Ezra 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezra 7:1-28

Ezra Awasili Yerusalemu

17:1 Ezr 4:7; Neh 2:1; 1Nya 6:14Baada ya mambo haya, wakati wa utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia, 27:2 1Fal 2:35; Eze 40:46; Neh 11:11mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu, 3mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi, 4mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki, 5mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani mkuu Aroni. 67:6 Neh 12:36; Ezr 5:5; Isa 41:20; Mwa 32:28; Neh 1:10-11Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika sheria ya Mose, ambayo Bwana, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye. 77:7 Ezr 8:1; 2:43Pia baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu,7:7 Yaani Wanethini (pia 7:24). nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.

8Ezra aliwasili Yerusalemu mwezi wa tano wa mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta. 97:9 Neh 2:8Ezra alianza safari yake kutoka Babeli tangu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa maana mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake. 107:10 Kum 33:10; Neh 8:1-8; 2Tim 4:2; 1Sam 7:3; 2Nya 12:14; Za 10:18; 119:45; Mal 2:7Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya Bwana na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.

Barua Ya Ezra Kutoka Kwa Mfalme Artashasta

11Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alikuwa amempa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo yahusuyo maagizo na amri za Bwana kwa Israeli.

127:12 Eze 26:7; Dan 2:37; Ezr 4:10Artashasta, mfalme wa wafalme,

Kwa Ezra kuhani, mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni:

Salamu.

13Sasa naamuru kwamba mtu yeyote Mwisraeli katika ufalme wangu, pamoja na makuhani na Walawi, ambaye anataka kwenda Yerusalemu pamoja nawe aweza kwenda. 147:14 Es 1:14Unatumwa na mfalme na washauri wake saba kuchunguza kuhusu Yuda na Yerusalemu kulingana na Sheria ya Mungu wako, iliyoko mkononi mwako. 157:15 Kum 12:5; 1Nya 29:6; 2Nya 6:2; Za 135:21Zaidi ya hayo, uchukue pamoja nawe fedha na dhahabu ambazo mfalme na washauri wake wamempa Mungu wa Israeli kwa hiari, Mungu ambaye maskani yake yako Yerusalemu, 167:16 Kut 3:22; Ezr 8:25; Zek 6:10; 1Nya 29:6pia fedha na dhahabu zote unazoweza kupata kutoka jimbo la Babeli, pamoja na sadaka za hiari watakazotoa watu na makuhani kwa ajili ya Hekalu la Mungu wao katika Yerusalemu. 177:17 2Fal 3:5; Hes 15:5-12; Kum 12:5-11Hakikisha kwamba fedha hizi zimetumika kununua mafahali, kondoo dume na wana-kondoo pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, uvitoe dhabihu juu ya madhabahu ya Hekalu la Mungu wenu katika Yerusalemu.

18Kisha wewe na Wayahudi ndugu zako mnaweza kufanya lolote linaloonekana jema sana kwa fedha na dhahabu zilizosalia, kulingana na mapenzi ya Mungu wenu. 197:19 Ezr 5:14; Yer 27:22Uvitoe kwa Mungu wa Yerusalemu vyombo vyote ulivyokabidhiwa kwa ajili ya ibada katika Hekalu la Mungu wako. 207:20 Ezr 6:4; 1Kor 4:1-2Kitu kingine chochote kinachohitajika kwa ajili ya Hekalu la Mungu wenu ambacho unatakiwa kukitoa, waweza kukitoa kutoka hazina ya mfalme.

217:21 Ezr 4:16-20; 5:3-6Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ngʼambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu, 22talanta 1007:22 Talanta 100 za fedha ni sawa na kilo 3,400. za fedha, ngano kori 100,7:22 Kori 100 za ngano ni sawa na kilo 10,000. divai bathi 100,7:22 Bathi 100 za divai ni sawa na lita 2,000. mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote. 237:23 Ezr 6:10; Isa 60:12; Yer 12:14; Za 68:29; 1Tim 2:1-2Chochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe? 247:24 Ezr 4:13; 8:36Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.

257:25 Kut 18:21-26; 16:18; Za 19:7; Kol 1:28; Kum 16:18; 2Nya 17:7; Mal 2:7; Mt 13:52Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu. 267:26 Eze 6:11Yeyote ambaye hataitii sheria ya Mungu wenu pia sheria ya mfalme, hakika lazima aadhibiwe kwa kuuawa, kuhamishwa, kunyangʼanywa mali au kufungwa gerezani.

277:27 Ezr 6:22; 1Nya 29:12; Neh 2:12; 2Kor 8:16; Flp 4:10; Mit 16:7Sifa ziwe kwa Bwana, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu, kwa namna hii 287:28 2Fal 25:28; Ezr 5:5; 9:9; Neh 1:117:28 Neh 8:7; Rum 8:28; Mit 3:6; Law 10:10-11; 2Nya 30:22ambaye ameniongezea kibali chake mbele ya mfalme, washauri wake na maafisa wote wa mfalme wenye uwezo. Kwa kuwa mkono wa Bwana Mungu wangu ulikuwa pamoja nami, nilijipa moyo nikakusanya watu walio viongozi kutoka Israeli wakwee pamoja nami.