Kum 1:46; Amu 11:17; Za 29:8; Kut 15:20Katika mwezi wa kwanza jumuiya yote ya Kiisraeli ilifika kwenye Jangwa la Sini, nao wakakaa Kadeshi. Miriamu akafa huko na kuzikwa.

220:2 Kut 15:22; 17:1; Hes 16:19Mahali hapo hapakuwa na maji kwa ajili ya jumuiya hiyo, nao wakakusanyika ili kumpinga Mose na Aroni. 320:3 Mwa 13:7; Kut 17:2; 21:18; 5:21; Hes 14:2; 16:31-35Watu wakagombana na Mose, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu zetu walipoanguka na kufa mbele za Bwana! 420:4 Hes 14:2; Kut 14:11; Hes 14:3; 16:13Kwa nini mmeileta jumuiya ya Bwana kwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu? 520:5 Hes 13:23; 16:14; Kut 17:1Kwa nini mmetupandisha kutoka Misri mpaka mahali hapa pa kutisha? Hapa hakuna nafaka wala tini, zabibu au makomamanga. Wala hapa hakuna maji ya kunywa!”

620:6 Kut 40:2; Hes 14:5; 16:19Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu wa Bwana ukawatokea. 7Bwana akamwambia Mose, 820:8 Kut 4:2; 10:12-13; 17:6; Isa 41:18; 43:20; Yer 31:9“Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Aroni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”

920:9 Hes 17:2; 17:10Kwa hiyo Mose akaichukua hiyo fimbo kutoka pale ilipokuwa mbele za Bwana kama alivyomwagiza. 1020:10 Za 106:32-33Mose na Aroni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?” 1120:11 Kut 17:6; Isa 33:21Ndipo Mose akainua mkono wake na kuupiga mwamba mara mbili kwa fimbo yake. Maji yakabubujika, nayo jumuiya na mifugo yao wakanywa.

1220:12 Hes 27:14; Kum 32:51; Isa 5:16; 8:13; Kum 3:27Lakini Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Kwa sababu hamkuniamini mimi kiasi cha kuniheshimu kama mtakatifu machoni pa Waisraeli, hamtaiingiza jumuiya hii katika nchi ninayowapa.”

1320:13 Kut 17:7; Law 10:3Haya yalikuwa maji ya Meriba,20:13 Meriba maana yake Kugombana. mahali pale ambapo Waisraeli waligombana na Bwana, naye akajionyesha mwenyewe huko kuwa mtakatifu katikati yao.

Edomu Wakatalia Israeli Kupita

1420:14 Hes 20:1, 16; Mwa 36:16; 25:30; 24:3; Kum 4:39; Yos 2:11; 9:9; Kut 18:8Mose akawatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwenda kwa mfalme wa Edomu, akisema:

“Hili ndilo ndugu yako Israeli asemalo: Wewe unafahamu juu ya taabu zote ambazo zimetupata. 1520:15 Mwa 46:6; 15:13; Kut 1:14Baba zetu walishuka Misri, nasi tumeishi huko miaka mingi. Wamisri walitutesa sisi na baba zetu, 1620:16 Mwa 16:11; 21:17; Kut 2:23; 14:19; 12:42; Kum 26:8; Hes 33:37lakini tulipomlilia Bwana, alisikia kilio chetu na akamtuma malaika akatutoa Misri.

“Sasa tupo hapa Kadeshi, mji ulio mpakani mwa nchi yako. 1720:17 Hes 21:22; Kum 2:27; Amu 11:17Tafadhali turuhusu tupite katika nchi yako. Hatutapita katika shamba lolote, wala shamba la mizabibu, au kunywa maji kutoka kwenye kisima chochote. Tutasafiri kufuata njia kuu ya mfalme, na hatutageuka kulia wala kushoto mpaka tuwe tumeshapita nchi yako.”

1820:18 Hes 21:23Lakini mfalme wa Edomu akajibu:

“Hamtapita hapa; kama mkijaribu kupita, tutatoka na kuwashambulia kwa upanga.”

1920:19 Kut 2:23; Kum 2:6, 28Waisraeli wakajibu:

“Sisi tutafuata njia kuu; tena ikiwa sisi au mifugo yetu tutakunywa tone la maji yenu, tutalilipia. Sisi tunataka tu kupita kwa miguu, wala si kitu kingine chochote.”

20Watu wa Edomu wakajibu tena:

“Hamwezi kupita hapa.”

Ndipo watu wa Edomu wakatoka dhidi ya Waisraeli, jeshi kubwa lenye nguvu. 2120:21 Hes 21:23; 21:4; Kum 2:8; Amu 11:18Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha.

Kifo Cha Aroni

2220:22 Kum 1:46; Hes 33:37; 34:7; Kum 32:50Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka kutoka Kadeshi, wakafika kwenye Mlima Hori. 23Kwenye Mlima Hori, karibu na mpaka wa Edomu, Bwana akamwambia Mose na Aroni, 2420:24 Mwa 25; 8; Kut 17:7“Aroni atakusanywa pamoja na watu wake. Hataingia katika nchi ninayowapa Waisraeli, kwa sababu ninyi wawili mliasi dhidi ya agizo langu kwenye maji ya Meriba. 2520:25 Hes 33:38Watwae Aroni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima wa Hori. 2620:26 Kut 28:1-4; 40:13; Law 16:4; Hes 27:13; 31:2Mvue Aroni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Aroni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.”

2720:27 Hes 33:38Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza: Wakapanda Mlima Hori mbele ya macho ya jumuiya yote ya Kiisraeli. 2820:28 Kut 29:29; Hes 33:38; Kum 10:6; 32:50; Mwa 27:41; Law 10:6; Kum 34:8Mose akamvua Aroni mavazi yake na kumvika mwanawe Eleazari mavazi hayo. Naye Aroni akafia pale juu ya mlima. Kisha Mose na Eleazari wakateremka kutoka mlimani. 29Jumuiya yote ilipofahamu kwamba Aroni amekufa, jamaa yote ya Kiisraeli wakamwomboleza kwa siku thelathini.