Ezekieli 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 22:1-31

Dhambi Za Yerusalemu

122:1 Hab 2:12; Hos 4:2; Eze 16:2; 23:36; 24:6Neno la Bwana likanijia kusema: 222:2 Eze 24:6, 9; Hos 4:2; Nah 3:1; Hab 2:12; Eze 16:2; 23:36“Mwanadamu, je, wewe utauhukumu? Je, utauhukumu huu mji umwagao damu? Basi uujulishe juu ya matendo yake yote ya machukizo 322:3 Eze 23:45; 24:2; Mik 6:16uuambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee mji ule ujileteao maangamizi wenyewe kwa kumwaga damu ndani yake na kujinajisi wenyewe kwa kutengeneza sanamu, 422:4 2Fal 21:16; Eze 5:14; 21:25; Za 44:13-14; Dan 9:16; Za 137:3umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote. 522:5 Isa 22:2Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, Ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia.

622:6 Isa 1:23; Eze 11:6; 18:10; 33:25“ ‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu. 722:7 Kum 27:16; Mik 7:6; Kut 22:21-22; Kum 5:16; Kut 23:9Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane. 822:8 Kut 20:8; Law 19:30; Eze 23:38-39Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu. 922:9 Law 19:16; Eze 18:11; Hos 4:10-14; Isa 59:3; Eze 23:29Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati. 1022:10 Law 12:2; 18:8; 1Kor 5:1Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa si safi. 1122:11 Mwa 11:31; Law 18:15; 18:9; 2Sam 13:14; Yer 5:8; Eze 18:9Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti wa baba yake hasa. 1222:12 Kut 18:21; Amo 5:12; Law 19:13; Kum 16:19; Za 26:10; Isa 5:23; 17:10Ndani yako watu hupokea rushwa ili kumwaga damu, mnapokea riba na faida ya ziada na kupata faida isiyokuwa halali kutoka kwa jirani ili kupata faida kubwa kupita kiasi. Nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mwenyezi.

1322:13 Eze 21:17; Hes 24:10; Isa 33:15; Eze 6:11“ ‘Hakika nitapiga makofi kwa ajili ya faida isiyo halali uliyojipatia na kwa damu uliyoimwaga ndani yako. 1422:14 Eze 17:24; 21:7; 24:14; 1Kor 10:22; Za 76:7; Yoe 2:11Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokushughulikia? Mimi Bwana nimesema na nitalifanya. 1522:15 Kum 4:27; Zek 7:14; Eze 16:41; 23:27; Law 26:33Nitakutawanya miongoni mwa mataifa na kukutapanya katika nchi mbalimbali nami nitakomesha unajisi wako. 1622:16 Za 9:16; Eze 6:7Ukiisha kunajisika mbele ya mataifa, utajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

17Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 1822:18 Za 119:119; Isa 1:22; Yer 6:28-30; Isa 48:10“Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa kwangu takataka ya chuma, wote kwangu wamekuwa shaba, bati, chuma na risasi iliyoachwa kalibuni. Wao ni taka ya madini ya fedha tu. 1922:19 Za 119:119Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa kuwa wote mmekuwa takataka ya chuma, nitawakusanya Yerusalemu. 2022:20 Hos 8:10; Mal 3:2Kama vile watu wakusanyavyo fedha, shaba, chuma, risasi na bati kalibuni ili kuyeyusha kwa moto mkali, ndivyo nitakavyowakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu kuwaweka ndani ya mji na kuwayeyusha. 2122:21 Isa 40:7; Za 68:2; Eze 21:31Nitawakusanya na kupuliza juu yenu moto wa hasira yangu na ghadhabu yangu nanyi mtayeyushwa ndani ya huo mji. 2222:22 Isa 1:25; 64:7; Eze 20:8; 7:8Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi Bwana nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’ ”

23Neno la Bwana likanijia tena kusema: 2422:24 Eze 24:13“Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijapata mvua wala manyunyu katika siku ya ghadhabu.’ 2522:25 Hos 9:6; Yer 11:9; 15:8; 18:21; 6:13; Mdo 20:29Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake. 2622:26 Hos 9:7-8; Sef 3:4; 1Sam 2:29; Eze 44:23; 42:20; Law 10:10; Hag 2:11-14; Mal 2:7-8; Law 20:25Makuhani wake wameihalifu sheria yangu na kunajisi vitu vyangu vitakatifu, hawatofautishi kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida. Wanafundisha kuwa hakuna tofauti kati ya vitu vilivyo najisi na visivyo najisi, nao wanafumba macho yao katika kutunza Sabato zangu, hivyo katikati yao nimetiwa unajisi. 2722:27 Mwa 37:24; Yer 12:2; 26:10; Mt 7:15; Eze 34:2-3; Isa 1:23Maafisa wake walioko ndani yake ni kama mbwa mwitu wararuao mawindo yao, wanamwaga damu na kuua watu ili kupata faida ya udhalimu. 2822:28 Eze 13:6-10; Mao 2:14; 4:13; Eze 21:29; 13:2-7Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo,’ wakati Bwana hajasema. 2922:29 Yer 5:26; Kut 22:21; 23:9; Isa 5:7; Za 106:23Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyangʼanyi, wanawatenda jeuri maskini na wahitaji na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki.

3022:30 Eze 13:5; Za 106:23; Isa 64:7“Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, ambaye angejenga ukuta na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka kwa ajili ya watu wa nchi ili nisije nikaiangamiza, lakini sikumwona mtu yeyote. 3122:31 Eze 16:43; 9:10; Rum 2:8; Kut 32:10; Isa 30:27; Mao 4:11; Eze 7:8-9Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwateketeza kwa moto wa hasira yangu, nikiyaleta juu ya vichwa vyao yale yote waliyotenda, asema Bwana Mwenyezi.”