Ezekieli 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 17:1-24

Tai Wawili Na Mizabibu

117:1 Amu 14:12; Eze 20:49Neno la Bwana likanijia kusema: 217:2 Amu 14:12; Eze 20:49“Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo. 317:3 Kum 28:49; Dan 7:4; Yer 22:23; 49:22; Hos 8:1Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi, 417:4 Isa 10:33akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi.

517:5 Kum 8:7-9; Isa 15:7; Eze 31:5; Isa 44:5“ ‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi, 617:6 Isa 18:5; Ay 5:3nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi.

717:7 Eze 31:4“ ‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji. 817:8 Ay 18:19; Mal 4:1Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.’

917:9 Yer 42:10; Amo 2:9“Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, utastawi? Je, hautangʼolewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuungʼoa na mizizi yake. 1017:10 Ay 1:19; Hos 12:1; Yud 12; Eze 15:4; Hos 13:15Hata kama utapandwa pengine, Je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani, hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’ ”

11Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 1217:12 Eze 12:9; 2Fal 24:15; Kum 21:10; 2Nya 36:10; Eze 24:19“Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli. 1317:13 2Nya 36:13; 2Fal 24:17; Kut 23:32; Isa 3:2Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi, 1417:14 Eze 29:14ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake. 1517:15 Yer 52:3; Kum 17:16; Isa 30:2; Za 56:7; Kum 17:16; Yer 34:3; Eze 29:16Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?

1617:16 Yer 52:11; Eze 12:13; Yer 32:5; 2Fal 24:17“ ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake. 1717:17 Yer 37:7; Eze 4:2; Isa 36:6; Mao 4:17; Eze 29:6-7Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia chochote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi. 1817:18 2Fal 10:15; 1Nya 29:24Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.

1917:19 Yer 7:9; Hos 10:4; Eze 16:59; 21:23“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja. 2017:20 Yos 10:16-18; Mhu 9:12; Eze 12:13; 32:3; 20:36; 15:8; Yer 2:35Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu. 2117:21 Eze 12:14; 2Fal 25:11; Law 26:33; Zek 2:5-6; 2Fal 25:5Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesema.

Hatimaye Israeli Kutukuzwa

2217:22 Isa 2:2; 53:2; Yer 23:5; 2Fal 19:30; Isa 4:2; Eze 20:40; 40:2; 43:12“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana. 2317:23 Dan 4:12; Mt 13:32; Mik 4:1; Yer 31:12; Isa 27:6; 2:2; Za 92:12; Hos 14:5-7Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake. 2417:24 Za 96:12; Isa 2:13; Eze 19:12; 21:26; 22:14; Amo 9:11; Za 52:5; Hes 17:8; Dan 5:21; 1Sam 2:7-8; Eze 37:13Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi.

“ ‘Mimi Bwana nimesema, nami nitatenda.’ ”