Esta 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Esta 10:1-3

Ukuu Wa Mordekai

110:1 Za 72:10; 97:1Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. 210:2 Es 8:15; Mwa 41:44Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi? 310:3 Dan 5:7; Mwa 41:40; Neh 2:10Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.