Ezekieli 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 7:1-27

Mwisho Umewadia

1Neno la Bwana likanijia kusema: 27:2 Amo 8:2-10; Ufu 20:8; Mao 4:18“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa nchi ya Israeli: Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi. 37:3 Eze 18:30; Mwa 6:13Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. 47:4 Yer 13:14; Eze 5:11; 23:49Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

57:5 2Fal 21:12“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa yanakuja. 67:6 Eze 39:8Mwisho umewadia! Mwisho umewadia! Umejiinua wenyewe dhidi yenu. Umewadia! 77:7 Sef 1:14; Mal 3:2; 1Pet 4:17; Ay 18:20; Isa 2:12; Amo 5:18-20; Eze 12:23Maangamizi yamekuja juu yenu, ninyi mnaoishi katika nchi. Wakati umewadia, siku imekaribia, kuna hofu kuu ya ghafula, wala si furaha, juu ya milima. 87:8 Hos 5:10; Nah 1:6; Eze 36:19; 14:19; 20:8, 21; 9:8; Isa 42:25Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu na kumaliza hasira yangu dhidi yenu, nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo. 97:9 Yer 21:9; Isa 9:13; Eze 5:11; 22:31; Za 39:10Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana ambaye huwapiga kwa mapigo.

107:10 Za 89:32; Isa 10:5“Siku imefika! Imewadia! Maangamizi yamezuka ghafula, fimbo imechanua majivuno yamechipua! 117:11 Yer 16:6; Sef 1:18; Isa 58:4; Za 55:9Jeuri imeinuka kuwa fimbo ya kuadhibu uovu, hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, hata mmoja wa kundi lile, hakuna utajiri, hakuna chenye thamani. 127:12 Isa 5:13-14; Eze 30:3; Isa 24:2Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na asifurahi wala muuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote. 137:13 Law 25:24-25Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai, kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake. 147:14 Ay 39:24; Yer 25:38Wajapopiga tarumbeta na kuweka kila kitu tayari, hakuna hata mmoja atakayekwenda vitani, kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote.

157:15 Kum 32:25; Yer 14:18; Mao 1:20; Eze 5:12; 33:27“Nje ni upanga, ndani ni tauni na njaa, wale walioko shambani watakufa kwa upanga, nao wale waliomo mjini njaa na tauni vitawala. 167:16 Mwa 8:8; Isa 59:11; 10:20; Ezr 9:15; Yer 9:19; 41:16; 42:17Wale wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake. 177:17 2Fal 19:26; Isa 13:7; Dan 6:5; Yer 43:7; Eze 21:7; 22:14Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. 187:18 Isa 15:2-3; Amo 8:10; Za 55:5; Yer 6:26; 4:8; 49:3; 48:37Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa. 197:19 Isa 42:25; Sef 1:18; Hos 4:5; Eze 3:20; Mit 11:4; Yoe 1:15; Eze 13:5; 14:3Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini. 207:20 Eze 5:11; 16:17; Yer 7:30; 10:3; Isa 2:20Walijivunia vito vyao vizuri na kuvitumia kufanya sanamu za machukizo na vinyago vya upotovu. Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao. 217:21 2Fal 24:13; Hes 14:3Nitavitia vyote mikononi mwa wageni kuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia, nao watavinajisi. 227:22 Yer 2:27; 19:13; Eze 39:23-24; Za 74:7-8Nitageuza uso wangu mbali nao, nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani, wanyangʼanyi watapaingia na kupanajisi.

237:23 2Fal 21:16; Isa 1:15; Za 10:8; Eze 11:6; 22:9; Mwa 6:11“Andaa minyororo, kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu na mji umejaa udhalimu. 247:24 Mao 2:7; Eze 24:21; 28:7; 2Nya 7:20Nitaleta taifa ovu kuliko yote ili kumiliki nyumba zao, nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi. 257:25 Yer 6:14; 8:11; Eze 13:10-16Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitakuwepo. 267:26 Kum 29:21; 31:17; Yer 4:20; 18:18; Amo 8:11; Mik 3:6; Mal 2:7-9; Isa 47:11; 3:11; Eze 18:20; Za 109:19Maafa juu ya maafa yatakuja, tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii, mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee. 27Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Bwana.”