Hagai 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Hagai 1:1-15

Wito Wa Kuijenga Nyumba Ya Bwana

11:1 Ezr 4:24; 5:1-3; 2:2; 3:2; 1Nya 3:19; 6:15; Mt 1:12-13Katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario wa Uajemi, katika siku ya kwanza ya mwezi wa sita, neno la Bwana lilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda na kwa Yoshua1:1 Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu. mwana wa kuhani mkuu Yehosadaki:

21:2 Isa 13:4; 29:13Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya Bwana.’ ”

31:3 Ezr 5:1Kisha neno la Bwana likaja kupitia kwa nabii Hagai: 41:4 2Sam 7:2; Yer 33:12“Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki, gofu?”

51:5 Mao 3:40; Hag 2:15-18Sasa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. 61:6 Law 26:20; Isa 5:10; 9:20; 55:2; Amo 4:8; Hag 2:16; Zek 8:10Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”

7Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. 81:8 Ay 22:3; Yer 13:11; 1Nya 14:1; Za 132:13-14; Kut 29:43Pandeni milimani mkalete miti na kujenga nyumba, ili nipate kuifurahia, na nitukuzwe,” asema Bwana. 91:9 Kum 28:38; Isa 5:10; Neh 13:11; Za 103:16; Eze 22:21“Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe. 101:10 Kum 28:24; Mwa 27:28; 1Fal 17:1; 2Nya 6:26; Yer 3:3; Law 26:19; Yoe 1:18-19Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake. 111:11 Kum 11:26; 28:22; Rut 1:1; 1Fal 17:1; Hag 2:17; Isa 5:6; 7:25; Hes 18:12Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na chochote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ngʼombe, pamoja na kazi za mikono yenu.”

121:12 Isa 1:9; 50:10; 55:11; Mt 28:20; Kum 31:12; Hag 2:2; Ezr 5:2; Mhu 12:13; Ay 36:11Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Bwana Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Bwana Mungu wao. Watu walimwogopa Bwana.

131:13 Hes 14:9; 27:21; 2Nya 15:2; 36:15; Mwa 26:3; Rum 8:31; Isa 41:10; Mt 28:20Kisha Hagai, mjumbe wa Bwana, akawapa watu ujumbe huu wa Bwana: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema Bwana. 141:14 Ezr 5:2; Za 110:3; 2Nya 36:22; Hag 2:21; 1Nya 6:15; 1Kor 15:58Kwa hiyo Bwana akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao, 151:15 Hag 2:10, 20; Ezr 4:24katika siku ya ishirini na nne mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.