Ezekieli 34 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 34:1-31

Wachungaji Na Kondoo

1Neno la Bwana likanijia kusema: 234:2 Mik 3:11; Yud 12; Yer 3:15; Isa 40:11; Za 78:70-72; Yn 21:15-17“Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo? 334:3 Amo 6:4; Zek 11:5; Eze 22:27; Isa 56:11Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi. 434:4 Law 25:43; Mik 3:3; 2Tim 2:24; Mdo 9:36; Isa 3:7; Zek 11:15-17Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili. 534:5 Hes 27:17; Isa 56:9; Mdo 20:29Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote. 634:6 Yer 50:6; Law 26:33; Za 95:10; Yer 10:21; 2Nya 18:16; Za 142:4; Hos 7:13; Mt 9:36; 18:12-13Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.

7“ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana: 834:8 2Nya 18:16; 1Pet 2:25; Yer 50:6; Za 95:10; Yer 10:21; Hos 7:13; Za 42:4; Mt 18:12-13Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu, 934:9 Amu 2:14; Isa 59:6; Yud 12kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno la Bwana: 1034:10 Yer 21:13; Za 72:14; Yer 23:2; Zek 10:3; 1Sam 2:29-30Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.

1134:11 Za 119:176“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo wangu na kuwatafuta. 1234:12 Zek 10:3; Lk 19:10; Eze 30:3; 32:7; Mdo 2:19-21; Isa 40:11Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene. 1334:13 Mwa 48:21; Yer 23:3, 8; 50:19; Kum 30:4; Eze 11:17Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi. 1434:14 Eze 20:40; 37:22; Za 23:2; 37:3; Isa 65:10; Amo 9:14; Eze 36:29-30Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli. 1534:15 Sef 3:13; Mik 5:4; Za 23:1-2; Yer 33:12Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo zangu na kuwafanya wapumzike, asema Bwana Mwenyezi. 1634:16 Isa 61:1-2; Mik 4:6; Sef 3:19; Yer 31:8; Lk 5:32; Mt 2:17; 15:24Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.

1734:17 Mt 25:32-33; Eze 20:37“ ‘Kwa habari yenu, enyi kundi langu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo dume na mbuzi. 1834:18 Mwa 30:15; Eze 32:2Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu? 19Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu?

2034:20 Eze 34:17“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda. 2134:21 Kum 33:17Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza, 2234:22 Za 72:12-14; Yer 23:2-3; Eze 20:37-38nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo. 2334:23 Ebr 13:20; Isa 40:11; Eze 37:24; Isa 31:4; Mik 5:4Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao. 2434:24 Eze 36:28; Yer 33:14; 30:4; Yn 10:16; Kut 29:45; Za 89:49; Isa 53:4; Ufu 7:17Mimi Bwana nitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. Mimi Bwana nimenena.

2534:25 Law 26:6; 25:18; Hos 2:18; Yer 23:6; Isa 11:6-9; Hes 25:12; Eze 16:62“ ‘Nitafanya nao Agano la amani na kuwaondoa wanyama wa mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama. 2634:26 Mwa 12:2; Za 68:9; Yoe 2:23; Kum 28:12; 11:13-15Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka. 2734:27 Yer 2:20; Law 26:13; Yer 30:8; Eze 20:42; Yer 25:14; Za 72:16; Ay 14:9Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa. 2834:28 Hos 11:11; Zek 14:11; Amo 9:15; Yer 30:10; 32:37; Eze 28:26; 39:26Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori hawatawala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna yeyote atakayewatia hofu. 2934:29 Isa 4:2; Yoe 2:19; Eze 36:15, 29; Za 137:3Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, hawatapatwa na njaa katika nchi tena wala hawatadharauliwa na mataifa. 3034:30 Eze 14:11; 37:27; 2Tim 1:12Ndipo watakapojua kuwa Mimi, Bwana, Mungu wao, niko pamoja nao, na kwamba wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana Mwenyezi. 3134:31 Za 100:3; Yer 23:1; Za 28:9Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 34:1-31

以色列的牧人

1耶和华对我说: 2“人子啊,你要这样说预言斥责以色列的牧人,‘主耶和华说:以色列的牧人啊,你们有祸了!你们只顾喂养自己,牧人岂不应该喂养羊群吗? 3但你们只顾吃羊的脂肪,穿羊毛衣,宰杀肥羊,却不喂养羊群。 4你们没有养壮瘦弱的,没有医治生病的,没有包扎受伤的,没有领回走散的,没有寻找迷失的。你们反用暴力辖制他们。 5因为没有牧人,羊群便流离失散,成了所有野兽的食物。 6我的羊在群山和高岗上游荡,分散在各地,没有人寻找他们。

7“‘所以,你们这些牧人啊,要听耶和华的话。 8主耶和华说:我凭我的永恒起誓,我的羊因为没有牧人而成了猎物,沦为所有野兽的食物。我的牧人不去寻找我的羊,他们只喂养自己,不喂养我的羊, 9所以你们这些牧人啊,要听耶和华的话。 10主耶和华说,我要攻击这些牧人,从他们手中要回我的羊,不再让他们喂养羊群,使他们无法再喂养自己。我要从他们口中救回我的羊,不再让羊成为他们的食物。

11“‘主耶和华说:看啊,我要亲自寻找我的羊,找到他们。 12牧人怎样寻找他四散的羊,我也照样寻找我的羊,他们在密云幽暗的日子失散到各地,我要把他们从那里救回来。 13我要把他们从列邦领出来,从列国招聚他们,带他们回到自己的故土,我要在以色列的山岭上、溪水旁和境内可居之地牧养他们。 14我要在佳美的草场上牧养他们,以色列的山岭必成为他们的草场。他们要在佳美的草场上安卧,在以色列山岭的肥美草场上吃草。 15我要亲自喂养我的羊,让他们得到安歇。这是主耶和华说的。 16我要寻找迷失的,领回失散的,包扎受伤的,医治患病的,但我要消灭肥壮的。我要秉公牧养他们。

17“‘我的羊群啊!至于你们,主耶和华这样说:我要在你们中间施行审判,在公绵羊和公山羊之间进行审判。 18你们肥壮的羊在茂盛的草场上吃还不够吗?你们非要用蹄子践踏吃剩的草吗?你们喝清水还不够吗?你们非要用蹄子搅浑剩下的水吗? 19我其余的羊只得吃你们践踏的草,喝你们搅浑的水。

20“‘因此,主耶和华对他们说:看啊,我要亲自在肥羊和瘦羊之间施行审判。 21你们肥羊用胁和肩拱,用角抵瘦弱的,使他们四散。 22因此我要拯救我的羊,使他们不再成为猎物,我要在羊与羊之间施行审判。 23我要立我的仆人大卫做他们的牧人,他将牧养他们,做他们的牧人。 24我耶和华要做他们的上帝,我的仆人大卫要在他们当中做王,这是耶和华说的。

25“‘我要跟他们立平安的约,除去地上的恶兽,让他们在旷野安居,在丛林安睡。 26我要赐福他们,也要赐福我圣山的周围,我要按季节降雨给他们,使恩福如雨降下。 27田间的树木必结果子,土地必长出庄稼,他们要在故乡安居。我要折断他们所负的轭,从奴役他们的人手中把他们拯救出来,那时他们便知道我是耶和华。 28他们必不再成为列国的猎物,也不会被地上的野兽吞吃。他们必安居乐业,不再受人惊吓。 29我要把沃土赐给他们,使他们不再被境内的饥荒吞噬,也不再受各国的侮辱。 30这样,以色列人就知道我耶和华——他们的上帝与他们同在,他们以色列人是我的子民,这是主耶和华说的。 31你们是我草场上的羊,你们是我的子民,我是你们的上帝。这是主耶和华说的。’”