Ayubu 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 8:1-22

Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu

18:1 Mwa 25:2; Ay 18:1; 25:1Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:

28:2 Ay 6:26; 11:2; 2Nya 36:16“Hata lini wewe utasema mambo kama haya?

Maneno yako ni kama upepo mkuu.

38:3 Mwa 18:25; 2Nya 19:7; Kum 32:4; Ay 34:12; Dan 9:14Je, Mungu hupotosha hukumu?

Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?

48:4 Ay 1:5, 18Watoto wako walipomtenda dhambi,

aliwapa adhabu ya dhambi yao.

58:5 Ay 5:8; 11:13; 22:23Lakini ukimtafuta Mungu,

nawe ukamsihi Mwenyezi,

68:6 Za 7:6; Isa 58:9; Ay 5:24; 5:15; 22:27; Isa 65:24ikiwa wewe ni safi na mnyofu,

hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako,

na kukurudisha katika mahali pako pa haki.

78:7 Ay 21:13; 22:21; 36:11; Za 25:13; Yer 29:11; 31:17Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,

lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.

88:8 Kum 4:32; 32:7; Za 71:18; Ay 15:18“Ukaulize vizazi vilivyotangulia

na uone baba zao walijifunza nini,

98:9 Mwa 47:9; 2Nya 10:6; Za 39:5-6; 1Nya 29:15; Ay 7:6kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote,

nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.

108:10 Mt 1:8; 2:1-2; 4:1Je, hawatakufundisha na kukueleza?

Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

118:11 Ay 40:21; Kut 2:3; Isa 19:6; 35:7Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope?

Matete yaweza kustawi bila maji?

128:12 Isa 34:4; Yer 17:6; Za 129:6; Yak 1:10, 11; 1Pet 1:24Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa,

hunyauka haraka kuliko majani mengine.

138:13 Za 50:13; 112:10; Mit 10:28; Yer 15:9; Ay 11:20; 18:14; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu;

vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.

148:14 Ay 8:15; 27:18; Isa 59:5Lile analolitumainia huvunjika upesi;

lile analolitegemea ni utando wa buibui.

158:15 Ay 27:18; 8:12; Za 49:11; Mt 7:26-27Huutegemea utando wake, lakini hausimami;

huungʼangʼania, lakini haudumu.

168:16 Za 80:11; 37:35; Isa 16:5; Yer 11:16Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua,

ukieneza machipukizi yake bustanini;

17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe,

na kutafuta nafasi katikati ya mawe.

188:18 Ay 14:20; 7:10; Za 37:36; 103:16Unapongʼolewa kutoka mahali pake,

ndipo mahali pale huukana na kusema,

‘Mimi kamwe sikukuona.’

198:19 Za 113:7Hakika uhai wake hunyauka,

na kutoka udongoni mimea mingine huota.

208:20 Mwa 18:25; Ay 21:30; 1The 5:23-24; Za 37:24“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia,

wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.

218:21 Ay 5:22; Ezr 3:13; Isa 35:6; Za 47:5; 107:22Bado atakijaza kinywa chako na kicheko,

na midomo yako na kelele za shangwe.

228:22 Za 6:10; Eze 7:27; 1Sam 8:3; Mit 14:11; Ay 18:6Adui zako watavikwa aibu,

nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.”