Ezekieli 46 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 46:1-24

Sheria Nyingine Mbalimbali

146:1 Eze 40:19; 1Nya 9:18; Isa 66:23“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa. 246:2 Eze 44:3; Mt 25:10; Eze 40:39Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni. 346:3 Za 100:4; Lk 1:10Siku za Sabato na za Mwezi mwandamo watu wote wa nchi wataabudu mbele za Bwana penye lile ingilio la ile njia. 446:4 Hes 28:5, 9, 11, 12; Eze 45:17Sadaka ya kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa Bwana siku ya Sabato itakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari. 546:5 Eze 45:24; Hes 28:12Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. 646:6 Hes 10:10; Law 22:20Siku ya mwezi mwandamo atatoa fahali mchanga, wana-kondoo sita na kondoo dume, wote wasiwe na dosari. 746:7 Eze 45:24Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. 846:8 Eze 46:2Wakati mkuu anayetawala aingiapo, atapitia kwenye baraza ya njia ya lango, naye atatoka nje kwa njia hiyo hiyo.

946:9 Kut 23:14; 34:20; Kum 16:16“ ‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za Bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia. 1046:10 2Sam 6:14-15; Za 42:4Mkuu anayetawala atakuwa miongoni mwao, akiingia nao ndani wanapoingia, naye atatoka nao nje wanapotoka.

1146:11 Eze 46:5“ ‘Kwenye sikukuu na kwenye sikukuu zilizoamriwa, sadaka ya nafaka itakuwa efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja pamoja na kondoo dume mmoja, pamoja na idadi ya wana-kondoo kama mtu apendavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. 1246:12 Eze 45:17; Gal 2:20; Yn 10:18; Law 7:16Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Bwana, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, naye akiisha kutoka nje, lango litafungwa.

1346:13 Kut 29:28; Hes 28:3; Za 5:3“ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, utaitoa kila siku asubuhi. 1446:14 Dan 8:11; Hes 15:6Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini46:14 Theluthi moja ya hini ni sawa na lita 1.3. ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Bwana ni amri ya daima. 1546:15 Kut 29:38-42; Hes 28:5-6Kwa hiyo mwana-kondoo na sadaka ya nafaka na mafuta vitatolewa kila siku asubuhi kwa ajili ya sadaka ya daima ya kuteketezwa.

1646:16 2Nya 21:3“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ikiwa mkuu atawalaye atatoa zawadi kutoka kwenye urithi wake na kumpa mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake, itakuwa mali yao kwa urithi. 1746:17 Law 25:9-10; Isa 61:2Hata hivyo, kama atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa watumishi wake, mtumishi anaweza kuiweka mpaka mwaka wa uhuru, kisha itarudishwa kwa mkuu anayetawala. Urithi wake ni wa wanawe peke yao, ni mali yao. 1846:18 Law 25:23; Mik 2:1-2; Za 78:72; Isa 8:14; Eze 45:8Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’ ”

1946:19 Eze 42:4-9Kisha mtu yule akanileta kwa kupitia kwenye ingilio lililokuwa kando ya lango mpaka kwenye vyumba vitakatifu vinavyoelekea kaskazini, ambavyo ni vya makuhani, naye akanionyesha mahali fulani upande wa mwisho wa magharibi. 2046:20 Law 6:27; Zek 14:20; Law 2:4-7Akaniambia, “Mahali hapa ndipo makuhani watakapotokosea sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na kuoka sadaka ya nafaka, kuepuka kuzileta katika ukumbi wa nje na kushirikisha utakatifu kwa watu.”

21Baada ya hapo akanileta kwenye ukumbi wa nje na kunizungusha kwenye pembe zake nne, nami nikaona katika kila pembe ya huo ukumbi kulikuwa na ukumbi mwingine. 22Katika pembe nne za huo ukumbi wa nje kulikuwa na kumbi nyingine, zenye urefu wa dhiraa arobaini na upana wake dhiraa thelathini, ambapo hizo kumbi kwenye hizo pembe nne zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. 23Mzunguko wa ndani wa hizo kumbi nne ulikuwa na ukingo wa jiwe, zikiwa na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya moto kuzunguka chini ya huo ukingo. 2446:24 Eze 46:20; Rum 12:1; 15:16; Ebr 13:16Akaniambia, “Hizi ndizo sehemu za kupikia ambazo wale wanaohudumu kwenye Hekalu watatokosea dhabihu za watu.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 46:1-24

君王与节期

1“主耶和华说,‘圣殿内院的东门在平时工作的六日内都要关闭,只在安息日和朔日才打开。 2在这些日子,君王要从东门穿过门廊通道进入内院,站在门框旁边。祭司要为他献燔祭和平安祭。他在入口的门槛那里敬拜,然后离去。这门要到晚上才关闭。 3在安息日和朔日,以色列人要站在这门口敬拜耶和华。 4君王在安息日献给耶和华的燔祭应是羊羔六只、公绵羊一只,都要毫无残疾。 5至于同献的素祭,一只公绵羊要同献十公斤细面粉,与羊羔同献的素祭则可随意奉献。每十公斤细面粉要加四升油。 6要在朔日献公牛犊一头、羊羔六只、公绵羊一只,都要毫无残疾。 7他也要预备素祭,每一头公牛犊要同献十公斤细面粉,公绵羊也是一样。与羊羔同献的素祭则可随意奉献。每十公斤细面粉要加四升油。 8君王从门廊进去,也要从原路出来。

9“‘以色列人在节期进去敬拜耶和华的时候,从北门进去的要从南门出来,从南门进去的要从北门出来。谁都不可回头从进去的门出来,必须从对面的门出来。 10在这些节期君王应和百姓一同进殿敬拜,百姓离开的时候,君王也要一同离开。

11“‘每逢节期和特定的圣会,要有与祭牲同献的素祭,每头公牛献十公斤细面粉,公绵羊也是一样,与羊羔同献的素祭则可以随意奉献。每十公斤细面粉要加四升油。 12倘若君王自愿向耶和华献燔祭或平安祭,便要为他打开东门。他献的燔祭或平安祭要与安息日所献的一样。他献完后就从东门出去,门也跟着关闭。

13“‘每天早晨,你们要献给耶和华一只毫无残疾的一岁羊羔为燔祭, 14同献的素祭是三公斤细面粉,调上一升油。献给耶和华的这种素祭是永久不变的律例。 15所以,每天早晨都要预备羊羔、素祭和油,作为日常献的燔祭。

16“‘主耶和华说,如果君王把一部分产业作为礼物赐给他儿子,这产业便归了他儿子,由他儿子的后代继承。 17如果君王把一部分产业作为礼物赐给他的仆人,他的仆人在得到自由之前可以拥有这产业,到他自由的那年46:17 “自由的那年”即“禧年”,参见利未记25:8‑17,这份产业仍要归还给君王,因为君王的产业只能由他的后代继承。 18君王不可驱逐百姓离开他们的土地,强夺他们的产业。他必须把自己拥有的产业赐给儿子,免得我的子民从自己的土地上被驱散。’”

19然后,那人领我从大门旁边的入口来到圣所北面的祭司圣屋,让我看圣屋西边的地方。 20他对我说:“这是祭司煮赎过祭牲、赎罪祭牲和烤素祭的地方。他们在这里烤煮,免得把圣肉带到外院,以致把圣洁传到百姓身上。”

21他又领我到外院,巡察外院的四个角落。我看见院中每个角落都有一个小庭院, 22每个庭院的四周都有围墙,长二十米,宽十五米,四角的庭院大小都一样。 23每个庭院的墙周围都有一排石屋,屋里有炉灶。 24他对我说:“这是圣殿的仆役替百姓煮祭物的地方。”