Hagai 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hagai 2:1-23

Utukufu Ulioahidiwa Wa Nyumba Mpya

12:1 Law 23:34; Yn 7:37; Ezr 5:1Katika siku ya ishirini na moja ya mwezi wa saba, neno la Bwana lilikuja kupitia nabii Hagai, kusema: 22:2 Hag 1:12; 1Nya 6:15“Sema na Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, na mabaki ya watu. Uwaulize, 32:3 Ezr 3:12; Isa 60:7; Zek 4:10‘Ni nani miongoni mwenu aliyebaki ambaye aliiona hii nyumba katika utukufu wake wa mwanzo? Sasa inaonekanaje kwenu? Je, haionekani kwenu kama si kitu? 42:4 Zek 8:9; Hag 1:13; 1Sam 16:18; Mk 16:20; Rum 8:31; 1Nya 28:20; Efe 6:10; Kut 3:12; 33:14; Hes 14:9; Mdo 7:9; 2Sam 5:10Lakini sasa uwe imara, ee Zerubabeli,’ asema Bwana. ‘Kuwa imara, ee kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Mwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema Bwana, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 52:5 Mwa 6:18; 15:1; Kut 29:46; Neh 9:20; Zek 4:6; 8:13; Isa 63:11; Ezr 5:2; 1Nya 28:20‘Hili ndilo nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri. Pia Roho wangu anadumu katikati yenu. Msiogope.’

62:6 Kut 19:18; Ay 9:6; Isa 10:25; 14:16; 34:4; Eze 38:19; Yer 4:26; Ebr 12:26“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Baada ya muda kidogo kwa mara nyingine nitazitikisa mbingu na nchi, bahari na nchi kavu. 72:7 1Sam 9:20; Isa 60:7; Mwa 3:15; Kum 18:15; Za 24:7; Lk 2:32; Kut 16:7; 29:43Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 82:8 1Nya 29:2‘Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 92:9 Za 85:9; Isa 9:6; 11:10; 60:7, 17; Law 26:6; Ezr 3:12; Lk 11:31; 2:14; Yn 1:14‘Utukufu wa nyumba hii ya sasa utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa ile nyumba ya mwanzoni,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. ‘Na mahali hapa nitawapa amani,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

Baraka Kwa Watu Waliotiwa Unajisi

102:10 Hag 1:15Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilikuja kwa nabii Hagai: 112:11 Law 10:10-11; Kum 17:8-11; 33:8; Yer 18:18“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ulizeni makuhani jinsi sheria inavyosema: 122:12 Yer 11:15; Mwa 7:2Kama mtu akibeba nyama iliyowekwa wakfu katika pindo la vazi lake, kisha lile pindo likagusa mkate au mchuzi, divai, mafuta au chakula kingine, je, kitu hicho kitakuwa kimewekwa wakfu?’ ”

Makuhani wakajibu, “La hasha.”

132:13 Law 22:4-6; Hes 19:13Kisha Hagai akasema, “Je, kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti akigusa mojawapo ya vitu hivi, kitu hicho kitakuwa kimetiwa unajisi?”

Makuhani wakajibu, “Ndiyo, huwa kimenajisiwa.”

142:14 Isa 1:13; 29:13; Tit 1:14-15; Za 51:17Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema Bwana. ‘Lolote wafanyalo na chochote watoacho hapo ni najisi.

152:15 Ezr 3:10; 4:24; Hag 1:5“ ‘Sasa fikirini kwa uangalifu kuanzia leo na kuendelea: tafakarini jinsi mambo yalivyokuwa kabla halijawekwa jiwe moja juu ya lingine katika Hekalu la Bwana. 162:16 Rut 3:7; Ay 24:11; Isa 5:2, 10; Hag 1:6; Kum 28:38Wakati mtu alipoendea lundo la nafaka la vipimo ishirini, kulikuwa na vipimo kumi tu. Wakati mtu alipoendea pipa la mvinyo ili kuchota vipimo hamsini, kulikuwa na vipimo ishirini tu. 172:17 Hag 1:11; Kut 9:18; Kum 28:22; Za 78:48; Isa 9:13; Amo 4:6; 1Fal 8:37; Yer 3:10; 5:3Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asema Bwana. 182:18 Zek 8:9; Hag 1:5; Ezr 3:11‘Tangu leo na kuendelea, kuanzia siku hii ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, tafakarini siku ambayo msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa. Tafakarini: 192:19 Kut 28:33; Yoe 1:12; 2:14; Mwa 12:2; Law 25:21; Za 128:1-6Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Mpaka sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda.

“ ‘Kuanzia leo na kuendelea, nitawabariki.’ ”

Zerubabeli Pete Ya Muhuri Ya Bwana

202:20 Ezr 1:5; Hag 1:15Neno la Bwana likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema: 212:21 Ezr 5:2; Isa 14:16; Eze 21:27; 38:19-20; Ebr 12:26“Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi. 222:22 Mwa 19:25; Ay 2:13; Dan 2:44; Mik 5:10; Mt 24:7; Kut 15:21; Eze 38:21; Amu 7:22Nitapindua viti vya enzi vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake.

232:23 Zek 4:10; Kut 28:9; Dan 9:24-26; Mwa 38:18; 2Kor 1:22; Mt 1:12; Wim 8:6; Yer 22:24; Isa 2:11; 10:20; 20:3; 2:1“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Bwana. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”