Ezekieli 44 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 44:1-31

Mkuu, Walawi, Makuhani

144:1 Eze 43:1Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali Patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. 244:2 Eze 43:4-5Bwana akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili. 344:3 Zek 6:12; Kut 24:9-11; Eze 46:2-8Yeye aliye mkuu peke yake ndiye anayeweza kukaa penye njia ya hilo lango na kula chakula mbele za Bwana. Itampasa aingie kwa njia hiyo ya lango la ukumbini na kutokea njia iyo hiyo.”

444:4 Isa 6:4; Ufu 15:8; Eze 1:28; Dan 8:17; Eze 40:35; 10:4Kisha yule mtu akanileta kwa njia ya lango la kaskazini mpaka mbele ya Hekalu. Nikatazama nami nikauona utukufu wa Bwana ukilijaza Hekalu la Bwana, nami nikaanguka kifudifudi.

544:5 Eze 40:4; 43:10-11; 42:9Bwana akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa uangalifu, usikilize kwa bidii na uzingatie kila kitu ninachokuambia kuhusu masharti yote yanayohusu Hekalu la Bwana. Uwe mwangalifu kuhusu wale wanaoruhusiwa hekaluni na wale wasioruhusiwa kuingia mahali patakatifu. 644:6 Eze 3:19Iambie nyumba ya kuasi ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Matendo yenu ya machukizo yatosha, ee nyumba ya Israeli! 744:7 Law 26:4; Mwa 17:14; Kut 12:48; Mdo 21:28; Law 22:25Zaidi ya matendo yenu yote ya machukizo, mmewaleta wageni wasiotahiriwa mioyo na miili katika patakatifu pangu, mkilinajisi Hekalu langu, huku mkinitolea chakula, mafuta ya wanyama na damu, nanyi mmevunja Agano langu. 844:8 Law 22:2; Hes 18:7; 2Tim 4:1Badala ya kutimiza wajibu wenu kuhusiana na vitu vyangu vitakatifu, mmeweka watu wengine kuwa viongozi katika patakatifu pangu. 944:9 Yoe 3:17; Zek 14:21Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.

1044:10 Neh 9:34; 2Fal 23:8; Za 95:10; Hes 18:23“ ‘Walawi walioniacha wakati Waisraeli walipopotoka wakatoka kwangu na kutangatanga kwa kufuata sanamu zao, watachukua adhabu ya dhambi zao. 1144:11 2Nya 29:34; Hes 16:9; 1Nya 26:12-19; Hes 3:5-37Wanaweza wakatumika katika mahali patakatifu pangu, wakiwa na uangalizi wa malango ya Hekalu, nao watachinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa ajili ya watu na kusimama mbele ya watu ili kuwahudumia. 1244:12 2Fal 16:10-16; Yer 14:10; Za 106:26; Yer 18:15Lakini kwa sababu waliwatumikia watu mbele ya sanamu zao na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema Bwana Mwenyezi. 1344:13 Eze 16:6; Hes 18:3; Hos 5:1Hawaruhusiwi kukaribia ili kunitumikia kama makuhani wala kukaribia chochote changu kilicho kitakatifu au sadaka iliyo takatifu kupita zote, bali watachukua aibu ya matendo yao ya kuchukiza. 1444:14 1Sam 2:36; 2Fal 23:9; 1Nya 23:28-32Lakini nitawaweka katika uangalizi wa Hekalu na kazi zote zile zinazotakiwa kufanyika ndani yake.

1544:15 Yer 33:18; Zek 3:7; Kum 10:8; 2Sam 8:17; Eze 7:2; Kum 29:13; Eze 40:46“ ‘Lakini makuhani, ambao ni Walawi na wazao wa Sadoki, ambao walitimiza wajibu wao kwa uaminifu katika patakatifu pangu wakati Waisraeli walipopotoka, watakaribia ili kutumika mbele zangu. Itawapasa wasimame mbele zangu ili kutoa dhabihu za mafuta ya wanyama na damu, asema Bwana Mwenyezi. 1644:16 Eze 41:22; 1Sam 2:35; Mal 2:7; Law 3:16-17; Hes 8:15; Law 17:5-6Wao peke yao ndio wenye ruhusa ya kuingia mahali patakatifu pangu. Wao peke yao ndio watakaokaribia meza yangu ili kuhudumu mbele zangu na kufanya utumishi wangu.

1744:17 Kut 39:27-28; Ufu 19:8“ ‘Watakapoingia kwenye malango ya ukumbi wa ndani, watavaa nguo za kitani safi, hawaruhusiwi kamwe kuvaa mavazi ya sufu wakati wanapokuwa wakihudumu kwenye malango ya ukumbi wa ndani wala ndani ya Hekalu. 1844:18 Kut 28:39; Isa 3:20; Law 16:4; Kut 28:42Watavaa vilemba vya kitani safi vichwani mwao na nguo za ndani za kitani safi viunoni mwao. Hawatavaa chochote kitakachowafanya kutoa jasho. 1944:19 Law 6:27; Eze 46:20; Kut 39:27-29; Law 6:10-11Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili kwamba wasije wakaambukiza watu utakatifu kwa njia ya mavazi yao.

2044:20 Law 21:5; Hes 6:5; Isa 28:7“ ‘Hawatanyoa nywele za vichwa vyao wala kuziacha ziwe ndefu, bali watazipunguza. 2144:21 Law 10:9Kuhani yeyote asinywe mvinyo aingiapo katika ukumbi wa ndani. 2244:22 Law 21:7Wasioe wanawake wajane wala walioachika, inawapasa kuoa wanawake bikira wenye heshima wa Israeli au wajane wa makuhani. 2344:23 Eze 22:26; Hag 2:11-13; Mal 2:7; Mwa 7:2; Law 13:50; Yer 15:19Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonyesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi.

2444:24 1Tim 4:5; 1Nya 23:4; 2Nya 19:8; Kum 17:8-9; 19:17“ ‘Katika magombano yoyote, makuhani watatumika kama mahakimu na kuamua hilo jambo kufuatana na sheria zangu. Watazishika sheria zangu na maagizo yangu katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa, nao watatakasa Sabato zangu.

2544:25 Law 21:1-4“ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti, lakini, kama mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hajaolewa, basi aweza kujitia unajisi kwa hao. 2644:26 Law 21:1-4; Hes 6:10Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba. 2744:27 Hes 3:28; 6:11; Law 4:28Siku atakapoingia katika ukumbi wa ndani wa mahali patakatifu ili kuhudumu, atatoa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe, asema Bwana Mwenyezi.

2844:28 Kum 10:9; Yos 13:33; Hes 18:20; Kum 18:1-2“ ‘Mimi nitakuwa ndio urithi pekee walio nao makuhani katika Israeli. Msiwape wao milki, mimi nitakuwa milki yao. 2944:29 Law 27:21; Hes 18:9, 14; Yos 13:14; Law 6:16Wao watakula sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia na kila kitu kitakachotolewa kwa Bwana katika Israeli kitakuwa chao. 3044:30 Hes 18:12-13; 2Nya 31:5; Hes 15:18-21; Neh 10:35-37; 2Nya 30:10Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili kwamba baraka ipate kuwa katika nyumba zenu. 3144:31 Kut 22:31; Law 22:8; 11:39-40Makuhani hawaruhusiwi kula chochote, ikiwa ni ndege au mnyama, aliyekutwa akiwa amekufa au aliyeraruliwa na wanyama pori.