Ezekieli 43 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 43:1-27

Utukufu Warudi Hekaluni

143:1 Eze 10:19; 1Nya 9:18; Eze 8:16; 42:15Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 243:2 Za 18:4; Ufu 1:15; 21:11; Isa 6:3nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake. 343:3 Eze 1:4; 3:21; Yer 1:10Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 443:4 Eze 1:28; 10:19; 44:2Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. 543:5 Eze 3:12; 11:24; Kut 16:7; Isa 6:4Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu.

643:6 Eze 40:3Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu. 743:7 Eze 20:29-39; Law 26:30; Kut 25:8; Yer 16:18; 16:18; 3:17; Eze 37:23Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu. 843:8 2Fal 16:14Walipoweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu na miimo yao ya milango karibu na miimo yangu, pakiwa na ukuta tu kati yangu na wao, walilinajisi Jina langu takatifu kwa matendo yao ya machukizo. Kwa sababu hiyo niliwaangamiza kwa hasira yangu. 943:9 Eze 37:26-28Basi sasa na waweke mbali nami ukahaba wao na sanamu za wafalme wao zisizo na uhai, nami nitakaa miongoni mwao milele.

1043:10 Eze 16:61; 40:4“Mwanadamu, elezea hilo Hekalu kwa watu wa Israeli, ili wapate kuona aibu kwa ajili ya dhambi zao. Wao na wapime hicho kielelezo. 1143:11 Eze 44:5-6; Mt 28:20Wakishaona aibu kwa ajili ya yale yote waliyotenda, wafahamishe kielelezo cha hilo Hekalu, yaani mpangilio wake, maingilio yake ya kutoka na kuingia, kielelezo chake chote, na masharti yake yote na sheria zake zote. Yaandike haya mbele yao ili wapate kuwa waaminifu kwa hicho kielelezo chake na kufuata masharti yake yote.

1243:12 Eze 40:2; 42:20; Ufu 21:27; Eze 17:22“Hii ndiyo sheria ya Hekalu: Eneo lote linalozunguka Hekalu juu ya mlima litakuwa takatifu kuliko yote. Hii ndiyo sheria ya Hekalu.

Madhabahu

1343:13 Kut 20:24; 2Nya 4:1“Hivi ndivyo vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ndefu, yaani, dhiraa moja na nyanda nne:43:13 Dhiraa 1 na nyanda 4 ni sawa na sentimita 53. Tako lake liwe na kina cha hiyo dhiraa moja na upana wa hiyo dhiraa moja, ikiwa na ukingo wa shibiri moja43:13 Shibiri 1 ni sawa na sentimita 22.5. kuizunguka pembeni. Hiki kitakuwa ndicho kimo cha madhabahu: 14Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja. 1543:15 Kut 27:2; Isa 29:2Pale pawashwapo moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale pawashwapo moto. 1643:16 Ufu 21:16Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili43:16 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. na upana wa dhiraa kumi na mbili. 1743:17 Kut 20:26; Eze 45:19; Kut 27:1Pia sehemu ya juu ni mraba, urefu wake dhiraa kumi na nne na upana wa dhiraa kumi na nne, ikiwa na ukingo wa nusu dhiraa na mfereji kuizunguka madhabahu. Ngazi za kupandia madhabahuni zitaelekea upande wa mashariki.”

1843:18 Kut 40:29; Ebr 9:21-22Kisha akaniambia, “Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Haya ndiyo yatakayokuwa masharti ya kutoa dhabihu za kuteketezwa na kunyunyiza damu juu ya madhabahu itakapokuwa imejengwa. 1943:19 Law 4:3; Eze 45:18-19; 2Nya 8:17; Ezr 7:2; Hes 16:40; Eze 40:46Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema Bwana Mwenyezi. 2043:20 Law 16:19; 4:7Itakupasa kuchukua baadhi ya hiyo damu ya mnyama huyo na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu na kufanya upatanisho kwa ajili yake. 2143:21 Kut 29:14; Ebr 13:11Itakupasa kumchukua huyo fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kumteketeza mahali palipoagizwa katika eneo la Hekalu nje ya mahali Patakatifu.

22“Siku ya pili yake utamtoa beberu asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nayo madhabahu itatakaswa kama ilivyotakaswa kwa yule fahali. 2343:23 Kut 29:1; Law 22:20Utakapokuwa umemaliza kazi ya kuitakasa, utamtoa fahali mchanga pamoja na kondoo dume toka kwenye kundi, wote wawe hawana dosari. 2443:24 Mk 9:49-50Utawatoa mbele za Bwana, nao makuhani watanyunyizia chumvi juu yao na kuwatoa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.

25“Kwa siku saba itakupasa kutoa beberu kila siku kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pia itakupasa kutoa fahali mchanga na kondoo dume kutoka zizini, wote wawe hawana dosari. 26Kwa siku saba itawapasa kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuitakasa na hivyo ndivyo watakavyoiweka wakfu. 2743:27 Kut 32:6; Law 17:5; Ay 42:8; Isa 60:7Mwishoni mwa hizi siku saba, kuanzia siku ya nane na kuendelea, itawapasa makuhani kutoa sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu. Kisha nitawakubali ninyi, asema Bwana Mwenyezi.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

以西結書 43:1-27

耶和華的榮光充滿聖殿

1後來,那人帶我來到東門, 2只見以色列上帝的榮光從東方而來,祂的聲音如澎湃的洪濤,大地也因祂的榮耀而發出光芒。 3這異象如同我從前在祂毀滅耶路撒冷時看見的異象,也像我在迦巴魯河邊看見的異象,我便俯伏在地。 4耶和華的榮光從東門進入聖殿。 5上帝的靈把我舉起,帶我進入內院,只見耶和華的榮光充滿聖殿。

6那人仍然站在我身旁,我聽見有一位從殿中對我說: 7「人子啊,這裡是我的寶座,是我踏腳的地方,我要在這裡永遠住在以色列人當中。以色列的君民必不再因不忠貞,或在邱壇為他們死去的君王立碑而玷污我的聖名。 8他們不再在我聖殿旁邊建廟宇,使它們的門檻和門柱緊挨著我的門檻和門柱,以致我與它們只有一牆之隔。他們行可憎的事,玷污了我的聖名,所以我發怒消滅他們。 9現在,他們要從我面前遠遠地除去他們的不忠貞和先王的碑,我就永遠住在他們當中。

10「人子啊,你要向以色列人描述所看見的聖殿,讓他們思考聖殿的設計,使他們為自己的罪惡而羞愧。 11他們若為自己的行為感到羞愧,你就把殿的構造、出入口等整個設計,以及殿中的一切律例和法則告訴他們,並且當著他們的面寫下來,讓他們忠於設計,遵行殿的一切律例。 12殿所在的山頂周圍都是至聖之地,這是有關殿的法則。

13「以下是祭壇的尺寸,底槽深五十釐米,寬五十釐米,周圍環繞著一條二十五釐米高的邊框。 14從底座到下層臺座高一米,邊寬五十釐米,下層臺座到上一層高二米,邊寬五十釐米。 15最高一層是祭台,高二米,祭台上的四角向上突起。 16祭台是方形的,長寬各六米, 17下面的臺座也是方形的,長寬各七米,周圍環繞著一條二十五釐米高的邊框。底座四圍的邊寬五十釐米,上祭台的石階在東面。」

18祂對我說:「人子啊,主耶和華這樣說,『祭壇建成後,要按以下的規矩在上面獻燔祭和灑血。 19你要將一頭公牛犢作為贖罪祭給撒督後裔中的利未祭司,他們可以前來事奉我。這是主耶和華說的。 20取些公牛犢的血抹在祭壇的四角、臺座的四角和四邊,使祭壇潔淨,為祭壇贖罪, 21並把贖罪用的公牛犢拿到聖所外指定的聖殿區焚燒。 22第二天,你要獻上一頭毫無殘疾的公山羊作贖罪祭,就像獻公牛一樣,使祭壇潔淨。 23祭壇潔淨後,你要取來一頭毫無殘疾的公牛犢和一隻毫無殘疾的公綿羊, 24祭司要把鹽撒在祭牲上,作為燔祭獻在耶和華面前。 25一連七天,每天都要獻上一隻公山羊、一頭公牛犢和一隻公綿羊作贖罪祭,都不可有殘疾。 26在這七天之內,他們要為祭壇贖罪,使壇潔淨,成為聖壇。 27七天結束後,從第八天開始,祭司要在祭壇上獻你們的燔祭和平安祭,我必悅納你們。這是主耶和華說的。』」