Ezekieli 27 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 27:1-36

Maombolezo Kwa Ajili Ya Tiro

1Neno la Bwana likanijia kusema: 227:2 Eze 19:1; 26:17; 28:12; 32:2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. 327:3 Hos 9:13; Isa 23:9; Eze 28:2; Za 83:16Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,

“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

427:4 Eze 28:12Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,

wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

527:5 Kum 3:9; Isa 2:13Walizifanya mbao zako zote

kwa misunobari itokayo Seniri;27:5 Yaani Hermoni.

walichukua mierezi kutoka Lebanoni

kukutengenezea mlingoti.

627:6 Za 29:9; Zek 11:2; Mwa 10:4; Isa 23:12; Yer 22:20; Hes 21:33Walichukua mialoni toka Bashani

wakakutengenezea makasia yako;

kwa miti ya msanduku

kutoka pwani ya Kitimu

wakatengeneza sitaha27:6 Yaani sakafu ya merikebu au mashua. yako

na kuipamba kwa pembe za ndovu.

727:7 Kut 25:4; Yer 10:9; Isa 19:9; Mwa 10:4; Kut 26:36Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,

nacho kilikuwa bendera yako;

chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau

kutoka visiwa vya Elisha.

827:8 Mwa 10:18; 1Fal 9:23-27Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;

watu wako wenye ustadi, ee Tiro,

walikuwa ndio mabaharia wako.

927:9 Yos 13:5; 1Fal 5:18; Za 104:26Wazee wa Gebali27:9 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). pamoja na mafundi stadi

walikuwa mafundi wako melini.

Meli zote za baharini na mabaharia wao

walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.

1027:10 Dan 8:20; Mwa 10:6; Nah 3:9; Yer 46:9; Eze 38:5; 2Nya 36:20; Isa 66:19; Wim 4:4“ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu

walikuwa askari katika jeshi lako.

Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako,

wakileta fahari yako.

1127:11 Eze 27:27Watu wa Arvadi na wa Heleki

walikuwa juu ya kuta zako pande zote;

watu wa Gamadi

walikuwa kwenye minara yako.

Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako;

wakaukamilisha uzuri wako.

1227:12 Mwa 10:4; 2Nya 20:36“ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako.

1327:13 Isa 66:19; Ufu 18:13; Yoe 3:6; Mwa 10:2; Eze 32:26; 38:2“ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.

1427:14 Mwa 10:3; Eze 38:6“ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako.

1527:15 Mwa 10:7; Yer 25:22; 1Fal 10:22; Ufu 18:12“ ‘Watu wa Dedani27:15 Yaani Rhodes. walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo.

1627:16 Amu 10:6; Isa 7:1-8; Kut 28:18; 39:11; Eze 28:13; 16:10; Ay 28:18“ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe27:16 Yaani marijani, jiwe laini la pwani au baharini, kama mawe ya chokaa. na akiki nyekundu.

1727:17 Amu 11:33; Mdo 12:20; Mwa 43:11“ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea.

1827:18 Mwa 14:15; Eze 47:16-18“ ‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari.

1927:19 Kut 30:24; Mwa 10:2, 27“ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai.

2027:20 Mwa 10:7“ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi.

2127:21 Mwa 25:13; Isa 60:7; 2Nya 9:14; Isa 21:17“ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.

2227:22 1Fal 10:1-2; Isa 60:8; Mwa 43:11; Za 72:10; Ufu 18:12“ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu.

2327:23 Mwa 11:26; 2Fal 19:12; Isa 37:12; Mwa 10:22; Hes 24:24“ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe. 24Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara.

2527:25 Mwa 10:4; Isa 2:16; Ufu 18:3“ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo

zinazokusafirishia bidhaa zako.

Umejazwa shehena kubwa

katika moyo wa bahari.

2627:26 Mwa 41:6; Za 48:7; Yer 18:7Wapiga makasia wako wanakupeleka

mpaka kwenye maji makavu.

Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande

katika moyo wa bahari.

2727:27 Mit 11:4; Eze 28:8Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako,

mabaharia wako, manahodha wako,

mafundi wako wa meli,

wafanyabiashara wako na askari wako wote,

na kila mmoja aliyeko melini

atazama kwenye moyo wa bahari

siku ile ya kuvunjika kwa meli yako.

2827:28 Yer 49:21; Eze 26:15Nchi za pwani zitatetemeka

wakati mabaharia wako watakapopiga kelele.

2927:29 Ufu 18:17Wote wapigao makasia

wataacha meli zao,

mabaharia wote na wanamaji wote

watasimama pwani.

3027:30 Yos 7:6; Yer 6:26; Ufu 18:17-19; Mao 2:10Watapaza sauti zao

na kulia sana kwa ajili yako;

watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao

na kujivingirisha kwenye majivu.

3127:31 Isa 16:9; Ay 3:20; Es 4:1; Law 13:40; Ay 1:20; Isa 3:17; Yer 48:37; Isa 22:12; Mao 2:10; Eze 7:16Watanyoa nywele zao kwa ajili yako,

nao watavaa nguo za magunia.

Watakulilia kwa uchungu wa moyo

na kwa maombolezo makuu.

3227:32 Eze 19:1; 26:17; Isa 23:1-6Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako,

watafanya maombolezo kukuhusu wakisema:

“Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro,

katika moyo wa bahari?”

3327:33 Eze 28:4-5Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini,

ulitosheleza mataifa mengi;

kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako

ulitajirisha wafalme wa dunia.

3427:34 Za 9:4Sasa umevunjavunjwa na bahari,

katika vilindi vya maji,

bidhaa zako na kundi lako lote

vimezama pamoja nawe.

3527:35 Eze 26:15; Law 26:32; Ay 18:20; Eze 32:10Wote waishio katika nchi za pwani

wanakustaajabia;

wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu,

nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.

3627:36 Yer 18:16; Sef 2:15; Eze 26:21; Za 37:10; Yer 19:8; 49:17; 50:13Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka;

umefikia mwisho wa kutisha

nawe hutakuwepo tena.’ ”