Ezekieli 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 2:1-10

Wito Wa Ezekieli

12:1 Dan 10:11; Mdo 26:16; Ay 25:6; Za 8:4; Eze 1:26; Mdo 9:6; 14:10Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 22:2 Eze 3:24; Dan 8:18; Amu 13:25Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami.

32:3 Yer 3:25; Eze 24:3; 20:8-24Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 42:4 Kut 32:9; Isa 9:9; Eze 3:7; Amo 7:15Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema Bwana Mwenyezi.’ 52:5 Eze 3:11; 3:27; Yn 15:22; Eze 33:33; Yer 5:3Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. 62:6 1Pet 3:14; Yer 1:8, 17; Hes 33:55; Mik 7:4Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi. 72:7 Yer 7:27; 42:21; Eze 3:10-11; Mt 28:20Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi. 82:8 Isa 8:11; 50:5; Ufu 10:9; Za 81:10; Hes 20:10-13; Yer 15:16Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiwe mwenye kuasi kama hiyo nyumba ya kuasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.”

92:9 Eze 8:3; Yer 1:9; Za 40:7; Yer 36:4; Ufu 5:1-5; 10:8-10Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na ukurasa wa kitabu, 102:10 Isa 3:11; Ufu 8:13ambao aliukunjua mbele yangu. Pande zote mbili ulikuwa umeandikwa maneno ya maombolezo, vilio na ole.