Hesabu 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 11:1-35

Moto Kutoka Kwa Bwana

111:1 Law 10:2; Kut 4:14; 14:11; 16:7; Mao 3:39; Hes 12:2; 21:28; Kum 1:34; Za 78:63; Isa 26:11; Kut 15:23, 24; 16:2, 3, 7; Kum 9:22; 2Fal 1:12Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 211:2 Kum 9:19; 1Sam 2:25; 12:23; Za 106:23; Mwa 20:7; Hes 21:7; Yn 2:1Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika. 311:3 Kum 9:20-22; Hes 16:35; Ay 1:16; Isa 10:17Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,11:3 Tabera maana yake Kunaungua. kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao.

Kware Kutoka Kwa Bwana

411:4 Kut 12:38; 16:3; Za 78:18; 1Kor 10:6Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! 511:5 Kut 16:3; Hes 21:5; Flp 3:19; Mt 6:24-34; Rum 8:7Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu. 611:6 Kut 16:14Lakini sasa tumepoteza hamu ya chakula; hatuoni kitu kingine chochote isipokuwa hii mana!”

711:7 Kut 16:31; Mwa 2:12; 2:12Mana ilifanana kama mbegu za giligilani, nayo ilikuwa na rangi ya manjano iliyopauka. 811:8 Kut 16:16Hao watu walikwenda kukusanya, kisha waliisaga kwa mawe ya kusagia ya mkono au kuitwanga kwenye vinu. Waliipika vyunguni au kutengeneza maandazi. Ladha yake ilikuwa kama kitu kilichotengenezwa kwa mafuta ya zeituni. 911:9 Kut 16:13Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao.

10Mose akasikia watu wa kila jamaa wakilia, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake. Bwana akakasirika mno, naye Mose akafadhaika. 1111:11 Mwa 34:30; Kut 5:22; 18:18; 17:4; Kum 1:12; Yer 15:10, 18; 20:7-18; Mal 3:14; 2Kor 11:28Akamuuliza Bwana, “Kwa nini umeleta taabu hii juu ya mtumishi wako? Nimekufanyia nini cha kukuchukiza hata ukaweka mzigo huu wa watu hawa wote juu yangu? 1211:12 Isa 40:11; 49:23; 66:11, 12; Hes 14:16; Mwa 12:7; Kut 13:5; Eze 34:23; Yn 10:11; 1The 2:7; Mwa 22:16; 26:3Je, watu hawa wote mimi ndiye niliyewatungisha mimba? Je, ni mimi niliyewazaa? Kwa nini unaniambia niwachukue mikononi mwangu, kama vile mlezi abebavyo mtoto mchanga, hadi kwenye nchi uliyowaahidi baba zao? 1311:13 Kut 12:37; Yn 6:5-9; 2Fal 4:43; Mt 15:33; Mk 8:4Nitapata wapi nyama kwa ajili ya watu wote hawa? Wanaendelea kunililia wakisema, ‘Tupe nyama tule!’ 1411:14 Kut 18:18Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu. 1511:15 Kut 32:32; 1Fal 19:4; Ay 6:9; 7:15-16; 9:21; Isa 38:12; Yn 4:3Kama hivi ndivyo unavyonitendea, uniue sasa hivi, yaani kama nimepata kibali machoni pako, wala usiniache nione maangamizi yangu mwenyewe.”

1611:16 Kut 3:16; 18:25; 40:2; 24:1, 9Bwana akamwambia Mose: “Niletee wazee sabini wa Israeli, unaowafahamu kama viongozi na maafisa miongoni mwa watu. Walete katika Hema la Kukutania, ili waweze kusimama huko pamoja nawe. 1711:17 Kut 18:18; 19:20; 1Sam 10:6; 2Fal 2:9, 15; 3:12; Isa 32:15; Yoe 2:28; Hag 2:5; Yer 19:1Nami nitashuka na kusema nawe huko. Nami nitachukua sehemu ya Roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao. Watakusaidia kubeba mzigo wa watu hao ili usije ukaubeba peke yako.

1811:18 Kut 19:10; 16:7; Mdo 7:39; Za 78:20“Waambie hao watu: ‘Jiwekeni wakfu wenyewe kwa ajili ya kesho, wakati mtakapokula nyama. Bwana aliwasikia mlipolia, mkisema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! Tulikuwa na hali nzuri zaidi katika nchi ya Misri!” Sasa Bwana atawapa nyama, nanyi mtaila. 19Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini, 2011:20 Za 78:29; 106:14-15; Law 26:43; Ay 1:14; 20:13, 23; Yos 24:27; Amu 8:23; 1Sam 10:19; Isa 59:13; Hos 13:11bali kwa mwezi mzima mpaka iwatokee puani, nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataa Bwana, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”

2111:21 Kut 12:37Lakini Mose alisema, “Mimi niko hapa miongoni mwa watu 600,000 wanaotembea kwa miguu, nawe umesema, ‘Nitawapa nyama ya kula kwa mwezi mzima!’ 2211:22 Mt 15:33; 2Fal 7:2; Mk 6:37Je, wangeweza kupata nyama ya kuwatosha hata kama makundi ya kondoo na ya ngʼombe yangechinjwa kwa ajili yao? Je, wangetosheka hata kama samaki wote wa baharini wangevuliwa kwa ajili yao?”

2311:23 Isa 50:2; 59:1; Hes 23:19; 1Sam 15:29; Eze 12:25; 24:14Bwana akamjibu Mose, “Je, mkono wa Bwana ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”

24Kwa hiyo Mose akatoka na kuwaambia watu lile ambalo Bwana alikuwa amesema. Akawakusanya wazee wao sabini, akawasimamisha kuzunguka Hema. 2511:25 Kut 19:9; Hes 12:5; 1Sam 10:6, 10; 19:20, 23; Mdo 2:17; Amu 3:10; Kut 34:5; 40:38; 2Fal 2:15; Yoe 2:29; 1Kor 14:1Kisha Bwana akashuka katika wingu na kunena na Mose, naye akachukua sehemu ya Roho iliyokuwa juu ya Mose na kuiweka juu ya wale wazee sabini. Roho aliposhuka juu yao, wakatoa unabii, lakini hawakufanya hivyo tena.

2611:26 1Nya 12:18; Ufu 1:10; 1Sam 20:26; Yer 36:5Lakini, watu wawili, ambao majina yao ni Eldadi na Medadi, walibaki kambini. Walikuwa wameorodheshwa miongoni mwa wale wazee sabini, lakini hawakutoka kwenda kwenye Hema. Lakini Roho pia alishuka juu yao, nao wakatabiri huko kambini. 27Mwanaume mmoja kijana alikimbia na kumwambia Mose, “Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.”

2811:28 Kut 17:9; 33:11; Hes 13:8; 26:65; Yos 14:10; Mk 9:38-40; Mdo 26:29; 1Kor 14:5Yoshua mwana wa Nuni, ambaye alikuwa msaidizi wa Mose tangu ujana wake, akajibu akasema, “Mose bwana wangu, wanyamazishe!”

2911:29 1Sam 10:5; 19:20; 2Nya 24:19; Yer 7:25; 44:4; 1Kor 14:5; Hes 27:18Lakini Mose akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote wa Bwana wangekuwa manabii na kwamba Bwana angeweka Roho yake juu yao!” 30Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini.

3111:31 Kut 16:13; Za 78:26-28Kisha ukatokea upepo kutoka kwa Bwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande. 3211:32 Kut 16:36; Eze 45:11Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.11:32 Homeri 10 ni sawa na kilo 1,000. Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote. 3311:33 Za 78:30; 106:15, 29; Hes 14:18; Kum 9:7; Amu 2:12; 2Fal 22:17; Yer 44:3; Eze 8:17; Isa 10:16Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni. 3411:34 Hes 33:16; Kum 9:22Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava,11:34 Kibroth-Hataava maana yake Makaburi ya wenye tamaa nyingi. kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine.

3511:35 Hes 33:17; Kum 1:1Kutoka Kibroth-Hataava watu wakasafiri mpaka Haserothi na kukaa huko.