Ayubu 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 9:1-35

Hotuba Ya Tatu Ya Ayubu

Hakuna Mpatanishi

1Kisha Ayubu akajibu:

29:2 Za 143:2; Rum 3:20; Ay 4:17“Naam, najua hili ni kweli.

Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

39:3 Ay 9:32; 40:5; Za 44:21Ingawa mtu angetaka kushindana naye,

asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.

49:4 Mit 2:6; 8:6; Mhu 2:26; 2Nya 13:12; Isa 40:26; Ay 5:9; 12:13; Za 93:4; Dan 2:20Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.

Ni nani aliyempinga naye akawa salama?

59:5 Isa 13:13; Mik 1:4; Mt 17:20; Za 18:7Aiondoa milima bila yenyewe kujua

na kuipindua kwa hasira yake.

69:6 Hag 2:6; 2:21; Ebr 12:26; Isa 2:19-21; 2Sam 22:8Aitikisa dunia kutoka mahali pake

na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.

79:7 Yer 4:23; Eze 32:8; Isa 34:4; Sef 1:15; Yoe 2:2Husema na jua, nalo likaacha kuangaza;

naye huizima mianga ya nyota.

89:8 Mwa 1:1, 8; Isa 48:13; Ay 38:16; Za 77:19; Mit 8:28; Hab 3:15Yeye peke yake huzitandaza mbingu

na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.

99:9 Mwa 1:16; Ay 38:31; 32:22; Amo 5:8Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,9:9 Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu. na Orioni,9:9 Orioni ni kundi la nyota kubwa.

Kilimia,9:9 Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus). na makundi ya nyota za kusini.

109:10 Kum 6:22; Za 72:18; 136:4; Yer 32:20Hutenda maajabu yasiyopimika,

miujiza isiyoweza kuhesabiwa.

119:11 Ay 23:8-9; 35:14Anapopita karibu nami, siwezi kumwona;

apitapo mbele yangu, simtambui.

129:12 Hes 23:20; Isa 43:13; 14:27; Dan 2:21; Rum 9:20; Ay 11:10Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?

Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’

139:13 Hes 14:18; Ay 10:15; Za 78:38; Isa 3:11; 6:5Mungu hataizuia hasira yake;

hata jeshi kubwa la Rahabu9:13 Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo. lenye nguvu

linajikunyata miguuni pake.

149:14 Ay 9:3“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?

Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?

159:15 Ay 10:15; 13:19; 34:5-6; 40:5; 42:7; Mwa 18:25; 1Sam 24:12; Za 50:6; 96:13Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;

ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.

169:16 Ay 13:22; Rum 9:20-21Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,

siamini kama angenisikiliza.

179:17 Isa 38:13; 38:13; Yn 1:4; Za 10:10; 83:15; Ay 16:12; 30:16; 16:14; 2:3Yeye angeniangamiza kwa dhoruba

na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.

189:18 Ay 7:19; 10:1Asingeniacha nipumue

bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.

199:19 Ay 9:4; Neh 9:32; Yer 49:19Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!

Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?

209:20 Ay 9:15Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;

kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.

219:21 Mwa 6:9; Hes 11:15; Ay 7:15-16; 6:29; 10:1“Ingawa mimi sina kosa,

haileti tofauti katika nafsi yangu;

nauchukia uhai wangu.

229:22 Mhu 9:2-3; Eze 21:3; Ay 3:19Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema,

‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’

239:23 Hab 1:3; 1Pet 1:7; Ebr 11:36; Za 64:4Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,

yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.

249:24 Za 73:3; 73:12; Mhu 8:11; Mao 3:9; Ay 1:15, 17; 10:3; 40:8; Yer 12:1; Isa 41:20Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,

yeye huwafunga macho mahakimu wake.

Kama si yeye, basi ni nani?

259:25 Ay 7:6, 7; 10:20“Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;

zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.

269:26 Isa 18:2; Ay 39:29; Za 46:3; Hab 1:8Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,

mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.

279:27 Ay 7:11Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,

nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

289:28 Kut 20:7; 34:7; Ay 3:25; 7:21bado ninahofia mateso yangu yote,

kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

299:29 Ay 9:3, 15; Za 37:33Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,

kwa nini basi nitaabishwe bure?

309:30 Hos 13:12; Isa 1:15-18; Mal 3:2; Ay 31:7; 14:4, 17; 17:9; Yer 2:22Hata kama ningejiosha kwa sabuni

na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

319:31 Za 35:7; 40:2; 51:9; Yer 2:22; Nah 3:6; Mal 2:3; Ay 7:20wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi

kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

329:32 Rum 9:20; Mhu 6:10; Za 143:2; Hes 23:19“Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,

ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

339:33 1Sam 2:25; Ay 9:19Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu,

aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

349:34 Ay 6:4; 21:9; Za 39:10; 73:5; 32:4mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,

ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

359:35 Ay 7:15; 13:21; 7:11Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,

lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.