Hesabu 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 1:1-54

Watu Wahesabiwa Kwa Mara Ya Kwanza

11:1 Kut 27:21; 40:2; 19:1; 6:14; 40:17; Hes 10:12Bwana alisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia, 21:2 Kut 30:11-16; Hes 3:40; 26:2; 1Nya 21:2; 2Sam 24:2“Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja. 31:3 Kut 4:14; 30:14; Hes 17:3; 26:2; Yos 5:4; 1Nya 5:18Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi. 41:4 Law 24:11; Hes 7:2; 30:1; 31:26; 34:18; Kut 18:21; Kum 1:15; Yos 22:14Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia. 51:5 Hes 2:10; 7:30; 10:18; 17:2; Mwa 29:32; Ufu 7:4-5Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia:

“kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;

61:6 Hes 25:14; 2:12; 7:36; 10:19kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;

71:7 Mwa 29:35; Za 78:68; Kut 6:23; Hes 7:12; Rut 4:20; 1Nya 2:10; Lk 3:32kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;

81:8 Mwa 30:18; Hes 10:15; 2:5; 7:18kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;

91:9 Hes 10:16; 2:7; 7:24kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

101:10 Hes 2:18, 20; 7:48-53; 10:22-23kutoka wana wa Yosefu:

kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi;

kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;

111:11 Hes 10:24; 2:22; 7:60; Za 68:27kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;

121:12 Hes 2:25; 7:66; 10:25kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;

131:13 Hes 10:26; 2:27; 7:72kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

141:14 Hes 10:20; 2:14; 7:42kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

151:15 Hes 10:27; 2:29; 7:78kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

161:16 Kut 18:25; Hes 32:28; Mwa 6:4; 1Nya 5:24; Amu 6:15Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.

17Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao, 181:18 Ezr 2:59; Ebr 7:3; Kut 30:14wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, 191:19 Kut 30:12; Hes 26:63; 31:49kama Bwana alivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

201:20 Mwa 10:15; 29:32; 46:9; Ufu 7:5Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 211:21 Hes 26:7Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.

221:22 Mwa 29:33; Ufu 7:7; 2Sam 22:35; Za 60:12; Efe 6:12Kutoka wazao wa Simeoni:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 231:23 Hes 26:14Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.

241:24 Mwa 30:11; Yos 13:24-28; Ufu 7:5Kutoka wazao wa Gadi:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 251:25 Mwa 46:16; Hes 26:18; 1Nya 5:11Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.

261:26 Mt 1:2; Mwa 29:35; Ufu 7:5; Mwa 49:8-10; Za 78:68; Ebr 7:14Kutoka wazao wa Yuda:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 271:27 Hes 26:22Idadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu 74,600.

281:28 Mwa 30:18; Ufu 7:7Kutoka wazao wa Isakari:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 291:29 Mwa 30:18; Hes 26:25Idadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu 54,400.

301:30 Mwa 30:20; Ufu 7:8Kutoka wazao wa Zabuloni:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 311:31 Hes 26:27Idadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu 57,400.

321:32 Mwa 49:26; 41:52; Hes 26:35-37; Za 60:7; Yer 7:15Kutoka wana wa Yosefu:

Kutoka wazao wa Efraimu:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 331:33 Hes 26:37; 1Nya 7:20Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.

341:34 Mwa 41:51; Ufu 7:6Kutoka wazao wa Manase:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 35Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.

361:36 Mwa 35:18; 2Nya 17:17; Yer 32:44; Oba 1:19; Ufu 7:8Kutoka wazao wa Benyamini:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 371:37 Hes 26:41Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.

381:38 Mwa 30:6; Kum 33:22Kutoka wazao wa Dani:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 391:39 Hes 26:43Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.

401:40 Mwa 30:13; Hes 26:44; Ufu 7:6Kutoka wazao wa Asheri:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 411:41 Hes 26:47Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.

421:42 Mwa 30:8; Ufu 7:6Kutoka wazao wa Naftali:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. 431:43 Hes 26:50; Kut 1:1-4Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.

441:44 Hes 26:64Hawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Mose, Aroni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake. 451:45 Hes 14:29; 2:32Wanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli walihesabiwa kufuatana na jamaa zao. 461:46 Kut 12:37; 2Sam 24:9; Mwa 13:16; Kut 38:26; Hes 26:51; 1Fal 4:20Jumla ya hesabu yao ilikuwa watu 603,550.

471:47 Hes 3:17-20; 26:57; 4:3, 49; 1Nya 21:6Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine. 48Bwana alikuwa amemwambia Mose: 491:49 Hes 26:62“Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine. 501:50 Kut 31:18; 15:9; 16:34; Mdo 7:44; Hes 4:15-33Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka. 511:51 Kut 21:12; 26:1; Hes 4:5, 15; 3:38Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa. 521:52 Hes 10:14; Za 20:4-5; Wim 2:4; 6:4Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake. 531:53 Hes 2:10; 3:23-38; 16:46; 18:2-5; Law 10:6; Kum 9:22; Kut 38:21; 1Nya 23:32; 2Nya 13:10Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

54Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kama Bwana alivyomwamuru Mose.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

民数记 1:1-54

以色列的第一次人口统计

1以色列人离开埃及后第二年的二月一日,耶和华在西奈旷野的会幕中对摩西说: 2“你要按以色列人的宗族和家系统计全体会众,登记所有男子的名字。 3你和亚伦要一队一队地统计以色列人中所有二十岁以上、有作战能力的男子。 4每一支派要有一个人来协助你们。他们都是各宗族的族长, 5名单如下:

吕便支派示丢珥的儿子以利苏6西缅支派苏利沙代的儿子示路蔑7犹大支派亚米拿达的儿子拿顺8以萨迦支派苏押的儿子拿坦业9西布伦支派希伦的儿子以利押10约瑟的后裔——以法莲支派亚米忽的儿子以利沙玛玛拿西支派比大苏的儿子迦玛列11便雅悯支派基多尼的儿子亚比但12支派亚米沙代的儿子亚希以谢13亚设支派俄兰的儿子帕结14迦得支派丢珥的儿子以利雅萨15拿弗他利支派以南的儿子亚希拉。”

16他们都是从会众中选出来的,是各支派的首领,也是以色列的将领。

17摩西亚伦带着这些被点名的人, 18在二月一日招聚全体会众,按照宗族和家系统计人口,一一登记所有二十岁以上的男子。 19摩西照耶和华的吩咐在西奈旷野统计人口。

20-21以色列的长子吕便支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有四万六千五百人。

22-23西缅支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有五万九千三百人。

24-25迦得支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有四万五千六百五十人。

26-27犹大支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有七万四千六百人。

28-29以萨迦支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有五万四千四百人。

30-31西布伦支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有五万七千四百人。

32-33约瑟的后裔中,以法莲支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有四万零五百人。

34-35玛拿西支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有三万二千二百人。

36-37便雅悯支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有三万五千四百人。

38-39支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有六万二千七百人。

40-41亚设支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有四万一千五百人。

42-43拿弗他利支派中,二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来,共有五万三千四百人。

44以上就是摩西亚伦和各代表自己族系的十二位以色列首领所统计的男子人数。 45这样,以色列人中二十岁以上、有作战能力的男子按宗族、家系和名字一一被登记下来, 46共有六十万三千五百五十人。 47然而,利未人没有按祖先的支派列在其中, 48因为耶和华曾经对摩西说: 49“你不可统计利未支派的人数,不可把他们的人数算在以色列人中。 50你要派利未人管理、搬运和照料放约柜的圣幕及其所有器具和附属物,他们要在圣幕四围扎营。 51在迁移的时候,利未人要负责拆卸和支搭圣幕。外人若近前来,必被处死。 52以色列人要按照他们的队伍各自扎营,各归本旗。 53利未人要在安放约柜的圣幕四周扎营,以免以色列人触怒耶和华。利未人负责看守放约柜的圣幕。” 54以色列人就按耶和华对摩西的吩咐行了。