Ezekieli 28 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 28:1-26

Unabii Dhidi Ya Mfalme Wa Tiro

1Neno la Bwana likanijia kusema: 228:2 Isa 14:13; Mwa 3:4-5; 2The 2:4; Kum 8:14; Mit 16:18; Sef 2:15; Za 9:20“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna

na umesema, “Mimi ni mungu;

nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu

katika moyo wa bahari.”

Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,

ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.

328:3 Dan 1:20; 2:20-23, 28; Zek 9:2; Eze 14:14Je, wewe una hekima kuliko Danieli?

Je, hakuna siri iliyofichika kwako?

428:4 Zek 9:3; Isa 10:13Kwa hekima yako na ufahamu wako,

umejipatia utajiri,

nawe umejikusanyia dhahabu

na fedha katika hazina zako.

528:5 Ay 31:25; Hos 13:6; Kum 8:12-14; Isa 23:8; Yer 9:23; 9:23; Eze 27:33Kwa werevu wako mwingi katika biashara,

umeongeza utajiri wako

na kwa sababu ya utajiri wako

moyo wako umekuwa na kiburi.

6“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,

mwenye hekima kama mungu,

728:7 Eze 32:12; 30:11; 31:12; Yer 9:23; Eze 7:24mimi nitawaleta wageni dhidi yako,

taifa katili kuliko yote;

watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,

na kuchafua fahari yako inayongʼaa.

828:8 Za 55:23; Eze 32:30; 27:27; 26:12; Ufu 18:7Watakushusha chini shimoni,

nawe utakufa kifo cha kikatili

katika moyo wa bahari.

928:9 Isa 31:3; Eze 16:49Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,”

mbele ya wale wanaokuua?

Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu,

mikononi mwa hao wanaokuua.

1028:10 1Sam 14:6; Yer 9:26; Eze 32:18-19Utakufa kifo cha wasiotahiriwa

kwa mkono wa wageni.

Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

11Neno la Bwana likanijia kusema: 1228:12 Eze 19:1; 27:2-4“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,

ukiwa umejaa hekima

na mkamilifu katika uzuri.

1328:13 Mwa 2:8; Eze 31:8-9; 27:16; Ufu 17:4; Isa 14:11; Ufu 21:20Ulikuwa ndani ya Edeni,

bustani ya Mungu;

kila kito cha thamani kilikupamba:

akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,

krisolitho, shohamu na yaspi,

yakuti samawi, almasi na zabarajadi.

Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake

kulifanywa kwa dhahabu;

siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari.

1428:14 Kut 30:26; 40:9; 25:17-20Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,

kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.

Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;

ulitembea katikati ya vito vya moto.

15Ulikuwa mnyofu katika njia zako

tangu siku ile ya kuumbwa kwako,

hadi uovu ulipoonekana ndani yako.

1628:16 Mwa 6:11; Hab 2:17; Mwa 3:24Kutokana na biashara yako iliyoenea,

ulijazwa na dhuluma,

nawe ukatenda dhambi.

Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu,

nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi,

kutoka katikati ya vito vya moto.

1728:17 Isa 10:12; Eze 16:49; 31:10; 19:12Moyo wako ukawa na kiburi

kwa ajili ya uzuri wako,

nawe ukaiharibu hekima yako

kwa sababu ya fahari yako.

Kwa hiyo nikakutupa chini;

nimekufanya kioja mbele ya wafalme.

1828:18 Oba 1:18; Mal 4:3; Zek 9:2-4Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,

umenajisi mahali pako patakatifu.

Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,

nao ukakuteketeza,

nami nikakufanya majivu juu ya nchi,

machoni pa wote waliokuwa wakitazama.

1928:19 Yer 51:64; Eze 26:21; Law 26:21Mataifa yote yaliyokujua

yanakustajabia;

umefikia mwisho wa kutisha

na hutakuwepo tena milele.’ ”

Unabii Dhidi Ya Sidoni

20Neno la Bwana likanijia kusema: 2128:21 Eze 6:2; 13:17; Yer 25:2; Mwa 10:15“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 2228:22 Kut 14:4; Za 9:16; Eze 30:19; 39:13; Law 10:3nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,

nami nitapata utukufu ndani yako.

Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana,

nitakapotekeleza hukumu zangu

na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.

2328:23 Eze 5:17; 38:22Nitapeleka tauni ndani yake

na kufanya damu itiririke katika barabara zake.

Waliochinjwa wataanguka ndani yake,

kwa upanga dhidi yake kila upande.

Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.

2428:24 Hes 33:55; Yos 23:13; Isa 5:6; Eze 2:6“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.

2528:25 Za 106:47; Yer 32:37; Isa 11:12; Eze 20:41; Yer 12:15; 12:15; 23:8; Eze 11:17“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo. 2628:26 Law 25:18; Yer 23:6; Hos 2:15; Amo 9:14-15; 1Fal 4:25; Yer 17:25; Kum 20:6; Eze 38:8; 39:26-27; Isa 65:21Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.’ ”