Ayubu 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 7:1-21

Ayubu: Mateso Yangu Hayana Mwisho

17:1 Ay 14:6, 13-14; Isa 40:2; Law 25:50; Za 39:4; Mhu 3:1, 2; Ay 5:7“Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani?

Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa?

27:2 Law 19:13; Ay 14:1; Mhu 2:23; Ay 14:6Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni,

au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake,

37:3 Mhu 4:1; Mao 1:2, 16; Za 39:5; Mhu 1:14; Isa 16:9; Yer 9:1ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili,

nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku.

47:4 Kum 28:67; Ay 7:13-14Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’

Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko.

57:5 Ay 17:14; Za 38:5-7; Isa 1:6Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu,

ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha.

Ayubu Anamlilia Mungu

67:6 Za 39:5; 52:9; Isa 38:15; Ay 9:25; 13:15“Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma,

nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini.

77:7 Mhu 7:15; Yak 4:14; Ay 9:25; Za 78:39Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi;

macho yangu kamwe hayataona tena raha.

87:8 Isa 41:12; Mdo 20:25; Ay 20:9Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena;

utanitafuta, wala sitakuwepo.

97:9 Ay 30:15; 38:17; 2Sam 12:23; Za 39:13Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka,

vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini7:9 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. harudi tena.

107:10 Ay 18:21; 21:18; 27:21; Za 58:9; Yer 18:17; 19:8; Za 37:10; 104:35Kamwe harudi tena nyumbani mwake;

wala mahali pake hapatamjua tena.

117:11 Za 39:1, 9“Kwa hiyo sitanyamaza;

nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu,

nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.

127:12 Mwa 1:21; Eze 32:2-3; Ay 38:8-11; Isa 1:14Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini,

hata uniweke chini ya ulinzi?

137:13 Ay 7:11Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji,

nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu,

147:14 Ay 9:34; 3:26; Mwa 41:8ndipo wanitisha kwa ndoto

na kunitia hofu kwa maono,

157:15 1Fal 19:4; Yn 4:3; Ay 6:9; Ufu 9:6hivyo ninachagua kujinyonga na kufa,

kuliko huu mwili wangu.

167:16 Mwa 27:46; Za 62:9; 1Fal 19:4; Ay 10:1; Mhu 6:11Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi.

Niache; siku zangu ni ubatili.

177:17 Za 144:3; 8:4; Ebr 2:6; Ay 4:19“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki,

kwamba unamtia sana maanani,

187:18 Ay 23:10; 14:3; Za 139:23; 17:3; 26:2; 66:10; 73:14kwamba unamwangalia kila asubuhi

na kumjaribu kila wakati?

197:19 Ay 7:16; 9:18; 13:26; 14:6; 27:2; Za 139:7Je, hutaacha kamwe kunitazama,

au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?

207:20 Yer 7:19; Ay 6:4; 16:12; 35:6; Za 36:6Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini,

Ewe mlinzi wa wanadamu?

Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako?

Je, nimekuwa mzigo kwako?

217:21 Yer 31:34; Mwa 3:19; Ay 9:28; Ebr 1:3; Za 119:120; 7:5; 22:15; 90:3; 104:29; Isa 43:25Kwa nini husamehi makosa yangu

na kuachilia dhambi zangu?

Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini;

nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”