Ezekieli 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 15:1-8

Yerusalemu Mzabibu Usiofaa

1Neno la Bwana likanijia kusema: 215:2 Za 80:8-16; Yn 15:2; Yer 2:21; Isa 27:2-6; 5:1-7; Hos 10:1“Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora zaidi kuliko tawi la mti mwingine wowote ndani ya msitu? 315:3 Yer 13:10; Isa 22:23Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza chochote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuningʼinizia vitu kutokana na huo mti wake? 415:4 Eze 17:3-10; Yn 15:6; Eze 19:14Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? 5Kama haukufaa kitu chochote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa chochote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuunguza?

6“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati kwa ajili ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu waishio Yerusalemu. 715:7 Yer 21:10; Law 26:17; Za 34:16; Isa 24:18; Amo 9:1-4; Eze 14:8; 5:2-4Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimi Bwana. 815:8 Eze 14:13; 17:20; Amo 5:19; Eze 18:24Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asema Bwana Mwenyezi.”