Ezekieli 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 24:1-27

Chungu Cha Kupikia

124:1 Eze 8:1; 26:1; 29:17Katika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi, neno la Bwana likanijia kusema: 224:2 2Fal 25:1; Yer 52:4; Isa 30:8; Hab 2:2; Yer 39:1“Mwanadamu, weka kumbukumbu ya tarehe hii, tarehe hii hasa, kwa kuwa mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu kwa jeshi siku hii ya leo. 324:3 Za 78:2; Eze 17:2; 11:3-6; 11:3Iambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke

na umimine maji ndani yake,

424:4 Eze 11:7Weka vipande vya nyama ndani yake,

vipande vyote vizuri,

vya paja na vya bega.

Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri;

524:5 Isa 34:12; Yer 52:10, 24-27; Mik 3:2-3chagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.

Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;

chochea mpaka ichemke

na uitokose hiyo mifupa ndani yake.

624:6 Eze 22:2; Ay 6:27; Nah 3:10; Oba 1:11; Eze 16:23; Yoe 3:3; Eze 11:11“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu,

ole wa sufuria ambayo sasa

ina ukoko ndani yake,

ambayo ukoko wake hautoki.

Kipakue kipande baada ya kipande,

bila kuvipigia kura.

724:7 Law 17:13; Kum 12:16“ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:

huyo mwanamke aliimwaga

juu ya mwamba ulio wazi;

hakuimwaga kwenye ardhi,

ambako vumbi lingeifunika.

824:8 Mt 7:2Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,

nimemwaga damu yake

juu ya mwamba ulio wazi,

ili isifunikwe.

924:9 Eze 24:6; Nah 3:1; Hab 2:12“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu!

Mimi nami nitalundikia kuni nyingi.

10Kwa hiyo lundika kuni

na uwashe moto.

Pika hiyo nyama vizuri,

changanya viungo ndani yake,

na uiache mifupa iungue kwenye moto.

1124:11 Yer 21:10; Eze 22:15Kisha teleka sufuria tupu kwenye makaa

mpaka iwe na moto sana na shaba yake ingʼae,

ili uchafu wake upate kuyeyuka

na ukoko wake upate kuungua na kuondoka.

12Imezuia juhudi zote,

ukoko wake mwingi haujaondoka,

hata ikiwa ni kwa moto.

1324:13 Mao 1:9; Zek 6:8; Eze 5:13; 8:18; Isa 22:14; Yer 6:28-30; Eze 16:18“ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutoka kwenye huo uchafu wako, hutatakasika tena mpaka ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua.

1424:14 Zek 8:14; Hes 23:19; Isa 3:11; Eze 18:30; Isa 22:14; Hes 11:23; Ay 27:22“ ‘Mimi Bwana nimesema, wakati umewadia wa mimi kutenda. Mimi sitazuia, mimi sitaona huruma wala sitapunguza hasira yangu, Utahukumiwa sawasawa na mwenendo na matendo yako, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Kifo Cha Mke Wa Ezekieli

15Neno la Bwana likanijia kusema: 1624:16 Yer 13:17; 16:5; Za 39:10; 84:1; Mao 2:4; Yer 22:10“Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote. 1724:17 Yer 16:7; Hes 20:29; Isa 3:20; 20:2; 20:2; Law 13:45Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.”

1824:18 Eze 12:7Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa.

1924:19 Eze 12:9; 37:18Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?”

20Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema: 2124:21 Za 27:4; Yer 7:14; Eze 23:25; Hos 9:12-16; Mal 2:12; Law 26:19, 31‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga. 2224:22 Yer 16:7; Law 13:45Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji. 2324:23 Kut 33:4; Ay 27:15; Za 78:64; Kut 28:39; Isa 3:20Mtajifunga vilemba vichwani mwenu na kuvaa viatu vyenu miguuni mwenu. Hamtaomboleza au kulia, lakini mtadhoofika kwa sababu ya dhambi zenu na kulia kwa uchungu kila mtu na mwenzake. 2424:24 Isa 20:3; Eze 4:3; Yn 13:19; Eze 12:11Ezekieli atakuwa ishara kwenu, mtafanya kama yeye alivyofanya. Wakati jambo hili litakapotokea, mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.’

2524:25 Kum 28:32; Yer 11:22; Za 20:4; Mao 2:4“Nawe, mwanadamu, siku ile nitakapoondoa ngome yao iliyo furaha yao na utukufu wao, kitu cha kupendeza macho yao, kile kilicho shauku ya mioyo yao, wana wao na binti zao vilevile, 2624:26 1Sam 4:12; Ay 1:15-19siku hiyo atakayetoroka atakuja kuwapasha habari. 2724:27 Eze 3:26; 33:22; Dan 10:15Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.”