Ezekieli 21 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 21:1-32

Babeli, Upanga Wa Mungu Wa Hukumu

121:1 Eze 20:1Neno la Bwana likanijia kusema: 221:2 Yer 11:12; Eze 20:46; Amo 7:16; Eze 9:6; 13:17“Mwanadamu, uelekeze uso wako juu ya Yerusalemu na uhubiri dhidi ya mahali patakatifu. Tabiri dhidi ya nchi ya Israeli 321:3 Yer 21:13; 47:6-7; Ay 9:22; Isa 27:1; Eze 14:21uiambie: ‘Hili ndilo Bwana asemalo: Mimi niko kinyume nawe. Nitautoa upanga wangu kwenye ala yake na kumkatilia mbali mwenye haki na mwovu. 421:4 Eze 20:47; Law 26:25; Yer 25:27Kwa sababu nitamkatilia mbali mwenye haki na mwovu, upanga wangu utakuwa wazi dhidi ya kila mmoja kuanzia kusini mpaka kaskazini. 521:5 Eze 20:47-48; Isa 45:23; 34:5Ndipo watu wote watajua ya kuwa Mimi Bwana nimeutoa upanga wangu kwenye ala yake, nao hautarudi humo tena.’

621:6 Isa 22:4; Yer 30:6; Eze 9:4“Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi. 721:7 Yer 47:3; Eze 7:17; Ay 23:2; Yos 7:5; Eze 22:14; Za 6:2; Ay 11:16Nao watakapokuuliza, ‘Kwa nini unalia kwa uchungu?’ Utasema hivi, ‘Kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila moyo utayeyuka na kila mkono utalegea, kila roho itazimia na kila goti litalegea kama maji.’ Habari hizo zinakuja! Hakika zitatokea, asema Bwana Mwenyezi.”

8Neno la Bwana likanijia, kusema: 921:9 Kum 32:41“Mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Upanga, upanga,

ulionolewa na kusuguliwa:

1021:10 Za 105:5-6; Isa 34:5-6; Kum 32:41umenolewa kwa ajili ya mauaji,

umesuguliwa ili ungʼae

kama umeme wa radi!

“ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unaidharau kila fimbo ya namna hiyo.

1121:11 Yer 46:4“ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa,

ili upate kushikwa mkononi,

umenolewa na kusuguliwa,

umewekwa tayari kwa mkono wa muuaji.

1221:12 Yer 31:19Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu,

kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu;

u dhidi ya wakuu wote wa Israeli.

Wametolewa wauawe kwa upanga

pamoja na watu wangu.

Kwa hiyo pigapiga kifua chako.

1321:13 Ay 9:23; 2Kor 8:2“ ‘Kwa maana upanga huu umejaribiwa na kuhakikishwa, itakuwaje basi fimbo ya ufalme ya Yuda inayoudharau kama haitakuwepo tena, bali itakuwa imeondolewa kabisa? asema Bwana Mwenyezi.’

1421:14 Hes 24:10; Eze 6:11; 30:24; 8:12“Hivyo basi, mwanadamu, tabiri

na ukapige makofi.

Upanga wako na upige mara mbili,

naam, hata mara tatu.

Ni upanga wa kuchinja,

upanga wa mauaji makuu,

ukiwashambulia kutoka kila upande.

1521:15 2Sam 17:10; Za 22:14Ili mioyo ipate kuyeyuka

na wanaouawa wawe wengi,

nimeweka upanga wa kuchinja

kwenye malango yao yote.

Lo! Umetengenezwa

umetemete kama umeme wa radi,

umeshikwa kwa ajili ya kuua.

1621:16 Eze 14:17Ee upanga, kata upande wa kuume,

kisha upande wa kushoto,

mahali popote makali yako

yatakapoelekezwa.

1721:17 Eze 22:13; 5:13; 14:17; 16:42Mimi nami nitapiga makofi,

nayo ghadhabu yangu itapungua.

Mimi Bwana nimesema.”

18Neno la Bwana likanijia kusema: 1921:19 Eze 14:21; 32:11; Yer 31:21“Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini. 2021:20 Yer 49:2; Amo 1:14; Kum 3:11Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamoni na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome. 2121:21 Mit 16:33; Hes 20:7; 23:23; Zek 10:2Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama. 2221:22 2Fal 25:1; Eze 4:2; Yer 51:14; 4:16; 32:24; Eze 26:9Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka vyombo vya kuvunjia boma, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka vyombo vya kuvunjia boma kwenye malango, kuweka jeshi kuzunguka na kufanya uzingiraji. 2321:23 Hes 5:15; Eze 17:19Itakuwa kama kupiga ramli kwa uongo kwa wale watu ambao wameapa kumtii yeye. Lakini mfalme wa Babeli atawakumbusha juu ya uovu wao na kuwachukua mateka.

24“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu enyi watu mmekumbusha uovu wenu kwa kuasi waziwazi, mkidhihirisha dhambi zenu katika yale yote mfanyayo, kwa kuwa mmefanya jambo hili, mtachukuliwa mateka.

2521:25 Eze 35:5; Mwa 13:13; Eze 22:4“ ‘Ee mtawala kafiri na mwovu wa Israeli, ambaye siku yako imewadia, ambaye wakati wako wa adhabu umefikia kilele chake, 2621:26 Isa 28:5; Yer 13:18; Isa 40:4; Mt 23:12; Za 75:7hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa na aliyekwezwa atashushwa. 2721:27 Mwa 49:10; Za 2:6; Hag 2:21-22; Yer 23:5-6; Eze 37:24Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya mpaka aje yule ambaye ndiye mwenye haki nao; yeye ndiye nitakayempa.’

2821:28 Mwa 19:38; Sef 3:8; Yer 12:12“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao.

“ ‘Upanga, upanga,

umefutwa kwa ajili ya kuua,

umesuguliwa ili kuangamiza

na unametameta kama umeme wa radi!

2921:29 Eze 22:28; 35:5; Yer 27:9Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako,

wanapobashiri uongo kwa ajili yako,

wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu,

wale walio waovu,

wale ambao siku yao imewadia,

wakati wa adhabu yao ya mwisho.

3021:30 Yer 47:6; Eze 16:3Urudishe upanga kwenye ala yake!

Katika mahali ulipoumbiwa,

katika nchi ya baba zako,

huko nitakuhukumu.

3121:31 Za 79:6; Eze 22:20-21; Yer 51:20-23; Za 18:15; Isa 11:4; Eze 16:39Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako

na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako;

nitakutia mikononi mwa watu wakatili,

watu stadi katika kuangamiza.

3221:32 Eze 20:47-48; 25:10; Mal 4:1Mtakuwa kuni za kuwashia moto,

damu yenu itamwagwa katika nchi yenu,

wala hamtakumbukwa tena;

kwa maana Mimi Bwana nimesema.’ ”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

以西結書 21:1-32

耶和華審判的刀

1耶和華對我說: 2「人子啊,你要面向耶路撒冷,開口斥責聖所,說預言斥責以色列3告訴以色列,耶和華這樣說,『看啊,我要與你為敵,我要拔刀出鞘,將你那裡的義人和惡人一同消滅。 4由於我要將你那裡的義人和惡人一同消滅,我的刀必出鞘從南到北殺向所有的人, 5使世人都知道我耶和華已拔刀出鞘,不再收回。』 6人子啊,你要在他們面前哀歎,要傷心欲絕地哀歎。 7如果他們問你為什麼哀歎,你就說因為有噩耗傳來,聽見的人都膽戰心驚、兩手發軟、精神萎靡、膝弱如水。災難來了,必很快發生。這是主耶和華說的。」

8耶和華對我說: 9「人子啊,你要說預言,告訴他們,主這樣說,

「『有一把刀,

有一把刀磨快擦亮了,

10磨利以行殺戮,

擦得亮如閃電。

我們豈能因我兒的權杖而快樂?這刀鄙視一切權杖。 11這刀已交給人去擦亮,好握在手中,這刀已磨快擦亮,預備交給屠殺的人。 12人子啊,號啕大哭吧,因為這刀要攻擊我的子民和所有以色列的首領,他們都要死於刀下。所以你要捶胸頓足。 13這刀必試驗他們,這刀所鄙視的權杖若不復存在,又怎麼辦呢?這是主耶和華說的。』

14「人子啊,你要拍掌對他們說預言,你要拿刀揮舞兩三次,預示這刀要從四面八方大肆殺戮, 15使他們嚇得肝膽俱裂,許多人倒在家門口。我已賜下這亮如閃電的刀,用來殺戮。 16刀啊,你要左砍右劈,橫掃四方。 17我也要拍掌,我的烈怒要平息。這是我耶和華說的。」

18耶和華對我說: 19「人子啊,你要為巴比倫王的刀畫出兩條進攻之路,兩條路要從一個地方出發,要在通往城邑的路口設路標。 20為刀畫一條路進攻亞捫拉巴城,再畫一條路進攻猶大的堅城耶路撒冷21巴比倫王會站在兩條路的岔口占卜,搖籤求問他的神像,察看祭牲的肝。 22他右手拿到的是攻打耶路撒冷的籤,於是他架起撞城錘,號令殺戮,高聲吶喊,用撞城錘攻打城門,建壘築臺圍攻城池。 23猶大人必認為這是虛假的占卜。他們曾向巴比倫王宣誓效忠,但巴比倫王要使他們想起自己的罪,並擄走他們。

24「所以,主耶和華說,『因為你們的過犯昭然若揭,使人想起你們的罪惡,你們的所作所為都顯出你們的罪過。因此,你們必遭擄掠。 25你這邪惡敗壞的以色列首領啊!你的結局到了,最終審判的日子來了。』 26主耶和華說,『取下你的禮帽,摘下你的冠冕吧,時局轉變了。要提拔卑微的,貶抑高貴的。 27毀滅,毀滅,我要毀滅這國,使它蕩然無存,直到那應得的人來到,我要把這國交給他。』

28「人子啊,你要說有關亞捫人及其恥辱的預言,告訴他們,主耶和華說,『有刀,有刀已出鞘,為要殺戮;它亮如閃電,要行毀滅。 29他們為你們看的異象是虛假的,所做的占卜謊話連篇,你們將與褻瀆的惡人一同被殺,因為他們的結局到了,最終審判的日子來了。 30你們要收刀入鞘,我要在你們的受造之處,在你們的出生之地審判你們, 31我要把烈怒倒在你們身上,將我的怒火噴在你們身上,把你們交在嗜殺成性的惡徒手中, 32你們必被當作柴焚燒,你們的血必流在自己的土地上,無人再記得你們。因為這是我耶和華說的。』」