Ezekieli 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 5:1-17

Upanga Dhidi Ya Yerusalemu

15:1 Law 21:5; Isa 7:20; Eze 44:20; Hes 6:5; 2Sam 10:14“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo. 25:2 Law 26:33; Yer 39:1-2; Zek 13:8; Yer 21:10; Eze 15:7; Yer 13:24; 9:16Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa. 35:3 Yer 40:6; 39:10; 2Fal 25:12; Za 74:11Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako. 45:4 Eze 10:7; 15:7Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka humo na kufika katika nyumba yote ya Israeli.

55:5 Kum 4:6; Mao 1:1; Eze 16:14“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Huu ndio Yerusalemu ambao nimeuweka katikati ya mataifa ukiwa umezungukwa na nchi pande zote. 65:6 Neh 9:17; Zek 7:11; Rum 1:25; Eze 16:16; 2Fal 17:15; Yer 11:10Lakini katika uovu wake umeasi sheria na amri zangu kuliko mataifa na nchi zinazouzunguka. Umeasi sheria zangu wala haukufuata amri zangu.

75:7 2Fal 21:9; 2Nya 33:9; Yer 2:10-11“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka.

85:8 Yer 21:5; Zek 14:2; Yer 24:9; Eze 11:9; 15:7“Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo, Mimi mwenyewe, niko kinyume nanyi Yerusalemu, nitawapiga kwa adhabu yangu mbele ya mataifa. 95:9 Dan 9:12; Amo 3:2; Mt 24:21Kwa ajili ya sanamu zenu zote za machukizo, nitawafanyia kile ambacho kamwe sijawafanyia kabla wala kamwe sitawafanyia tena. 105:10 Law 26:29; Mao 2:20; Yer 13:14; Zek 2:6; Za 44:11; Eze 12:14Kwa hiyo katikati yenu baba watakula watoto wao na watoto watakula baba zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami nitawatawanya watu wenu walionusurika pande zote za dunia. 115:11 Eze 7:20; 8:6; 2Nya 36:14; Eze 11:18-21; Yer 16:18; Ay 27:22; Hes 14:21; Law 15:2; 15:31; Mao 2:17Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbaya sana na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu. 125:12 Ufu 6:8; Za 107:39; Eze 12:14; Zek 13:8; Eze 6:11-12; Yer 21:9; 13:24Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa.

135:13 2Nya 12:7; Ay 20:23; Isa 1:24; Mao 4:11; Eze 21:17; 24:13; Hos 10:10“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi Bwana nimenena katika wivu wangu.

145:14 Mik 3:12; Isa 64:11; Neh 2:17; Za 74:3-10; Eze 22:4; Dan 9:16“Nitakuangamiza na kukufanya kitu cha kudharauliwa miongoni mwa mataifa yanayokuzunguka, machoni pa watu wote wapitao karibu nawe. 155:15 Kum 28:20; 1Fal 9:7; Yer 23:40; Eze 25:17; Mao 2:15; Isa 43:28; Yer 22:8-9Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi Bwana nimesema. 165:16 Law 26:26; Kum 32:24; Eze 14:21Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. 175:17 Eze 38:23; Law 26:25; Eze 28:22Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi Bwana nimenena haya.”