Danieli 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Danieli 5:1-31

Maandishi Ukutani

15:1 1Fal 3:15; Mk 6:21; Es 3:1; Yer 50:35; Dan 7:1; 8:1Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. 25:2 2Nya 36:10; Yer 52:19; Es 1:7; Mit 20:1; Isa 21:5; 2Fal 24:13; Es 2:14; Dan 1:2Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea. 3Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea. 45:4 Es 1:10; Ufu 9:20; Za 115:4-8; Amu 16:24; Hag 2:19; Za 135:15-18Walipokuwa wakinywa mvinyo, wakaisifu miungu ya dhahabu na fedha, ya shaba, chuma, miti na mawe.

5Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika. 65:6 Dan 4:5; Za 22:14; Nah 2:10; Ay 4:15; Isa 7:2; Eze 7:17Uso wa mfalme ukageuka rangi, naye akaogopa sana, kiasi kwamba magoti yake yaligongana na miguu yake ikalegea.

75:7 Isa 44:25; 47:13; Dan 4:6-7; Mwa 41:42; Dan 2:5-6, 48; 6:2-3; Mwa 41:8; Isa 19:3; 44:25; Yer 50:35; Es 10:3Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”

85:8 Dan 2:10, 27; 4:18; Mwa 41:8; 41:8; Kut 8:18Ndipo watu wote wa mfalme wenye hekima wakaingia, lakini hawakuweza kusoma yale maandishi wala kumwambia mfalme maana yake. 95:9 Za 48:5; Isa 21:4Basi Mfalme Belshaza akazidi kujawa na hofu, na uso wake ukageuka rangi zaidi. Wakuu wake wakapigwa na bumbuazi.

105:10 Neh 2:3; Dan 3:9Malkia5:10 Au: Mama yake mfalme. aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho! 115:11 Mwa 41:38; Dan 4:8-9; 1:17; 2:47-48; 2:22; Mwa 41:38; Dan 2:22Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi. 125:12 Dan 1:7; 6:3; Hes 12:8; Eze 28:3Mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alionekana kuwa na akili nyepesi, maarifa na ufahamu, pia uwezo wa kufasiri ndoto, kueleza mafumbo na kutatua matatizo magumu. Mwite Danieli, naye atakuambia maana ya haya maandishi.”

135:13 Es 2:5-6; Dan 6:13Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda? 14Nimesikia kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na kwamba una ufahamu, akili na hekima ya pekee. 155:15 Dan 4:18Watu wenye hekima na wasihiri waliletwa mbele yangu ili kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, lakini hawakuweza kunifafanulia. 165:16 Mwa 41:15; 42; Es 5:3; Dan 2:6; Mwa 41:15, 42Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.”

175:17 2Fal 5:16Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.

185:18 Yer 27:7; Dan 4:36; Yer 28:14; Dan 2:37-38“Ee mfalme, Mungu Aliye Juu Sana alimpa baba yako Nebukadneza utawala, ukuu, utukufu na fahari. 195:19 Dan 2:12-13; 3:6; Yer 25:9; Dan 4:22Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha. 205:20 Dan 4:30; Yer 13:18; Ay 40:12; Eze 31:10-11; Isa 14:12; Yer 43:10; Dan 8:8Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwa kiti chake cha ufalme na kuvuliwa utukufu wake. 215:21 Eze 17:24; Kut 9:14-16; Dan 4:16-17Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu, akala majani kama ngʼombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, mpaka alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala juu ya falme za wanadamu na kwamba humtawaza juu yao yeyote amtakaye.

225:22 Kut 10:3; 2Nya 33:23“Lakini wewe mwanawe, ee Belshaza, hukujinyenyekeza, ingawa ulifahamu haya yote. 235:23 Ufu 13:6; Isa 14:13; Hes 2:19; Yer 50:29; Ufu 9:20; Ay 12:10; Mdo 17:28; Yer 44:9; Ay 31:4; Za 115:4-8; Hab 2:19; Isa 13:11; Yer 10:23; 48:26Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake. 24Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno.

25“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa:

mene, mene, tekeli na peresi

265:26 Yer 27:7; Isa 13:9“Hii ndiyo maana ya maneno haya:

Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.

275:27 Za 62:9; Yer 6:30; Ay 6:2Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.

285:28 Isa 13:17; Yer 50:41-43; Dan 6:28; Yer 7:27Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”

295:29 Mwa 41:42; Dan 2:6Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.

305:30 Isa 21:9; Yer 51:31; 50:35Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa, 315:31 Yer 50:41; Dan 11:1; Isa 13:3naye Dario Mmedi akashika ufalme akiwa na miaka sitini na miwili.