Ezekieli 19 – NEN & HTB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 19:1-14

Maombolezo Kwa Ajili Ya Wakuu Wa Israeli

119:1 Yer 7:29; 2Nya 24:6; Eze 26:17; Yer 9:10, 20; Eze 27:32; 28:12“Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli 219:2 Hes 23:24; Mwa 49:9na useme:

“ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike

miongoni mwa simba!

Alilala katikati ya wana simba

na kulisha watoto wake.

319:3 Eze 19:6; 2Fal 23:31, 32Alimlea mmoja wa watoto wake,

naye akawa simba mwenye nguvu.

Akajifunza kurarua mawindo

naye akala watu.

419:4 2Nya 36:4; Mao 4:20; Ay 41:2; 2Fal 23:33-34Mataifa wakasikia habari zake,

naye akanaswa katika shimo lao.

Wakamwongoza kwa ndoana

mpaka nchi ya Misri.

519:5 2Fal 23:34; Mwa 49:9“ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki,

nayo matarajio yake yametoweka,

akamchukua mwanawe mwingine

na kumfanya simba mwenye nguvu.

619:6 Yer 22:13; 2Nya 36:9; 2Fal 24:9Alizungukazunguka miongoni mwa simba,

kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu.

Akajifunza kurarua mawindo

naye akala watu.

719:7 Eze 29:10; 30:12Akabomoa ngome zao

na kuiharibu miji yao.

Nchi na wote waliokuwa ndani yake

wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake.

819:8 2Fal 24:2, 11; Mao 4:20; Eze 12:13; 2Fal 24:11Kisha mataifa wakaja dhidi yake

kutoka sehemu zilizomzunguka.

Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake,

naye akanaswa katika shimo lao.

919:9 2Fal 25:7; 24:15; 2Nya 36:6; 2Fal 19:28; Zek 11:3Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu

na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli.

Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake

hakukusikika tena

katika milima ya Israeli.

1019:10 Za 80:8-11; Eze 15:2; Yer 17:8; Mwa 49:22“ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu

katika shamba lako la mizabibu

uliopandwa kando ya maji,

ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi

kwa sababu ya wingi wa maji.

1119:11 Eze 31:3; Dan 4:11Matawi yake yalikuwa na nguvu,

yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.

Ulikuwa mrefu kupita miti mingine

katikati ya matawi manene;

ulionekana kwa urahisi

kwa ajili ya urefu wake

na wingi wa matawi yake.

1219:12 Kum 29:28; Eze 17:10; Hos 13:15; Isa 27:11; Eze 28:17; Mwa 41:6Lakini ulingʼolewa kwa hasira kali

na kutupwa chini.

Upepo wa mashariki uliufanya usinyae,

matunda yake yakapukutika,

matawi yake yenye nguvu yakanyauka

na moto ukayateketeza.

1319:13 Eze 20:35; Hos 2:14; 2:3Sasa umepandwa jangwani

katika nchi kame na ya kiu.

1419:14 Amu 9:15; Eze 20:47; 15:4Moto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwa

na kuteketeza matunda yake.

Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake

lifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’

Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”

Het Boek

Ezechiel 19:1-14

1Ge moet een klaagzang aanheffen over de vorsten van Israël, en 2zeggen: Wat een prachtleeuwin was uw moeder Onder de leeuwen; Liggend tussen haar jongen, Bracht zij haar welpen groot. 3Een van haar welpen voedde zij op: Een echte jonge leeuw! Hij leerde zijn prooi zoeken, Mensen verscheurde hij. 4Maar men riep volken tegen hem op, En in hun kuil werd hij gevangen; Ze sleurden hem met haken Naar het land van Egypte. 5Toen zij zag, dat haar wachten vergeefs, En haar hoop was vervlogen, Koos zij een van haar welpen, Bestemde hem tot jonge leeuw. 6Met leeuwen ging hij samenleven: Een echte jonge leeuw! Hij leerde zijn prooi zoeken, Mensen verscheurde hij. 7Hij maakte veel weduwen En ontvolkte hun steden; Het land en zijn bewoners stonden versteld Van zijn dreigend gebrul! 8Maar volken spanden hem strikken Aan alle kanten; Wierpen hun net over hem heen, In hun kuil werd hij gevangen. 9Ze zetten hem in een kooi, Sleurden hem met haken voor Babels koning, de burchten in, Opdat zijn gebrul niet meer zou worden gehoord Op Israëls bergen. 10Uw moeder stond als een wingerd In uw wijngaard aan het water geplant; Ze was bloeiend en vruchtbaar Door de rijkdom van water. 11Ze kreeg een krachtige tak Tot konings-schepter, Wiens top zich tot in de wolken verhief, Die opviel door zijn hoogte en talrijke twijgen. 12Maar in woede werd zij uitgerukt, Op de grond geworpen. Een oostenwind verdroogde haar: Haar vrucht viel af. Haar krachtige tak verdorde: Het vuur verslond hem. 13Nu staat ze geplant in de steppe, In een streek van dorheid en dorst; 14Er schoot een vlam uit de tak, Die haar ranken en vruchten verteerde. Nu heeft ze geen krachtige tak meer over, Geen konings-schepter meer! Dit is een klaaglied, dat men nog altijd jammert.