Ezekieli 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 20:1-49

Israeli Waasi

120:1 Eze 8:1; 1:1-2; 21:1; Mwa 25:22Katika mwaka wa saba, mwezi wa tano siku ya kumi, baadhi ya wazee wa Israeli wakaja ili kutaka ushauri kwa Bwana, wakaketi mbele yangu.

2Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 320:3 Mwa 25:22; Eze 14:3; 1Sam 28:6; Amo 8:12; Mit 15:8; Mt 15:8; Isa 1:15“Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema Bwana Mwenyezi.’

420:4 Eze 22:2; 23:36; 16:2“Je, utawahukumu? Je, mwanadamu, utawahukumu? Basi uwakabili kwa ajili ya machukizo ya baba zao 520:5 Kum 7:6; Law 11:44; Kut 20:2; Kum 4:34; Mwa 14:22; Hes 14:30na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Siku ile nilipochagua Israeli, niliwaapia wazao wa nyumba ya Yakobo kwa mkono ulioinuliwa nami nikajidhihirisha kwao huko Misri. Kwa mkono ulioinuliwa niliwaambia, “Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” 620:6 Kut 3:8; Dan 8:9; Za 48:2; Dan 11:41; Kut 6:8; Kum 29:18Siku ile niliwaapia wao kwamba nitawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta katika nchi niliyowachagulia, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kupita zote. 720:7 Kut 20:2-4; Law 18:3; Eze 6:9; Kum 29:18Nami nikawaambia, “Kila mmoja wenu aondolee mbali sanamu za chukizo ambazo mmekazia macho, nanyi msijitie unajisi kwa sanamu za Misri. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”

820:8 Yer 11:10; Eze 16:26; Kut 32:7; Kum 9:7; Isa 63:10; Yer 7:26“ ‘Lakini waliniasi na hawakunisikiliza, hawakuondolea mbali sanamu za machukizo ambazo walikuwa wamezikazia macho, wala kuondolea mbali sanamu za Misri. Ndipo nikasema, nitawamwagia ghadhabu yangu na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko Misri. 920:9 Eze 36:22; 39:7; Kut 32:12; Hes 14:13; Isa 48:11Lakini kwa ajili ya Jina langu nilifanya kile ambacho kingelifanya lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa waliyoishi miongoni mwao na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli kwa kuwatoa katika nchi ya Misri. 1020:10 Kut 13:18Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani. 1120:11 Kut 20:1-23; Rum 10:5; Neh 9:13; Eze 18:9; Kum 4:7-8; Law 18:5Nikawapa amri zangu na kuwajulisha sheria zangu, kwa kuwa mtu anayezitii ataishi kwa hizo. 1220:12 Kut 31:13; Kum 5:12; Kut 20:10; Yer 17:22; Law 20:8Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi Bwana niliwafanya kuwa watakatifu.

1320:13 Za 78:40; Kum 9:8; Law 26:15; Hes 14:29; Za 95:8-10; Isa 56:6; Kut 32:10“ ‘Lakini watu wa Israeli waliniasi Mimi jangwani. Hawakufuata amri zangu, bali walikataa sheria zangu, ingawa mtu yule anayezitii ataishi kwa hizo sheria, nao walizinajisi Sabato zangu kabisa. Hivyo nilisema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwaangamiza huko jangwani. 1420:14 Eze 36:23; Isa 48:11Lakini kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kitalifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli. 1520:15 Hes 14:22-23, 28; Ebr 3:11; Kum 1:34; Za 106:26; 95:11Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba nisingewaingiza katika nchi niliyokuwa nimewapa, yaani, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi nzuri kuliko zote, 1620:16 Hes 16:39; Amo 5:26; Mdo 7:42-43; Yer 1:8; Amo 2:4; Hes 15:39kwa sababu walikataa sheria zangu na hawakufuata amri zangu na wakazinajisi Sabato zangu. Kwa kuwa mioyo yao iliandama sanamu zao. 1720:17 Za 78:38Lakini niliwahurumia wala sikuwaangamiza wala hakuwafuta kabisa jangwani. 1820:18 2Nya 30:7; Za 106; 39Niliwaambia watoto wao kule jangwani, “Msifuate amri za baba zenu wala kushika sheria zao au kujinajisi kwa sanamu zao. 1920:19 Kut 20:2; Kum 11:1; 5:32-33Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, fuateni amri zangu tena kuweni waangalifu kushika sheria zangu. 2020:20 Yer 17:22; Kut 20:10; 31:13Zitakaseni Sabato zangu ili ziwe ishara kati yangu nanyi. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”

2120:21 Yer 7:26; Hes 25:3; Eze 7:8“ ‘Lakini watoto hao wakaniasi: Hawakufuata amri zangu, wala hawakuwa waangalifu kushika sheria zangu, ingawa mtu anayezitii anaishi kwa hizo sheria, nao wakazinajisi Sabato zangu. Hivyo nikasema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko jangwani. 2220:22 Za 78:38Lakini nikauzuia mkono wangu na kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kingelifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli. 2320:23 Law 26:33; Kum 28:64; Za 106:27; Yer 15:4Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba ningewatawanya miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, 2420:24 Eze 2:3; 6:9; 18:6; Amo 2:4kwa sababu hawakutii sheria zangu lakini walikuwa wamekataa amri zangu na kuzinajisi Sabato zangu, nayo macho yao yakatamani sanamu za baba zao. 2520:25 Za 81:12; Rum 1:24-28; 2The 2:11; Isa 66:4Pia niliwaacha wafuate amri ambazo hazikuwa nzuri na sheria ambazo mtu hawezi kuishi kwa hizo sheria. 2620:26 Law 20:2-5; 2Fal 17:17; Eze 16:20-21; Law 18:21Nikawaacha wanajisiwe kwa matoleo yao, kuwatoa wazaliwa wao wa kwanza kafara kwa sanamu, yaani, kule kuwapitisha wazaliwa wao wa kwanza kwenye moto, nipate kuwajaza na hofu ili wajue kwamba Mimi ndimi Bwana.’

2720:27 Hes 15:30; Rum 1:23; 2:24; Eze 18:24; Za 78:57“Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi: 2820:28 Neh 9:23; Za 78:55-58; Yer 19:13; Eze 6:13; Yer 2:7; 3:6Nilipowaleta katika nchi ile ambayo nilikuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima chochote kirefu au mti wowote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji. 29Ndipo nikawaambia: Ni nini maana yake hapa mahali pa juu pa kuabudia miungu mnapopaendea?’ ” (Basi jina la mahali pale panaitwa Bama20:29 Bama maana yake ni mahali pa juu pa kuabudia miungu. hata hivi leo.)

Hukumu Na Kurudishwa

3020:30 Amu 2:16-19; Yer 16:12“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, mtajinajisi kama vile baba zenu walivyofanya na kutamani vinyago vyao vya machukizo? 3120:31 Mit 1:27-28; Eze 16:20; Amo 8:12; Zek 7:13; Za 106:37-39; Yer 7:31Mnapotoa matoleo yenu, yaani, wana wenu kafara katika moto, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi siku hii ya leo. Je, niulizwe neno na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, mimi sitaulizwa neno na ninyi.

3220:32 Eze 11:5“ ‘Lile lililoko mioyoni mwenu kamwe halitatokea, mnaposema, “Tunataka tuwe kama mataifa mengine, kama watu wengine wa dunia, wanaotumikia miti na mawe.” 3320:33 Yer 21:5; Eze 25:16; 16:27Hakika kama niishivyo asema Bwana Mwenyezi, nitatawala juu yenu kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa. 3420:34 2Kor 6:17; Yer 44:6; Mao 2:4; Kum 30:4; Isa 27:12-13; 31:3Nitawatoa toka katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlikotawanywa, kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa. 3520:35 1Sam 12:7; Ay 22:4; Eze 19:13; Yer 2:35Nitawaleta katika jangwa la mataifa na huko nitatekeleza hukumu juu yenu uso kwa uso. 3620:36 Hes 14:28-30; 1Kor 10:5-10; Hes 11:1-35Kama nilivyowahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, ndivyo nitakavyowahukumu ninyi, asema Bwana Mwenyezi. 3720:37 Law 27:32; Yer 33:13; Eze 16:62Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa Agano. 3820:38 Eze 34:17-22; Amo 9:9-10; Hos 2:14; Ebr 4:3; Za 95:11; Eze 13:9; Zek 13:8-9Nitawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi yangu. Ingawa nitawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

3920:39 Yer 44:25; Isa 1:13; Amo 4:4; Mit 21:27; Kut 20:7; Eze 13:19; 43:7“ ‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu. 4020:40 Isa 60:7; 56:7; Mal 3:4; Zek 8:20; Rum 12:1; Eze 17:22; 34:14Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema Bwana Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote. 4120:41 Eze 28:25; 36:23; Isa 5:16; 2Kor 6:17; 2:14; Kum 30:4Nitawakubali ninyi kama uvumba wenye harufu nzuri wakati nitakapowatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlipokuwa mmetawanyika, nami nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwenu na machoni mwa mataifa. 4220:42 Eze 38:23; Yer 23:8; Eze 36:24; Yer 30:3; Eze 34:13; 34:27Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, nchi niliyokuwa nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu. 4320:43 Eze 16:61; Law 26:39; Eze 6:9; Hos 5:15Hapo ndipo nitakapokumbuka mwenendo wenu na matendo yenu yote ambayo kwayo mlijitia unajisi, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya maovu yote mliyokuwa mmetenda. 4420:44 Za 109:21; Isa 43:25; Eze 24:24; 36:32Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Bwana, nitakaposhughulika nanyi kwa ajili ya Jina langu na wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, ee nyumba ya Israeli, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Unabii Dhidi Ya Kusini

45Neno la Bwana likanijia kusema: 4620:46 Eze 21:2; Amo 7:16; Isa 30:6; Yer 13:17-19“Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri juu ya upande wa kusini na utoe unabii juu ya msitu wa Negebu. 4720:47 Yer 21:14; Isa 13:8; Eze 21:4; 2Fal 19:23; Isa 9:18-19; Eze 19:14Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno la Bwana. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo. 4820:48 Yer 7:20; Eze 21:5, 32; 23:25Kila mmoja ataona kuwa mimi Bwana ndiye niliyeuwasha huo moto, nao hautazimwa.’ ”

4920:49 Amu 14:12; Yn 16:24-25; Eze 4:14; Za 78:2; Eze 12:9; Mt 13:13Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’ ”