Habakuki 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Habakuki 2:1-20

12:1 Isa 21:8; Za 48:13; 85:8; Eze 3:17; Za 73:16, 17; 5:3Nitasimama katika zamu yangu,

na kujiweka mwenyewe juu ya maboma;

nitatazama nione atakaloniambia,

na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili.

Jibu La Bwana

22:2 Isa 8:1; 30:8; Kum 27:8; Rum 4:24; 15:4; Yer 36:2; Eze 24:2; Ufu 1:19Kisha Bwana akajibu:

“Andika ufunuo huu,

na ukaufanye wazi juu ya vibao,

ili mpiga mbiu akimbie nao.

32:3 Dan 10:14; 11:27; 8:17; Za 27:14; Eze 12:25Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;

unazungumzia mambo ya mwisho,

na kamwe hautakosea.

Iwapo utakawia, wewe usubiri;

kwa hakika utakuja na hautachelewa.

42:4 Eze 18:9; Yn 3:36; 2Kor 5:7; Rum 1:17; Gal 3:11; Ebr 10:37-38“Tazama, amejaa majivuno;

anavyovitamani si vya unyofu:

lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake:

52:5 Mit 20:1; Isa 2:11; Mit 27:20; 30:15-16; Hab 1:9hakika mvinyo humsaliti;

ni mwenye kiburi na hana amani.

Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu

na kama kifo kamwe hatosheki;

anajikusanyia mataifa yote

na kuchukua watu wote mateka.

62:6 Isa 14:4; Amo 2:8“Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema,

“ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa

na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu!

Ataendelea hivi kwa muda gani?’

72:7 Mit 29:1Je, wadai wako hawatainuka ghafula?

Je, hawataamka na kukufanya utetemeke?

Kisha utakuwa mhanga kwao.

82:8 Zek 1:122:8 Isa 33:1; Yer 50:17-18; Oba 1:15; Zek 2:8-9; Eze 39:10Kwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi,

watu waliobaki watakuteka nyara wewe.

Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu;

umeharibu nchi na miji, na kila mmoja ndani yake.

92:9 Yer 22:13; 51:13; Ay 39:27; Isa 10:14“Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu,

awekaye kiota chake juu,

ili kukimbia makucha ya uharibifu!

102:10 Yer 26:19; Nah 3:6Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi,

ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako.

112:11 Yos 24:27; Zek 5:4; Lk 19:40Mawe ya kuta yatapiga kelele,

na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake.

122:12 Eze 22:2; Mik 3:10“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga

damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

132:13 Isa 50:11; 47:13Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha

kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto,

na kwamba mataifa

yanajichosha bure?

142:14 Kut 16:7; Hes 14:21; Isa 11:9Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana,

kama maji yaifunikavyo bahari.

152:15 Mit 23:20“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo,

akiimimina kutoka kwenye kiriba

cha mvinyo mpaka wamelewa,

ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.

162:16 Eze 23:32-34; Hos 4:7; Law 10:9; Mao 4:21; Za 16:5; Isa 51:22Utajazwa na aibu badala ya utukufu.

Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue!

Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia,

na aibu itafunika utukufu wako.

172:17 Yer 50:33; 51:35; 50:15Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika,

na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha.

Kwa sababu umemwaga damu ya mtu;

umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.

182:18 1Sam 12:21; Amu 10:14; Isa 40:19; Yer 5:21; 14:22; 10:14; 1Kor 12:2“Sanamu ina thamani gani,

kwani mwanadamu ndiye alichonga?

Ama kinyago kinachofundisha uongo?

Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza

hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe;

hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.

192:19 1Fal 18:27; Yer 10:4; Hos 4:12; Dan 5:4, 23Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’

Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’

Je, linaweza kuongoza?

Limefunikwa kwa dhahabu na fedha;

hakuna pumzi ndani yake.

202:20 Za 11:4; Isa 41:1Lakini Bwana yuko katika Hekalu lake takatifu;

dunia yote na inyamaze mbele yake.”