Ezekieli 39 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 39:1-29

Majeshi Ya Gogu Yataangamizwa

139:1 Eze 27:13; 38:2; Ufu 20:6“Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. 239:2 Eze 32:30; 38:4, 15Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukuburuta. Nitakuleta kutoka kaskazini ya mbali na kukupeleka wewe dhidi ya milima ya Israeli. 339:3 Amo 2:15; Za 76:3Kisha nitaupiga upinde wako kutoka mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale ianguke kutoka mkono wako wa kuume. 439:4 Yer 25:33; Eze 29:5; Mwa 40:19; Isa 34:2-8Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama wa mwituni. 539:5 Eze 32:4Utaanguka katika uwanja, kwa kuwa nimenena, asema Bwana Mwenyezi. 639:6 Ufu 20:9; Yer 25:22; Eze 30:8; Kut 6:7Nitatuma moto juu ya Magogu na kwa wale wanaoishi kwa salama huko pwani, nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana.

739:7 Kut 20:7; Eze 13:19; Isa 12:6; 54:5; Eze 20:9; 36:23; Isa 49:26“ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi Bwana ndimi Aliye Mtakatifu wa Israeli. 839:8 Eze 7:3-8; 38:17Hili jambo linakuja! Hakika litatokea, asema Bwana Mwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake.

939:9 Za 46:9; 76:3“ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni. 1039:10 Isa 33:1; Hab 2:8; Isa 14:2; Kut 3:22Hawatahitaji kukusanya kuni kutoka mashambani wala kukata kuni kutoka kwenye misitu, kwa sababu watatumia silaha kuwa kuni. Nao watawateka mateka wale waliowateka na kuchukua nyara mali za wale waliochukua mali zao nyara, asema Bwana Mwenyezi.

1139:11 Eze 38:2; Isa 34:3“ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.39:11 Hamon-Gogu maana yake Makundi ya wajeuri wa Gogu.

1239:12 Kum 21:23“ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi. 1339:13 Eze 28:22; Za 126:2Watu wote wa nchi watawazika, nayo siku nitakayotukuzwa itakuwa siku ya kumbukumbu kwa ajili yao, asema Bwana Mwenyezi.

1439:14 Eze 39:12“ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao. 15Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu. 1639:16 Eze 39:12(Pia mji uitwao Hamona39:16 Hamona maana yake Kundi (la wajeuri). utakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’

1739:17 Isa 18:6; Ay 15:23; Ufu 19:17; Eze 32:4“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu. 1839:18 Za 22:12; Yer 51:40Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za kondoo dume na kondoo wake, mbuzi na mafahali, wote walionona kutoka Bashani. 1939:19 Law 3:9Katika dhabihu ninayoandaa kwa ajili yenu, mtakula mafuta mpaka mkinai na kunywa damu mpaka mlewe. 2039:20 Yer 12:9; Ufu 19:17-18; Eze 38:4; Isa 56:9Kwenye meza yangu watajishibisha kwa farasi na wapanda farasi, watu mashujaa na askari wa kila aina,’ asema Bwana Mwenyezi.

2139:21 Kut 9:16; Isa 37:20; Eze 38:16“Nitauonyesha utukufu wangu miongoni mwa mataifa, nayo mataifa yote wataiona adhabu nitakayotoa na mkono wangu nitakaouweka juu yao. 22Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wao. 2339:23 Isa 1:15; Kum 31:17; Yer 22:8-9; Isa 59:2; Yer 44:23Na mataifa watajua kuwa nyumba ya Israeli walikwenda utumwani kwa ajili ya dhambi yao, kwa sababu hawakuwa waaminifu kwangu. Hivyo niliwaficha uso wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga. 2439:24 2Fal 17:23; Dan 9:7; Eze 36:19; 16:53; Yer 4:18Niliwatendea sawasawa na uchafu wao na makosa yao, nami nikawaficha uso wangu.

2539:25 Eze 34:13; Yer 30:18; Isa 27:12-13; Eze 16:53; Yer 33:7“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu. 2639:26 1Fal 4:25; Yer 32:37; Isa 17:2; Mik 4:4; Dan 9:16; Eze 38:8Wataisahau aibu yao na jinsi walivyoonyesha kutokuwa waaminifu kwangu mimi wakati waliishi salama katika nchi yao, bila kuwa na mtu yeyote wa kuwatia hofu. 2739:27 Eze 37:21; 38:16; 36:23Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka nchi za adui zao, mimi nitajionyesha kuwa mtakatifu kwa kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi. 2839:28 Za 147:2; Eze 36:23, 36Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma. 2939:29 Isa 11:2; Mdo 2:27; Hos 2:20; Yoe 2:28; Kum 31:17; Eze 37:9; 16:42Sitawaficha tena uso wangu, kwa maana nitamimina Roho wangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana Mwenyezi.”