Danieli 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Danieli 12:1-13

Nyakati Za Mwisho

112:1 Dan 10:13; Yud 9; Dan 9:12; Lk 10:20; Yer 17:13; Mt 24:21; Mk 13:19; Yer 30:7; Za 56:8; Kut 32:32“Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. 212:2 Isa 26:19; Yn 5:28-29; Mt 25:46; Yn 11:24Wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele, wengine kwa aibu na kudharauliwa milele. 312:3 Dan 11:33; Yn 5:35; Flp 2:15; Mit 4:18; 1Kor 15:42; Mt 13:43Wale wenye hekima watangʼaa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watangʼaa kama nyota milele na milele. 412:4 Isa 8:16; Ufu 22:10; Yer 5:1Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko, na maarifa yataongezeka.”

512:5 Dan 10:4Ndipo mimi Danieli nikaangalia, nako mbele yangu walisimama wengine wawili, mmoja katika ukingo huu wa mto, na mwingine ukingo wa pili wa mto. 612:6 Eze 9:2; Dan 8:13; Za 74:9Mmoja wao akasema na yule mtu aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, “Je, itachukua muda gani kabla mambo haya ya kushangaza hayajatimizwa?”

712:7 Dan 6:26; Ufu 10:5-7; Lk 21:24; Dan 8:24; 8:24; Ufu 11:2; Mwa 14:22Kisha mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, akainua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, nami nikamsikia akiapa kwa jina lake yeye aishiye milele, akisema, “Itakuwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.12:7 Wakati, nyakati mbili na nusu wakati maana yake mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka, yaani miaka mitatu na nusu. Nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimevunjwa kabisa, ndipo mambo haya yote yatakapotimizwa.”

8Nilisikia, lakini sikuelewa. Kwa hiyo nikauliza, “Bwana wangu, matokeo ya haya yote yatakuwa nini?”

912:9 Isa 29:11Akajibu, “Danieli, enenda zako, kwa sababu maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri mpaka wakati wa mwisho. 1012:10 Isa 1:25; Zek 13:9; Hos 14:9; Isa 32:7; Ufu 22:11; Dan 11:35Wengi watatakaswa, na kuondolewa mawaa na kufanywa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.

1112:11 Mk 13:14; Dan 8:11; 9:27; Mt 24:15; Kut 29:38; Ufu 11:2“Tangu wakati ule wa kukomeshwa dhabihu ya kila siku na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu, kutakuwako siku 1,290. 1212:12 Isa 30:18; Eze 4:5-6; Dan 8:14Amebarikiwa mtu yule atakayevumilia hadi kufikia mwisho wa hizo siku 1,335.

1312:13 Isa 57:2“Lakini wewe, enenda zako mpaka mwisho. Utapumzika, nawe ndipo mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.”