Ezekieli 45 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 45:1-25

Mgawanyo Wa Nchi

145:1 Mit 3:9-10; Hes 34:13; Eze 47:21-22; 48:8-9, 29“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000,45:1 Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25. upana wake dhiraa 20,00045:1 Dhiraa 20,000 ni sawa na kilomita 9. eneo hili lote litakuwa takatifu. 245:2 Eze 42:20Katika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. 345:3 Eze 48:10Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000.45:3 Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu. 445:4 Eze 40:46; 48:10-11Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu. 545:5 Eze 48:13; 40:17Eneo la urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000 litakuwa la Walawi wale wanaotumika hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi.

645:6 Eze 48:15-18“ ‘Utatoa mji kama mali yao wenye upana wa dhiraa 5,00045:6 Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25. na urefu wa dhiraa 25,000, karibu na sehemu takatifu, itakuwa mali ya nyumba yote ya Israeli.

745:7 Eze 48:21“ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na lile eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu upande huu na upande huu na eneo la mji. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi na upande wa mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila. 845:8 Hes 26:53; Eze 46:18Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.

945:9 Yer 22:3; Zek 7:9-10; 8:16; Za 12:5“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mwenyezi. 1045:10 Kum 25:15; Law 19:35; Mit 11:1; Mik 6:10-11; Amo 8:4-6Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa45:10 Efa ni kipimo cha ujazo cha kupimia vitu vikavu ambacho ni sawa na omeri 10; efa 1 ni sawa na kilo 22. na bathi.45:10 Bathi ni kipimo cha ujazo cha kupimia vitu vya humiminika ambacho ni sawa na 1/10 ya homeri; homeri 1 ni bathi 10 au efa 10. 1145:11 Isa 5:10Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili. 1245:12 Law 27:25; Hes 3:47; Kut 30:13Shekeli moja itakuwa gera ishirini.45:12 Gera 20 ni sawa na shekeli 1. Shekeli ishirini, jumlisha na shekeli ishirini na tano, jumlisha na shekeli kumi na tano zitakuwa mina moja.45:12 Mina 1 hapa ni sawa na shekeli 60; mina ya kawaida ilikuwa sawa na shekeli 50.

Sadaka Na Siku Takatifu

(Kutoka 12:1-20; Walawi 23:33-43)

13“ ‘Hili ndilo toleo maalum mtakalotoa: moja ya sita ya efa kutoka kila homeri ya ngano na moja ya sita ya efa kutoka kila homeri ya shayiri. 14Sehemu ya mafuta iliyoamriwa, yaliyopimwa kwa bathi, ni sehemu ya kumi ya bathi kutoka kila kori moja45:14 Kori 1 ni sawa na bathi 10 au homeri 1. (ambayo ina bathi kumi au homeri moja.) 1545:15 Law 1:4; 6:30; Rum 5:10; Efe 2:16; Kol 1:21; Tit 2:14Pia kondoo mmoja atachukuliwa kutoka kwenye kila kundi la kondoo mia mbili kutoka kwenye malisho yaliyonyeshewa vizuri ya Israeli. Hivi vitatumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya watu, asema Bwana Mwenyezi. 16Watu wote wa nchi wataungana pamoja na mkuu anayetawala Israeli ili kutoa hii sadaka maalum. 1745:17 Yn 6:51; Gal 3:13; Isa 66:23; 1Fal 8:62; 2Nya 31:3; Hes 10:10; Eze 46:4-12Huu utakuwa ndio wajibu wa mkuu anayetawala kutoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kwenye sikukuu, Mwezi Mwandamo na Sabato, kwenye sikukuu zote zilizoamriwa za nyumba ya Israeli. Atatoa sadaka za dhambi, sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.

1845:18 Kut 12:2; Law 22:20; Ebr 9:14; Law 16:33“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya huo mwezi utamchukua fahali mchanga asiye na dosari na kutakasa mahali patakatifu. 1945:19 Eze 43:17; Law 16:18-19; Eze 43:20Kuhani itampasa achukue sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi na kuipaka kwenye miimo ya Hekalu, kwenye pembe nne za juu za ukingo wa hayo madhabahu na juu ya miimo ya lango la ukumbi wa ndani. 2045:20 Law 4; 27Itakupasa kufanya vivyo hivyo katika siku ya saba ya mwezi huo kwa ajili ya mtu yeyote ambaye hutenda dhambi bila kukusudia au bila kujua, hivyo utafanya upatanisho kwa ajili ya Hekalu.

2145:21 Kut 12:11; Law 23:5-6; Hes 9:2-3“ ‘Katika mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne utaadhimisha Pasaka. Sikukuu itaendelea kwa siku saba, wakati huo wa hizo siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. 2245:22 Law 4:14; 1Pet 2:24Katika siku hiyo mkuu anayetawala atatoa fahali kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote wa nchi. 2345:23 Hes 28:15, 25; 22:40; Ay 42:8Kila siku wakati wa hizo siku saba za sikukuu atatoa mafahali saba na kondoo dume saba wasio na dosari kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana na beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 2445:24 Hes 28:12-13; Eze 46:5-7Pia atatoa sadaka ya nafaka efa moja kwa kila fahali na efa moja kwa kila kondoo dume, pamoja na hini moja45:24 Hini ni kipimo cha kupimia vitu vya humiminika chenye ujazo wa 1/6 ya bathi, na ni sawa na lita 4. ya mafuta kwa kila efa.

2545:25 Kum 16:13; Law 23:34-43; Hes 29:12-38“ ‘Wakati wa hizo siku saba za sikukuu, ambayo huanza katika mwezi wa saba kwenye siku ya kumi na tano, mkuu anayetawala atatoa mahitaji yale yale kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 45:1-25

划分圣地

1“‘当你们抽签把土地分给以色列各支派作产业的时候,要分出一块献给耶和华作圣地。圣地要长十二公里半,宽十公里,整块地都要圣洁。 2你们要在其中分出一块长宽各二百五十米的地建圣所。圣所的周围要有二十五米宽的空地。 3圣地当中要量一块长十二公里半、宽五公里的地,其中要有圣所,是至圣的地方。 4这块圣地应归那些在圣所供职并事奉耶和华的祭司,作为他们的居所和建圣所之用。 5另一块十二公里半长、五公里宽的土地给那些在圣殿工作的利未人建城居住,作他们的产业45:5 “作他们的产业”或译作“有二十间房作他们的产业”。

6“‘在圣地旁边要分出一块十二公里半长、两公里半宽的地建城,归给所有以色列人。

7“‘在圣地和城的东西两边是给君王的土地,西边延伸至西边的边境,东边延伸至东边的边境,从西到东长度与各支派分得的土地一样。 8这地方要作君王在以色列的产业。我的君王必不再欺压我的子民,而是按支派把地分给他们。

9“‘主耶和华说,你们这些以色列的君王啊,够了!你们应当放弃暴行和抢掠,按公平和正义行事,不要再向我的子民横征暴敛了!这是主耶和华说的。 10你们要用公道的天平、伊法和罢特。 11伊法和罢特容量要相同,量固体的伊法是十分之一贺梅珥45:11 一贺梅珥相当于一百五十公斤或二百升。,量液体的罢特也是十分之一贺梅珥,贺梅珥是标准的容量单位。 12舍客勒45:12 一舍客勒约合十一克。是标准的重量单位,一舍客勒是二十季拉。六十舍客勒等于一弥那。

13“‘以下是你们应当献的供物,每一贺梅珥小麦要献上六分之一伊法,每一贺梅珥大麦也要献上六分之一伊法。 14献橄榄油要按规定以罢特计量,每一柯珥的油要献十分之一罢特,一柯珥等于十罢特或一贺梅珥,因为一贺梅珥等于十罢特。 15以色列肥美的草场上,每二百只羊便要献上一只。这些供物用来作素祭、燔祭和平安祭,为以色列人赎罪。这是主耶和华说的。 16所有的以色列人都要这样拿供物来献给君王。 17君王要在节期、朔日45:17 “朔日”即每月初一。、安息日等以色列人一切的节期献上燔祭、素祭和奠祭。他要预备赎罪祭、素祭、燔祭和平安祭的祭物,为以色列人赎罪。

18“‘主耶和华说,一月初一,你要献一只毫无残疾的公牛犊,洁净圣所。 19祭司要取些赎罪祭牲的血抹在圣殿的门柱、祭台的四角和内院门口的柱子上。 20到了一月七日,要同样为一切在无意和无知中犯罪的人赎罪,使圣殿洁净。

21“‘一月十四日开始,你们要守逾越节七天,节期间要吃无酵饼。 22在逾越节当天,君王要预备一头公牛为自己和全体百姓作赎罪祭。 23在七天的节期间,他要每天预备毫无残疾的公牛七头、公绵羊七只作燔祭献给耶和华,公山羊一只作赎罪祭。 24他要预备细面粉和油作素祭与牛羊一同献上。每头公牛或公绵羊要同献十公斤细面粉和四升油。 25在七月十五日开始一连七天的住棚节期间,君王也要供应同样的赎罪祭、燔祭、素祭和油。’