Ezekieli 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 8:1-18

Ibada Ya Sanamu Hekaluni

18:1 2Fal 6:32; Eze 14:1; 33:31; 40:1; 24:1Katika siku ya tano ya mwezi wa sita mwaka wa sita, baada ya kupelekwa uhamishoni nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda walikuwa wameketi mbele yangu, mkono wa Bwana Mwenyezi ulikuja juu yangu. 28:2 Eze 1:4, 26-27; Dan 7:9Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma kingʼaavyo kikiwa ndani ya moto. 38:3 Eze 3:12; 11:1; Kut 20:5; Kum 32:16; Yer 7:30; Kut 24:10; Eze 2:9Akanyoosha kitu kilichoonekana kama mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho akaniinua juu kati ya nchi na mbingu nikiwa katika maono ya Mungu akanichukua mpaka Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la upande wa kaskazini ya ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu ichocheayo wivu. 48:4 Kut 24:16; Eze 1:28; 3:22Hapo mbele yangu palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule ua wa ndani.

58:5 Za 78:58-60; Yer 4:1; 32:34Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio upande wa kaskazini wa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu.

68:6 Eze 5:11; Kum 31:16; Hos 5:6Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayofanya, haya mambo ya machukizo kabisa nyumba ya Israeli wanayotenda hapa, ambayo yatanifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utaona vitu ambavyo vinachukiza zaidi hata kuliko hivi.”

7Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. 8Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango.

9Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.” 108:10 Kum 4:15-18; Yer 16:18; Amu 17:4-5; Eze 23:14; Yer 44:4; Kut 20:4Hivyo nikaingia ndani na kutazama, nikaona kuta zote zimechorwa kila aina ya vitu vitambaavyo na ya wanyama wachukizao wa kila aina na sanamu zote za nyumba ya Israeli. 118:11 Hes 16:17; Yer 26:24; Law 10:1; Hes 16:17-35; Kut 3:16; Eze 11:1-2Mbele yao walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu.

128:12 2Fal 21:16; Za 10:11; Ay 22:13; Isa 29:15; Eze 9:9Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mmoja kwenye sehemu yake mwenyewe ya kufanyia ibada za sanamu yake? Wao husema, ‘Bwana hatuoni, Bwana ameiacha nchi.’ ” 13Akasema tena, “Bado utaona machukizo wanayofanya ambayo ni makubwa kuliko haya.”

148:14 Eze 11:12Ndipo akanileta mpaka ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Bwana, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi. 15Akaniambia, “Unaliona hili, mwanadamu? Utaona vitu ambavyo ni machukizo kuliko hili.”

168:16 Yoe 2:17; Kum 4:19; Ay 31:28; Mwa 1:16; Yer 2:27; Eze 40:6; 9:6Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Bwana, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwepo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la Bwana na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki.

178:17 Mwa 6:11; Ezr 9:6; Hes 11:33; 1Fal 14:9; Eze 16:2; 16:26Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka! 188:18 Yer 13:14; 44:6; Eze 24:14; Isa 1:15; Mik 3:4; Mit 1:28; 1Sam 8:18; Isa 58:4; Eze 9:10Kwa hiyo nitashughulika nao kwa hasira, sitawaonea huruma wala kuwaachilia. Wajapopiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

以西結書 8:1-18

聖城中的可憎之事

1第六年六月五日,我正在家中與猶大的眾長老同坐,主耶和華的手按在我身上。 2我觀看,只見有一位形狀像人,祂的腰部以下像火,腰部以上像閃亮的金屬。 3祂好像伸出一隻手,抓住我的頭髮。在異象中,耶和華的靈把我舉到天地之間,將我帶到耶路撒冷聖殿內院的北門,那裡供奉著惹耶和華憤恨的神像。 4我忽然看見那裡有以色列上帝的榮耀,跟我在平原所見的一樣。

5祂對我說:「人子啊,你舉目北望。」於是,我舉目朝北一望,見在祭壇門北面的入口處有惹耶和華憤恨的神像。 6祂又對我說:「人子啊,你看見以色列人的所作所為了嗎?他們在這裡行那些極其可憎的事,以致我遠離我的聖所。你會看到更可憎的事。」

7祂帶我到院子的門口,我看見牆上有一個洞。 8祂對我說:「人子啊,你挖這牆。」我挖開牆後,看見一道門。 9祂對我說:「你進去看看他們在這裡做的邪惡可憎的事吧。」 10我進去後,看見四周的牆上畫滿了各種爬蟲、可憎的獸類和以色列人拜的所有偶像。 11偶像前面站著以色列的七十個長老,沙番的兒子雅撒尼亞也在當中,他們每人手中都拿著香爐,煙霧繚繞。 12祂又對我說:「人子啊,你看見以色列的長老在自己藏偶像的房間裡暗中所做的了嗎?他們說,『耶和華看不見我們,祂已經拋棄了這片土地。』」 13祂繼續說:「你會看到他們做更可憎的事。」

14祂帶我來到耶和華殿的北門,看見一些婦女坐在那裡為搭模斯神像哭泣。 15祂對我說:「人子啊,你看見了嗎?你會看到更可憎的事。」

16祂帶我來到耶和華殿的內院,在殿門口,走廊和祭壇中間約有二十五個人背向耶和華的殿,面向東方朝拜太陽。 17祂又對我說:「人子啊,你看見了嗎?猶大人的這些可憎行徑還算小事嗎?他們到處行殘暴之事,再三惹我發怒。看啊,他們手拿樹枝舉向鼻前。 18因此,我必憤怒地對待他們,我必不顧惜他們,也不憐憫他們,即使他們大聲向我呼求,我也不聽。」