Ezekieli 14 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 14:1-23

Waabudu Sanamu Walaumiwa

114:1 Eze 8:1; 20:1Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. 2Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 314:3 Eze 7:19; Ufu 2:14; Isa 1:15; Eze 20:31; Mit 15:8; Eze 6:4“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote? 4Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Bwana nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu. 514:5 Ebr 3:12-19; Kum 32:15; Hos 5:7; Yer 2:11; Eze 16:45; Zek 11:8Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.’

614:6 Isa 2:20; 30:22; Neh 1:9; Yer 3:12; 35:15“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!

714:7 Kut 12:48; 20:10; Mt 6:24; Yer 2:13; Isa 8:14; Mwa 25:22; Hos 4:5“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimi Bwana nitamjibu mwenyewe. 814:8 Eze 15:7; Za 102:8; Hes 26:10; Eze 5:15; Yer 42:20; Hes 16:38Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumwadhibu na kumfanya ishara kwa watu. Nitamkatilia mbali kutoka watu wangu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

914:9 Yer 14:15; Isa 63:17; Yer 4:10; 2Nya 18:22; Zek 13:3; 1Fal 22:23“ ‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, Mimi Bwana nitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli. 10Watachukua hatia yao, nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake.

1114:11 Eze 48:11; 11:19-20; 37:23; Isa 13:19; 51:16“ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Ndipo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Hukumu Isiyoepukika

12Neno la Bwana likanijia kusema, 1314:13 Law 26:26; Eze 5:16; 5:16; 6:14; Mit 13:21; Eze 15:8“Mwanadamu, kama nchi itanitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikinyoosha mkono wangu dhidi yake kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao, 1414:14 Mwa 6:8-9; Dan 6:13; Ay 42:9; Eze 28:3; 18:20; 3:19hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asema Bwana Mwenyezi.

1514:15 Hes 21:6; Eze 5:17; Law 26:22“Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori, 1614:16 Mwa 19:29; Eze 18:20hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa.

1714:17 Law 26:25; Yer 25:27; Eze 25:13; 5:12; Yer 42:16“Au kama nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikiua watu wake na wanyama wao, 1814:18 Eze 14:14hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.

1914:19 Yer 14:12; Eze 38:22; Ufu 16:3-6; Eze 7:8; Isa 34:3“Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao, 2014:20 Eze 14:14hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.

2114:21 Eze 5:17; Amo 4:6-10; Ufu 6:8; Hes 33:4; Isa 31:8; 34:6; Eze 21:3; 2Sam 24:13“Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao! 2214:22 Eze 12:16; 20:43; Yer 41:16; Eze 31:16; 32:31Lakini watakuwepo wenye kuokoka, wana na binti wataletwa kutoka nje ya nchi hiyo. Watawajia ninyi, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya yale yote niliyoleta juu yake. 2314:23 Yer 22:8-9; Eze 8:6-18Mtafarijika wakati mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwa kuwa mtajua kwamba sikufanya lolote ndani yake bila sababu, asema Bwana Mwenyezi.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 14:1-23

斥责拜偶像的以色列人

1那时,几位以色列的长老到我这里来,坐在我面前。 2耶和华对我说: 3“人子啊,这些人在心里立起偶像,把导致犯罪的绊脚石放在自己面前,我岂能让他们来求问? 4你告诉他们,主耶和华这样说,‘任何以色列人若在心里立起偶像,把导致犯罪的绊脚石放在自己面前,又来求问先知,我耶和华必按他心中偶像的数目亲自用惩罚回答他, 5好夺回以色列人的心,他们都因为拜偶像而远离我。’

6“因此,你要告诉以色列人,主耶和华这样说,‘你们要悔改,离弃你们的偶像,离弃一切可憎之事。 7因为任何以色列人或是在以色列定居的外族人若背弃我,在心中树立偶像,把导致犯罪的绊脚石放在自己面前,又来向先知求问我的旨意,我耶和华必亲自用惩罚回答他。 8我必严惩他,使他成为众人的鉴戒和笑柄。我必将他从我的子民中铲除。这样,你们就知道我是耶和华。 9如果先知受迷惑说预言,那是我耶和华任他受迷惑,我必伸手惩治他,把他从我的以色列百姓中除灭。 10他们必担当自己的罪过,假先知与求问的人要担当同样的罪过。 11这样,以色列人便不再偏离我,不再犯罪玷污自己。他们要做我的子民,我要做他们的上帝。这是主耶和华说的。’”

12耶和华对我说: 13“人子啊,若有国家犯罪背叛我,我必伸手断绝他们的粮源,使饥荒遍地,毁灭人和牲畜。 14即使挪亚但以理约伯三人在那里,他们也只能因义行而自己得救。这是主耶和华说的。 15倘若我使猛兽在那里横行、肆虐,以致那里荒凉、人踪绝迹, 16纵然这三个义人在那里,我凭我的永恒起誓,他们也不能救自己的儿女,只能自己得救,那里却要荒凉。这是主耶和华说的。 17倘若我使刀剑临到那里,让刀剑横扫那里,毁灭人和牲畜, 18纵然这三个义人在那里,我凭我的永恒起誓,他们也不能救自己的儿女,只能自己得救。这是主耶和华说的。 19倘若我叫瘟疫在那里肆虐,在杀戮中倾倒我的烈怒,毁灭那里的人和牲畜, 20纵然挪亚但以理约伯在那里,我凭我的永恒起誓,他们也不能救自己的儿女,只能因义行而自己得救。这是主耶和华说的。

21“主耶和华说,‘我要把刀剑、饥荒、猛兽和瘟疫这四大刑罚降在耶路撒冷,毁灭人和牲畜。 22然而,其中仍有幸免的人带着儿女逃出来。他们会逃到你们这里,你们看见他们的所作所为,便会对我在耶路撒冷所降的一切灾难感到欣慰。 23你们看见他们的所作所为,就知道我不是无缘无故地惩罚耶路撒冷。’这是主耶和华说的。”