Hesabu 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 13:1-33

Kupeleleza Kanaani

(Kumbukumbu 1:19-33)

1Bwana akamwambia Mose, 213:2 Hes 13:16; Kum 1:22; Law 14:34; 24:11; Yos 1:3“Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”

313:3 Hes 14:6; 24; 34:19; Kum 1:36; Amu 1:12-15Hivyo kwa agizo la Bwana Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. 4Haya ndiyo majina yao:

kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;

5kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;

613:6 Hes 14:6; 24; 34:19; Kum 1:36; Amu 1:12-15; Yos 14:6kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;

7kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;

813:8 Hes 11:28kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;

9kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;

10kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,

11kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;

12kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;

13kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;

14kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;

15kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.

1613:16 Kum 32:44; Kut 17:9Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)

1713:17 Yos 14:7; Mwa 12:9; Kum 1:7; Yos 9:1; Mwa 14:10; Kum 1:19; Amu 1:9-10Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. 18Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi. 19Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? 2013:20 Kum 1:25; Law 25:5; Kum 8:7, 8; Neh 9:25-35; Eze 20:6; 34:14; Kum 31:6; Yos 1:6, 9; Ebr 13:6Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)

2113:21 Hes 20:1; 27:14; 33:36; 34:8; Kum 32:51; Yos 15:1; 19:28; 13:5; Amu 1:31; 18:28; 2Sam 10:6; 1Nya 6:75; 13:5; 1Fal 8:65; 2Fal 14:25; 2Nya 7:8; Yer 52:7; Eze 47:16-20; Amo 6:14Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi. 2213:22 Hes 13:28; Mwa 13:18; 23:19; Yos 15:14; Amu 1:10; Kum 2:10; 9:2; Yos 11:21; 15:13; Za 78:12; Isa 19:11-13; 30:4; Eze 30:14Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.) 2313:23 Mwa 14:13; Kut 28:33; Mwa 3:7; Hes 20:5; Kum 8:8; 2Fal 18:31; Neh 13:15Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini. 24Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko. 2513:25 Mwa 7:4; Hes 14:34Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

Taarifa Juu Ya Upelelezi

2613:26 Mwa 14:6-7; Hes 32:8; Kum 1:25Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi. 2713:27 Kut 3:8; Kum 1:25; Yer 2:7Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. 2813:28 Kum 1:28; Yos 14:12Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki. 2913:29 Mwa 10:16, 18; 13:10; 14:7; 10:15; Kum 7:1; 20:17; 1Fal 9:20; 10:29; 2Fal 6:7; Kut 3:8; Hes 22:1; 32:5; Amu 3:28; Za 42:6Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”

3013:30 Yos 14:7; Za 60:12; 119:10; Isa 11:10; Rum 8:31; Flp 4:13; Ebr 11:33, 34Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.”

3113:31 Kum 9:1; Yos 14:8Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.” 3213:32 Hes 14:36-37; Eze 36:13-14; Kum 1:28; Amo 2:9Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 3313:33 Mwa 6:4; Kum 1:28; Yos 11:22; 14:12; Mhu 12:5; Isa 40:22Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”